Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Hapo tunakubaliana ila mimi naona mtu mwenye hizo sifa ni Freeman Aikaeli Mbowe. Na amefanya hivyo kwa zaidi ya miaka 20...Chadema inahitaji Mwenyekiti atakayewatia hamasa viongozi na wanachama kukijenga chama chao.
..Pia Mwenyekiti mjenga hoja mzuri, anayeaminika ndani na nje ya chama, atakayeshawishi Watanzania wengi zaidi kujiunga, au kuiunga mkono Chadema.
Huyu ni mtu aliyekubali kukaa meza moja na mtu aliyemuweka ndani kwa zaidi ya miezi 7 kwa manufaa ya chama chake. Huo ni ukomavu, sio uoga. Ingekuwa rahisi sana kwake kugoma kukutana nae na jamii ingemuelewa lakini hakufanya hivyo.
Kwangu mimi Lissu amepoteza sifa hizo kwa matendo yake ya hivi karibuni ambayo yanaweza kujenga jeraha katika chama ambalo hana uwezo wa kulitibu.
Amandla...