Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Huwa napenda Sana jinsi ulivyo huru, licha ya Kwamba baba yako so mtu Ni JIWE ⛰️ na anajinadi ameimarisha chama. Je chama imara kwanini kinauogopa upinzani dhaifu?Katika maisha yangu ya kisiasa sijawahi kushuhudia mgombea wa CCM akimkwepa au kukwepeshwa mpinzani wake hata mara moja kuanzia enzi za chama kimoja hadi vyama vingi.
Kuanzia ubunge wa mzee Warioba vs Wassira, enzi za Augustino Lyatonga Mrema vs Abdul Cisco Mtiro hadi msimu wa mzee Malecela vs Kibajaji.
Katika ligi zote hizo nilizotaja kama mifano fomu za wagombea zilipokelewa na figisu zikaachiwa kwenye uwanja wa Mapambano.
Ndio najiuliza misuli ya kifua cha CCM inazidi kuimarika au imeanza kusinyaa?!
Kwa kazi hii kubwa ya kuleta maendeleo kwa haraka iliyofanywa na serikali ya awamu ya 5 kuna haja gani ya kuwapa wapinzani visingizio vya kushindwa?.......au CCM inahujumiwa maana waswahili wana msemo wao eti ....Kikulacho ki nguoni mwako!
Maendeleo hayana vyama.
Jibi Ni rahisi kabisa CCM haikubaliki