Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja na kuwa inaelekea unadhani kuwa mimi ni kibaraka wa Mbowe, nitaingiza my two cents. Hamuwezi kulinganisha vyama tawala na vyama vya upinzani. Vyama vya upinzani vinahitaji mtu ambae ana uzoefu na ameonyesha uwezo wa kukiwezesha chama chake ki survive katika mapito magumu. Kitendo cha Lissu kurudi nchini na kuanza kukandia chama chake hadharani hakikuonyesha leadership qualities.Duh TUJIGEMEE, kwa namna moja uko sawa lakini kamwe si kama unavyowaza, mimi siku zote niko upande wa uhuru, haki na utawala wa sheria. Mpaka hapo uko sawa niko upande wa T.A. Lissu.
Lakini hapa tena si habari ya kuwa upande wa mtu binafsi, nawapenda Lissu na Mbowe kwa pamoja lakini si kwa kila jambo. Wote wawili ni binadamu na hakuna binadamu asiye na mapungufu
Mimi ni mpenda demokrasia na nilitegemea wagombea wengi tu kujitokea kugombea hicho kiti lakini kitendo cha Mbowe kujitokeza kutetea hicho kiti alichokikalia kwa miaka zaidi ya ishirini, kilishtua!
Ukweli lazima usemwe, Mbowe anaungwa mkono zaidi na wajumbe wenye maslahi katika uenyekiti wake. Kitendo chake kimesaliti dhana ya demokrasia ndani ya Chadema tegemeo pekee la wananchi.
Binafsi nilipigwa butwaa nikakumbuka kauli ya jiwe kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 kwa wasimamizi nanukuu si kila neno, "nikuteue, nikulipe mshahara halafu umtangaze mpinzani kuwa kashinda!"
Mpaka hapo tofauti ya Chadema na chama cha wezi CCM ni ipi?
Ni imani yako. Sasa tusubiri maamuzi ya wapiga kura...kasikilize Powerbreakfast ya Clouds Media ndio utasikia maoni ya Tundu Lissu kuhusu Mwenyekiti Freeman Mbowe.
..sio sahihi kumlaumu Lissu, na hata Mbowe, kwa maneno, kejeli, na matusi, ya wapambe.
..Watanzania wako pale wanasubiri kuona kama wajumbe watachagua Mwenyekiti anayejibu matarajio ya wananchi, au la.
..Taifa linahitaji Mwenyekiti wa Chadema mwenye rekodi ya uadilifu, mwenye msimamo thabiti, mjenga hoja mahiri, na msomi anayeijua nchi, na dunia.
Siko hapa kubishana na watu wnao nitukana. Tubadilishane mawazo kwa hoja na sio matusi. Mbona wengi tu tuna tofautiana mawazo lakini hatuvunjiani heshima?Kumbe uko hapa kubishana! Ndio maana unapata shida.
Utukanwe na nani boss. Fahamu huku ni kwenye mitandao ya kijamii na sio group la wanaparokia. Matumisi ni vibwagizo tu, lakini hoja zinaeleweka.Siko hapa kubishana na watu wnao nitukana. Tubadilishane mawazo kwa hoja na sio matusi. Mbona wengi tu tuna tofautiana mawazo lakini hatuvunjiani heshima?
Amandla...
Na ni haki yangu mimi mparokia kumkatia mtu ambae sipendi lugha yake.Utukanwe na nani boss. Fahamu huku ni kwenye mitandao ya kijamii na sio group la wanaparokia. Matumisi ni vibwagizo tu, lakini hoja zinaeleweka.
Matokeo ni ama Mbowe awe Mwenyekiti au Mwenyekiti awe Mbowe. Wanachadema hawana chaguo jingine.
Kuna tatizo gani kusubiri sanduku la kura liamue? Wagombea 3 wamechukua fomu sasa si tusubiri nani ataibuka kidedea? Au mlitaka Mbowe ajitoe? Hoja ni nini hasa hapa?? Uchaguzi usifanyike au kuwe na mgombea mmoja tuu TAL???Kwa yaliyopo CHADEMA ni bora mtu uwe tu CCM, hawana uafadhali wa kuzidi CCM. Maybe siku chama kikiacha Kuongozwa kama Kikoba cha Mbowe!
