Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Nilikuwa naona kama watu wa bandari walafi tu wa eneo. Ila ukilinganisha na bandari zingine, bandari ya Dar ina eneo dogo sana. Bandari kubwa(kwa mizigo) zaidi Afrika ni ya Tangier, Morocco. Ina eneo la ardhi la ekari 2,500. Bandari ya Mombasa, Kenya ina jumla ya eneo la ekari 3,000. Ban mydari ya Durban, Afrika Kusini ina eneo la karibu ekari 5000. Hizi ni bandari kubwa sana Afrika. Bandari ya Djbout ina ukubwa wa ekari 1,700.
Tukirudi Dar es Salaam, eneo la bandari ni ekari 270 tu!! Ili kwenda sawa na hizo bandari kubwa Afrika, kuongeza eneo la bandari ya Dar Es Salaam naona kama ni muhimu.
Tukirudi Dar es Salaam, eneo la bandari ni ekari 270 tu!! Ili kwenda sawa na hizo bandari kubwa Afrika, kuongeza eneo la bandari ya Dar Es Salaam naona kama ni muhimu.