Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Mwaka 1994, wana CCM waliokuwa wakifaidika chini ya utawala wa Rais Mwinyi, kwa kuogopa mabadiliko, hawakutaka ang'atuke baada ya kumaliza kipindi chake.
Kampeni kubwa ilifanywa ya kutaka Katiba ifanyiwe mabadiliko Mwinyi awe mgombea pekee kwa kuogopa nguvu na moto waliyokuwa nao wapinzani na hasa NCCR.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM walikuwa tayari kupitisha azimio hilo la kuomuongezea Mwinyi awamu ya tatu kwa wasi wasi wa kupoteza uchaguzi mwaka uliofuata.
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alijitokeza na kupinga kwa nguvu azimio hilo akionya kuwa Katiba si kama shati unalochagua uvae lipi kila ukiamka.
Wazo la Mwinyi kuendelea likafa kibudu lakini CCM ikaendelea kuwa pamoja licha ya wagombea kujitokeza huku kampeni za kumpata mrithi zikiendelea bila mizengwe.
Mwaka huu Chadema nayo imejikuta iko njia panda na wajumbe wana wasiwasi kuwa mwenyekiti aking'atuka hawajui hatma yao na chama kwa ujumla itakuwaje .
Je wazee wenye hekima, busara na ushawisi kama Mwalimu hawapo tena? Woga wangu ni kuwa inawezekana wapo wajumbe ambao hawana maisha nje ya Chadema.
KIla baada ya miaka mitano Watanzania wenzetu wengi hujitokeza kugombea Urais Tanzania lakini, pamoja na mizengwe, mwisho wa siku sote tunabaki ni Watanzania.
Kwa nini kwa Chadema, chama cha kidemokrasia na maendeleo, hii isiwezekane kwa wagombea kujitokeza na wana Chadema wakabaki wamoja baada ya uchaguzi?
Najua jinsi ndani ya CCM, chama cha majizi kinachoendeshwa kimla, hili haliwezi kutokea na watafanya kila wawezalo kuhujumu uchaguzi huru na kuwasambaratisha.
Walaaniwe wale wote watakaojaribu kuuvuruga uchaguzi wa Chadema utakaofanyika tarehe 23/1/2025 kwani ni uchaguzi unaotazamiwa kuwa wa kihistoria nchini.
Tahadhari...nawaomba wana Chadema, kwa kuwa mnajua mnaandika historia, hiyo hiyo historia itawahukumu na kama kutatokea mizengewe isiyo ya lazima...hatutawasemehe!