Pre GE2025 Kwa lugha ya picha CHADEMA imekata tamaa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna 'MKANGANYIKO' usio kuwa wa lazima, ambao Sekretariati ya CHADEMA imeruhusu uwepo na kuvuruga matarajio ya wananchi juu ya chama hiki.
Sitaki kumlaumu Mnyika, kwa sababu natambua uwezo wake mkubwa. Bila shaka haya ni maswala asiyo kuwa na uwezo juu yake.
Inasikitisha kuwa haya yanatokea wakati muda huu ni hatarishi sana juu ya programu ya chama hicho.
 
Acha usengerema wewe!
 
Mimi ni Free Soul, hupenda kuongea my Mind. Ila sio Loose Canon kama Mdude😀
EEEeeeenHeeeeEEE!

Umekwisha peleka pongezi za ushindi mnono lakini alio upata 'idol' wetu; pamoja na kwamba hakuna tofauti iliyo tegemewa kutokea bila miujiza?
 
Ninakubaliana nawe katika hili.
Sasa nakuomba uligeuzie huko CCM upate picha itakuwaje pakiondolewa gundi inayo lishikilia genge ndani ya chama hicho.
Huku afadhali kidogo kuna checks and balances ndio maana wana dumu.
 
Huku afadhali kidogo kuna checks and balances ndio maana wana dumu.
"Checks and Balances" ni kutishiwa mchuzi kuwekwa mchanga kwa atakayenyoosha kidole.
Hapo ndipo CCM ilipofikia sasa hivi.
 
"Checks and Balances" ni kutishiwa mchuzi kuwekwa mchanga kwa atakayenyoosha kidole.
Hapo ndipo CCM ilipofikia sasa hivi.
Elements za taasisi bado zipo kwa mbaaali.
 
Elements za taasisi bado zipo kwa mbaaali.
Hapana.
Sasa hivi ni 'maslahi' tu ndiyo yanayo tawala ndani ya hiki chama. Tazama Kamati Kuu au Halmashauri Kuu; halafu niambie kuna watu huko ndani wanao jali chochote kuhusu mfumo!

Pangekuwepo na mfumo, 'Chura Kiziwi' asinge ingia na mara moja hiyo kubadili yote aliyokuwa akisimamia mtangulizi wake.
 
Tujadili kauli ya NAPE goli la mkono kwa Byabato Kagera. Wizi ndio unaokivusha ccm na siyo udhaifu wa chadema wakarlti mwingine
 
Umeona vyema Mkuu, CDM imekwama mahali ikitaka kujitutumua kuna namna ari inazimwa.

Rejea kabla na baada ya kesi ya Mbowe kuisha watu walihamasika sana hasa kwenye ishu ya Katiba Mpya, ila siku Mbowe anatoka jela, jioni yuko Ikulu na hamasa yote ikafa.

Mpaka leo ni historia, na chama kimebaki kuchechemea mpaka leo. Inasikitisha.
 
Tatizo lilianza kuthibitika kuwepo wakati huo ulio uelezea vizuri kabisa. Lakini mimi nakurudisha nyuma kidogo kuongezea uzito wa haya yote.
Wale wanawake kwenda Bungeni...; hapo ndipo mkoroganyo ndani ya CHADEMA ulipo anzia. Na Mbowe alipoingizwa kwenye "Mazungumzo ya Maridhiano" na kuamriwa yeye na wenzake wote atumie "lugha za staha"; mambo yakaanza kuvurugika ndani ya chama.

Sasa Mbowe ni kama anayezinduka usingizini, lakini hajui anakokipeleka chama sasa. Hajui kama kuwa sehemu ya serikali ya 'chura kiziwi' ndiyo bora zaidi, au kujitutumua na kufanya juhudi kuiondoa moja kwa moja CCM madarakani.
Kadri ya muda unavyo zidi kuyoyoma, ndivyo CCM wanavyo zidi kuwa na uhakika wa kumlisha tope Mbowe.
Inasikitisha sana.
 
Kwa taarifa yako hao watu unawaona hapo kwenye mikutano ya cdm ndio uhalisia wa siasa zetu ulipofikia baada ya dhalimu magu kuharibu siasa za ushindani hapa nchini. Usidanganywe na nyomi za ccm, maana zile hazina uhalisia bali ni za kulazimisha, ili kuhadaa umma kuwa wanakubalika.
 
Vyama pinzani havina fuba kama chama tawala, laiti kama wangekua wanakaribiana kwenye ukwasi basi chama tawala kingekua na tumbo joto.
 
Mama na yake ccm wako juu misafara wa magari 150, tutalipa Kodi tu ili wafanye matanuzi

Chadema hawajaathiri maisha yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…