Kwa yaliyopo CHADEMA ni bora mtu uwe tu CCM, hawana uafadhali wa kuzidi CCM. Maybe siku chama kikiacha Kuongozwa kama Kikoba cha Mbowe!
😂😂😂😂😂😂Mwingine huyu ambae sina muda wa kujibishana nae.
Amandla...
Hakuna popote ambapo Lissu alimpaka Matope Mbowe. Tatizo lenu mmetafsiri kitendo cha Lissu kutangaza nia ndiyo upakaji wa matope.Mimi binafsi sina tatizo na Lissu kugombea Uenyekiti. Naamini inaonyesha ukomavu wa chama chake. Ninachopinga ni namna alivyoingia kwenye hicho kinyang'anyiro. Hapakuwa na sababu za kumpaka matope Mwenyekiti aliyekuwepo. Yeye angejikita kwenye kuuelezea umma sababu za yeye kuamua kugombea. Na pale surrogates au wafuasi wake walipoanza kumsema vibaya Mbowe angewanyamazisha kama vile McCain alivyofanya pale shabiki wake alipotaka kupaka matope Obama. Yeye bado relatively ni kijana ambae bado ana nafasi ya kugombea urais na Uenyekiti hata mwaka 2030. Alikosea kuacha kampeni ya kumfanya Mbowe aonekane ndio villain namba moja wa Chadema iendelee. Hapo ndipo aliponi boa.
Amandla...
Hapana. Board room politics ndio wakati wake sasa. Na kusema kuwa anafanya hizo tu sio kumtendea haki. Mbowe ameonyesha uwezo mkubwa wa kuorganise protests n.k. Uzuri wake yuko pia willing kulipia gharama.
Tatizo letu watanzania tunapenda majibu mepesi kwenye maswali magumu. Tunawapenda wale ambao wanatuambia kuwa watapigana kwa ajili yetu kuliko wale wanaotuonyesha kuwa watapigana pamoja nasi.
Sio bure watu kama Babu wa Loliondo, Mwamposa, Gwajima na wengine wanakuwa na wafuasi wengi. Hii ni kwa sababu wana ofa miracle cures zinazotoa majibu immediately. Kwa mtindo huo hatutafika mbali.
Amandla...
Haki yako inaheshimiwa. Ila kwenye mitandao ya kijamii sio sehemu utapata utulivu uutakao. Ni sawa na stand, kuna matusi ya wazi lakini watu hawaachi kusafiri.Na ni haki yangu mimi mparokia kumkatia mtu ambae sipendi lugha yake.
Amandla...
Kuna mambo hufahamu mkuuAlikosea kuacha kampeni ya kumfanya Mbowe aonekane ndio villain namba moja wa Chadema iendelee. Hapo ndipo aliponi boa.
Mimi naona tatizo ni kuwa mmeigeuza kuwa kama Instergram/ X. Ndio gharama ya mafanikio.Haki yako inaheshimiwa. Ila kwenye mitandao ya kijamii sio sehemu utapata utulivu uutakao. Ni sawa na stand, kuna matusi ya wazi lakini watu hawaachi kusafiri.
Ngoja tuongee kuhusu ushujaa wa Lissu.Kuna ushujaa gani katika kupigwa risasi? Mashujaa kwangu mimi ni wale waliohakikisha haendi Muhimbili. Wale waliosimama kidete apate huduma zote muhimu.Punguza uongo. Usijisahaulishe Lissu aliyopitia kipindi Cha Magufuli. Kapigwa risasi na kafutwa ubunge. Ni mtu straight. Nakataa board room politics hazina maana Kwa CCM.
Nimekuelewa Mkuu. Hata hivyo, mkinyima Uwenyekiti Aikael na kumpa Uwenyekiti huo Antipasu hapo mtakuwa mnamlazimisha Aikael agombee uRais. Sasa kwa wasiwasi wako juu Chadema Maslahi ikatokea Aikael akaukwaa...huoni utakuwa umewaingiza Watanzania kwenye mkenge?Ukweli lazima usemwe, Mbowe anaungwa mkono zaidi na wajumbe wenye maslahi katika uenyekiti wake.