Liwagu
JF-Expert Member
- Jan 25, 2017
- 5,593
- 6,754
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahhaa si kweli nakataaDuuuh mnazi nimesha kukumbuka tulikutana siku ile usiku [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Nina ringi la shaba nimenunua 5000 ...kuna mzee mmoja wa kinyakyusa siku moja akanitania niuzie mjukuu wangu hilo ringi?nadhani alijua mi nipo vizuri nikamwambia hili siuzi hata kwa milioni akacheka tu angejua mi mtupu tu nadhsni anngenijaribu...mi ubaya nauota tu na kwa mganga sijawahi kwendaMKUU KUNA siku nilikuwa nakwenda TANGA,,,nipo na jamaa kama 4 kwenye GARI ndogo nikiwa naendesha ,, nakumbuka tulitoka hapa DAR ,mapema kama SAA 12 jioni,,tukaenda mdogo mdogo kufika CHALINZE tukatulia SEHEM vurugu za MABASI NA MAFUSO ZIPUNGUWE,,,kufika kama SAA 4 USIKU tukaanza safari ya kwenda NGAMIANI TANGA,,,TUKIWA kwenye gari story ziliendelea kama kawaida ili DEREVA NISILALE.,,tukaipita MSATA,,salama,,WAMI,,, MKATA,,SEGERA hyo,,,,Salama salmini, HALE ,, tukatoboa MUHEZA SAA nane USIKU,muda huo wenzangu wote nilihisi wamelala,maana ilikuwa kmya,,nlikuwa nasikiliza MVUMO WA INJINI YA GARI NA UPEPO TU,,, sasa balaa likaanza TUMEFIKA kuna SEHEM inaitwa MKANYAGENI,,nikaona mbele kama mita 50 kuna MWANAMKE katikati ya Barabara,,kakaa chini tena yupo UCHI WA MNYAMA,,,amekaa mkao wa kunyoosha miguu kuangalia tulipokuwa tunakuja,,Nikasikia KELELE MMOJA,,,wa JAMAA yangu aliyokuwa mbele ananambiya KANYAGA MAFUTA,,USIFUNGE brake TUTAKUFA,,MCHAWI YULE,,,,,jamaa wote waliamka,,,wakati huo nilikuwa nipo SPEED KAMA 120 HIVI...basi nikakanyaga mafuta nikampitia yule MAMA katikati ,,,means NIMEMGONGA,,,lakini sikusikia DALILI YEYOTE YA KUGONGA,,,,muda huo watu wote walikuwa macho,,,,huku tukiwa na Taharuki ya kugonga MTU,,,nilizidisha speeds ya gari hadi NGAMIANI MJINI,kwa kuwa ilikuwa ni USIKU ilibidi kusubiri kukuche, ,ilipofika ASUBUHI nikaanza kuikaguwa GARI,,AJABU haikuonyesha DALILI YEYOTE YA KUGONGA MTU,,aisee tulishangaa sana,,wala hakuna DALILI KWAMBA TULIGONGA MTU PALE,,PIA,,TULISHANGAA SANA,,, KUNA SIKU ingine nipo PEKE YNGU kwenye GARI,,,ilikuwa kama SAA NANE za USIKU ,, Barabara ya MOROGORO maeneo ya MAGARI SABA DARESALAM , ,,njia ilikuwa imetulia sana muda huo,,,NIKIWA SPEEDS PEKE YNGU BARABARANI,,,,,,mbele kidogo nikaona LORI LINAKUJA KWA KASI WRONG SITE,,means limehama UPANDE wake linakuja kwngu,,ikabidi NIHAME UPANDE wa pili KULIPISHA,,,kuangalia kulia naona kuna LORI LINGINE limewasha taa nalo linakuja kwa speed,,Duu,yaani nipo katikati UPANDE wa kushoto kuna LORI LINAKUJA UPANDE WNGU,,na kulia pia KUNA Lori kwa kifupi niliwekwa katikati ya magari mawili yanayokuja mbele yngu kwa KASI KUBWA,,nilihisi mikono imekufa GANZI,,,pale pale nikapata UJASIRI NIKASEMA MIMI hapa SIENDI PEMBENI,,maana huko pembeni kuna MAKORONGO ,, wakati natafakari ZILE LORI hizi hapa karibu yngu,,yaani zinakuja kwa pamoja mbele yangu,,,,zikiwa zimewasha taa fully..basi na