Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Side mirror ikavunjika, ikaweka na kreck????.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila unachokiona huwa ni halisi, Mara nyingi ni maruerue (Hallucination) kwaajir ya kuchoka, Usingizi ama ulevi. Angalia hata muda mnaodai kukutana na hayo, Ni wastani wa muda mwafaka wa binadamu kuchoka.
Uchawi na miujiza mnavisingizia tu, Havina kweli yeyote.
Dereva pumzika vya kutosha, kunywa maji vzur, usitumie vilevi, usisikilize music kwa sauti kubwa, Pumzika walau dk10 kila masaa matatu-manne ya safari.
Hiyo miujiza utakuwa unahadithiwa tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi wa tano mwaka huu,natoka Dar naenda Lindi nilikuwa na gari ndogo.Mbele ya Njia nne(wakazi wa kilwa na kusini watapajua) kuelekea Nangurukuru kuna sehemu hapo katikati kuna pori kubwa kiasi,nikakutana na mtu mrefu hatari (Sioni mwisho wake kwenda juu) afu kavaa nguo nyeupe kama kanzu hivi amesimama pemben ya barabara *****! nilikuwa speed 100 lakn niliona gari haitembei na niliwasha ac ila nililoa jasho,kufika nangurukuru nikasema nipark mzani nisubir kukuche mweee nakutana na madere wawili wadangote wametokea dsm pia,kumbe nao walikutana na lile dubwana ***** sitosahau ilibdi nipumzike pale mzan mpk saa kum na mbili
 
Kuna dereva wa daladala Mwanza,,alipata ajali maeneo ya nyakato sokoni,miaka ya 90,yeye alikuwa anadai amegonga mbwa,,sisi wananchi,,tunamuona mwanafunzi wa kike kalala chini ,,tulimpa kipigo sana,,tukahisi amechanganyikiwa kwakuuwa mwanafunzi,,police ndio waliomuokoa,lakini akakomalia msimamo wake kuwa kagonga mbwa huku akipandishwa kwenye defender,akaenda kukaa siku 14 butimba gerezani,
baada ya wiki moja,ikasemekana kupitia wanafunzi wenzake wa primary ,, kuwa yule binti,,anaonekana akienda sokoni mida ya saa nne asubuhi,,wananchi wakaunda kamati,wakafatilia,kweli wakamuona yule binti anaenda sokoni ,mpaka nyumba anayoishi,,kumbe ni kwa bibi mmoja mitaa ya hapo hapo nyakato sokoni,,isssue ikavuma nyakato nzima,,watu wakaandamani mpaka kwa bibi,,baaada ya timbwili lakutosha,,bibi akamtoa yule binti,watu wakataka kuchoma nyumba na bibi,,police ndio ikamuokoa.
yule dereva alitolewa na akawa anaendelea na kazi zake kama kawaida,,HAYA MAMBO YAPO NASIO YAKUSADIKIKA
 
Yalivyo nikuta ni saa 8 mchana, Arusha na Mombo mkuu uchovu utokee wapi ? Safari ya masaa 4 ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka 1996 nlikuwa mdogo sana lkn bado nna akili ya kumbukumbu kuna safari moja tumepanda basi ni mwanza tunakwenda Musoma na Mzee nlikuwa nmekaa siti ya mbele......dereva akiwa mwendo kasi mara ghafla akatokea mbwa mbele nachokumbuka na kushangaa ni yule mbwa alitoka spidi kutoka pembeni halafu akasimama ghafla barabarani katikati halafu akusogea tena akaganda kama sanamu analiangalia tu gari.......dereva akaenda mvaa hivyohivyo kwa spidi na kishindo........lkn watu walizungumza sana na kwa gumzo sikumbuki walizungumza nini lakini baada kupitia uzi huu naweza kurelate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku natoka Mtwara nakuja Dar,,,kibabu kimoja,kikiwa na tenga kimeweka bata wawili,Akatuomba lifti anashuka mbagala,,tukamchukua,,chakushangaza ndio safari pekee ambayo nimesafiri bila kukaguliwa hata mara moja,na mbaya zaidi nilikuwa nimebeba MBAO NA Magunia ya Mkaa,,na hii njia yakusini,,ndio inaongoza kwa ukaguzi ,,hasahasa mageti ya maliasili,tulikuwa tukifika kwenye geti la maliasili,tunafunguliwa geti kama waheshimiwa,,,,tunaruhusiwa tu,,,natamani sana huyu babu niwe nambeba kila siku,,,mwisho wa safari babu akatuambia,,msiwe mnazarau watu,,hamjui wanamsaada gani kwenu,,haya safari njema,
 
