Umenidownplay, ila hilo naliacha kwanza!
Sijakudownplay (your words sic!) ila kwa bahati wewe unayo choice...Chadema ikikuzingua, CCM inakusubiri kwa mikono miwili. Wengine hatuna hiyo choice, hakuna namna naweza nikahamia chama hicho...not over my dead body!
Unatumainia nini kwenye huu uchaguzi?
Wapambe maslahi ni wa kuogopwa kama ukimwi.
Baba wa taifa alitaka kuachia uongozi mapema sana lakini wapambe maslahi hawakuwa tayari, walimlilia wakitaka aendelee kwa kudai hakuwepo mtu wa kuvaa viatu vyake.
Mwaka 1975 wapambe maslahi walimsihi aendelee wakidai haukuwa wakati muafaka wa kuachia madaraka kati ya chochoko za Idi Amin Dada wa Uganda zilikuwa zimepamba moto.
Mwaka 1980, wapambe hao hao nuksi walimuomba aendelee tena wakidai ndiyo tumetoka vitani (vita vya Kagera) na hivyo uongozi wake bado ulihitajika kuliko wakati wowote ule!
Mwalimu alikubali lakini kwa sharti moja ingekuwa awamu yake ya mwisho na kweli mwaka 1985 aling'atuka baada ya kutembea nchi nzima akimnadi mrithi wake Hasan Mwinyi wa Zanzibar.
Sasa shuhudia lawama alizopewa Mwalimu baada ya kung'atuka madarakani alipopinga Mwinyi huyo huyo kuongezewa miaka mingine mitano baada ya kumaliza muda wake mwaka 1995!
Wapambe maslahi wa Mwinyi walimtaka Mwalimu akae kimya wakidai inakuwaje apinge wakati yeye mwenyewe aling'ang'ania madaraka kwa miaka zaidi ya ishirini bila kumpisha mtu!
Chama kile kile, wapambe wale wale...na sasa tunawashuhudia wapambe wa mwenyekiti wa chama mbadala Chadema wakiwa kazini wakifuata nyayo za wapambe wa CCM, hakuna cha ajabu!
Birds of a feather fly together...ndege wafananao huruka pamoja! Ni Lissu tu ndio mpaka sasa ameaonesha nia na ari ya kulikwamua taifa letu kutoka mikononi mwa walafi, wanafiki na wafuata nyayo!