Kuna ambao hawataiona hoja yako iliposimama hasa kwa vile baadhi ya aya umeingiza utani wa jadi. Lakini hoja zako zote mbili zina mashiko.
1.Binafsi sikutegemea nahodha wa timu inayoahiriki Ligi kuu na FA kuwa "mshamba" kiasi kile. Timu inayotegemea kuwakilisha Taifa kimataifa inatakiwa kuongozwa na mtu anayejitambua na mwenye uwezo wa "kuchagua maneno". Nahodha anaongea kama shabiki wa Kijiwe Nongwa?
2.Tatizo la rushwa kwenye soka ni kubwa na si Tanzania tu bali ni Dunia nzima japo sababu zinatofautiana kulingana na maeneo ikiwemo hii ya Njaa za waamuzi, njaa za wachezaji, Kamali, status za matajiri nk. Mbali ya shughuli nyingine binafsi Mimi rafiki yako ni mwamuzi wa soka professionally. Najua ukweli wa unachoongea, siongezi kitu.