Kwahiyo umenihadithia ili nami niamini kua kuna mambo kama hayo au?.
Uchawi ulikuwepo, upo na utaedelea kuwepo. Hakika sijakutana na ninahakika sitakutana navyo kwakua mimi sio mshirika wao.
 
Miaka mingi naendesha gari tena usiku,hasa njia ya tanga nimeendesha roli zaidi ya miaka mi4 na mara nyingi napita usiku, na saa hii Niko safari be ktk nchi fulani, sijawahi kuona kitu cha kunitumia, nawasikiaga tu watu wengine, nilichowahi ona ni mtu yuko uchi saa 8 usiku mbele kdg kupita muheza town kuelekea lusanga na mtu akiwa anatembea uchi usiku kipande cha segera hale, lkn wote hawa nafikiri ni wendawazimu tu kama tunaowakutaga mchana barabarani, na siku moja wkt nakaribia kuingia mkata saa 9 usiku nilimgonga bundi nilikuwa speed akajipiga kwenye kioo kikubwa cha mbele mpk kafa lkn kioo hakikuvunjika, lkn nikiwa tanboi zamani wkt nikiwa njia ya tabora arusha wkt huo ktk basi za kampuni fulani hv dereva wangu alitaka kuangusha gari maeneo ya ziba kuelekea nzega baada ya kuruka kwenye kiti akiwa anaendesha baada ya kudai panya kamwingia kwenye suruali, lkn mi nilikua hapo jirani sikuoni panya, lkn baada ya kuwa dereva na mara nyingi nasafiri peke yangu tena nakesha, ninachokijua ukiendesha mda mrefu na ukiwa na uchovu unaweza anza sinzia na kuona kama mko wawili na huyo ulienae anakuongelesha, au unaweza ona kama mtu anavuka au mnyama kumbe ni uchovu tu na usingizi, ushauri paki gari na upumzike hata saa moja,mf.juzi maeneo fulani ya Zambia mchana naendesha nikaona kama farasi barabarani kucheki kwa makini gari inaelekea kulia mwa barabara nikailudisha barabarani kumwangalia kijana nilienae kalala fofofo, napaki gari pembeni anashtuka na kuniuliza anko vp namwambia nasinzia je umeona gari ilivyotaka kuhama njia? ananijibu sijaona, nikamwambia usingizi unaambukiza mi nimesinzia kwa kuwa njia nzima we unalala tu kushoto hapo, nikamwambia nalala baada ya saa moja niamshe, aliponiamsha nikaendendelea na safari, khs kumgonga mtu usimwone inatokea wengine waoga hukimbia baada ya kuguswa na magari kwa uzembe wao, hata mi nikiwa nasoma siku moja utotoni niliingia barabarani bila kuangalia ikatokea hilux moja ikashika bleak lkn inapushi na kuanguka ile dereva kufungua mlango mi nikainuka mbio nyingi, ushauri ukiona unadrive hata kama ni mchana ukaona mauza uza paki gari panda kitandani lala kwa muda, kama haina kitanda kunjua siti lala, mara nyingi kuendesha gari mda mrefu hukupunguzia umakini
 
Hakika nisiwe mwongo, nasafiri sana usiku tena pekeyangu sijawahi kuona chochote kitu. Haya ni maneno ya waafrika wenye uoga moyoni na imani za kujumlisha.
Kwakuwa hayajawahi kukukuta, haimaanishi haya hayapo.
 
Usingizi na mwendo kasi + mbuyu uko karibu na barabara = imani potofu!
 
Ubongo wa binadamu ni very complex! Unaweza kukuletea taswira fulani na wewe ukaona kama ni kweli kumbe siyo. Ni mazingira na mawazo uliyonayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…