Wilson Gamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 808
- 878
Kwanza niwape pole walimu na pia wale wote waliohusika hadi kutufikisha hapa na kutupa uelewa kupitia wa elimu.Miaka ya 90 watu walisoma wakubwa lakini walikuwa watiifu sana wa kufata maelekezo na pia adabu kwa wakubwa lilikuwa si ombi bali ni lazima uliweza adhibiwa na yoyote ili miradi umetenda kosa(misingi ya sheria za nyumbani).Kipindi hicho nahisi ndio kulikuwa na kizazi chenye uelewa mpana licha tu wengi hawakupata nafasi ya kuendelea mbele kwa sababu ya ufinyu wa shule za sekondari .
Kwa sasa wazazi tuna deni kubwa la kuandaa hiki kizazi kweli kuna kazi kubwa sana kulifikisha taifa mbele maana changamoto kubwa kwa sasa ni kutowajibika kikamilifu sisi wazazi tokea nyumbani kumuweka mtoto kwenye mstari huku shule ambazo zilizoaminiwa zamani kwa kuwanyoosha watoto nazo zikikabiliana na kanuni na taratibu za kufuata(kitu ambacho ni chema kuepuka madhara kwa watoto,hakuna adhabu za fimbo),kwa sasa kuwakuta watoto wanafanya vitu vichafu ni kawaida huku jamii ikijitenga navyo(matusi na yanayofanana na hayo ata mbele za watu) na ata kurudi wewe mtu mzima.
Kwa hili walimu wetu wa sasa wana kazi kubwa sana tofauti na zamani maana mtoto anamaliza muda mwingi shule kuliko nyumbani ambako kwa miaka ya sasa hakuna sheria ndogo ndogo kama ilivyokuwa zamani.Wazazi tushituke maana husipozifa ufa utajenga ukuta. Niwatakie mfungo mwema.