Kwa maamuzi haya ya Rais Trump bila shaka Hayati Magufuli alikuwa mbele ya muda

Kwa maamuzi haya ya Rais Trump bila shaka Hayati Magufuli alikuwa mbele ya muda

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kuanzia mwaka 2025 kuzilazimisha nchi za Afrika kujitegemea kupitia kuzinyima misaada mbalimbali umeshaabiana na Uamuzi wa Rais wa tano wa Tanzania hayati Magufuli kuanzia mwaka 2015-2020 kuilazimisha Tanzania kuacha kutegemea misaada ya mabeberu na badala yake watanzania wajitegemee kupitia kujenga viwanda vyao.

Hayati Magufuli alikataa hata misaada ya mawazo kutoka kwa mabeberu aliposema kuwa katika kipindi chake Tanzania haitakuwa nchi ya kukopi na kupaste kutoka kwa mabeberu. Chukulia mfano suala la Corona.

Sasa hivi watanzania hawana wasiwasi hata tukinyimwa misaada maana tulishafundishwa na Magufuli kuwa watanzania tunaweza na nchi yetu ni tajiri.

Maamuzi ya Trump yamechelewa sana, yalitakiwa yawahi ili kukomesha tabia ya viongozi kupanda ndege first class na rundo la wasanii kwenda kuomba misaada kwa mabeberu.
 
Magufuli alikuwa kichaa alikataa chanjo za Covid -19 kwa ujinga wake huku akisahau kuna watu walizihitaji chanjo hizo , naye Covid -19 ikamfyekelea mbali .

Huwezi kumlinganisha Trump na kichaa kama yule.
Kunywa bia
 
Misaada imesimamishwa kwa Siku 90 tu, kuangalia Kama kuna tija, baada ya hapo ombaomba wataendelea Kama kawaida
 
Magufuli alikuwa kichaa alikataa chanjo za Covid -19 kwa ujinga wake huku akisahau kuna watu walizihitaji chanjo hizo , naye Covid -19 ikamfyekelea mbali .

Huwezi kumlinganisha Trump na kichaa kama yule.
Ni watanzania wa ngapi walichanjwa?
 
Wenzio wanaongea mikopo wewe unaongelea covid 19.
Ndio utofauti wa mawazo yeye kaongelea mikopo mimi nimeongelea COVID -19, Magufuli aliwakosesha waliohitaji chanjo hii haikukabaliki.

Na kwenye hiyo mada COVID -19 imetajwa , hutaki tuchangie ?
Bila shaka hasira za kukosa ajira ualimu zinakutesa
Pole sana, wewe na mleta mada bado hamjakubali kuwa yule mungu wenu harudi tena sishangai bado mpo hatua za mwisho kufikia ile stage ya acceptance.
 
SGR ni mkopo 💯
Shida ya mleta mada ni ushabiki uliopitiliza hata Magufuli wakajiaminisha eti alikuwa hakopi.

Akasome hapa kama lugha haimpigi chenga aone pesa za hiyo SGR zilitoka wapi.

Shida ya mleta mada ni ushabiki uliopitiliza hata Magufuli wakajiaminisha eti alikuwa hakopi.

Akasome hapa kama lugha haimpigi chenga aone pesa za hiyo SGR zilitoka wapi.

Tumia akili basi
 
Tumia akili basi
Mimi ninatumia akili wewe unaendeshwa na ukabila ilhali hata Magufuli hakuwa msukuma.

Ni aibu karne ya 21 mtu kutumia ukabila kama turufu ya uongozi.

Magufuli alizuia chanjo kwa sababu anazozijua yeye kikatiba huyu alizuia haki za wengine na ni kinyume cha taratibu na haki za binadamu , mkileta mada zake tutamjadili tu maana ukweli ni kuwa aliyafanya tunayoyasema.
 
Ndio utofauti wa mawazo yeye kaongelea mikopo mimi nimeongelea COVID -19, Magufuli aliwakosesha waliohitaji chanjo hii haikukabaliki.

Na kwenye hiyo mada COVID -19 imetajwa , hutaki tuchangie ?

Pole sana, wewe na mleta mada bado hamjakubali kuwa yule mungu wenu harudi tena sishangai bado mpo hatua za mwisho kufikia ile stage ya acceptance.
Una akili ndogo sana. Ok.
1. Kujitegemea na covi 19 zinahusiana vipi ? Hata hivyo badala ya kuchanja alisema peta hivyo hivyo immunity yako inatosha
2. Unadhani Covi 19 haukuwa mradi? Mbona dunia sasa haihangaiki na ujinga huo?
3. Sasa ARV utakosa tuone utakula vocha gani
4. Afrika jipange kujitegemea acha kuomba omba utaolewa.
Kama umechafukwa njoo na povu
 
Back
Top Bottom