Mimi sijuwi nilipata ujasiri GANI,, nikajikuta nimeng'ang'ania steering huku nakanyaga mafuta,,,kufumba na kufumbuwa nikajiona nimepita katikati ya yale malori lakini sijasikia kishindo,,au DALILI ya KUGONGA,,, na sehemu niliyopita katikati YAKE hata BODABODA HAIPITI..NIKAGEUKA NYUMA SIKUONA HATA DALILI YA GARI KUPISHANA NALO,,..HAPO nilikuwa natetemeka na gari ilizima kwa woga,,,,KESHO,,, nilipo muhadithia jamaa yng mmoja akaniuliza HIVI UNAJUWA YALE MARINGI YA SHABA,, WANAYOVAA MADEREVA WA MASAFA MAREFU MKONONI NI YA KAZI GNI? MFANO MADEREVA WA MALORI AU MABASI MAKUBWA YA MIKOANI,,,,WENGI WAO WANA MARINGI YA SHABA MKONONI,, nikamwambiya sijuwi,,akasema WAULIZE,,vinginevyo usipende kutembea usiku wa manane,,especially peke YAKO,, nikakumbuka kuna kitu natakiwa nikifanye kama DEREVA WA USIKU....
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa katupa chai ya MotoDah aisee sasa mkuu hukuona kama unatembea sana ukachoka ama ulitembea kiasi cha muda ule ule ila kutizama saa inasoma 9?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisikia busu la mwendokasi ndo hiloKuna siku ilikuwa 2007. Nikitoka Arusha kwenda Dar saa Saba Nane usiku nilikuwa napita maeneo ya kwedikwazu. Kuna mahala Barbara imenyooka Sana Basi nikawa natembea speed 100-120.
Kuna mrembo mmoja mdada akawa anasimamisha gari akiomba lift. Nikapiga taa kubwa kumwona vizuri mrembo haswaa, sikusimama nikanuoosha goti, huku najiuliza huyu anaenda Wapi saa hizi,. Bwana ile nampita kwa speed ile alinipiga busu Mara tatu hapo dirishani. Maana sikuwa nimefunga madirisha ili nipigwe upepo nisilale. Nilifika dar Sina raha kutwa nzima.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa natokea Dar nikiwa na pikipiki aina ya Honda Benly 250 niliyokuwa natoka kuichukua Bandarini ,sikutaka kuipandisha kwenye Lori,niliamua kuendesha mwenyewe kwenda mwanza ili nipate kutalii,safari ni ndefu mno ilikuwa,nilichoka sana hasa mikononi na begani,Nilipofika Singida niliamua kulala,lakini ilipofika saa 3 Usiku nikaamua kuendelea na safari na nikaghairi kulala kwa Sababu nilihisi mwili umepata nguvu.Mshukuru Mungu kwa kuwa upo salama mkuu
Jini hilo linawatokea wengi hapo sekenke hasa pale magari yanapoharibikaNilikuwa natokea Dar nikiwa na pikipiki aina ya Honda Benly 250 niliyokuwa natoka kuichukua Bandarini ,sikutaka kuipandisha kwenye Lori,niliamua kuendesha mwenyewe kwenda mwanza ili nipate kutalii,safari ni ndefu mno ilikuwa,nilichoka sana hasa mikononi na begani,Nilipofika Singida niliamua kulala,lakini ilipofika saa 3 Usiku nikaamua kuendelea na safari na nikaghairi kulala kwa Sababu nilihisi mwili umepata nguvu.
Nilipoanza kuteremka mlima Sekenke niliona mwanamke mrembo mno kwenye ile misitu usiku wa saa 5 eneo pweke lile lisilo na makazi ya watu zaidi ya mashimo marefu kando ya barabara ,mwanamke yule alikuwa akinisimamisha,nilipunguza mwendo na kuwasha full light ili nimwone vema,hakika alikuwa mzuri hasa,alivaa mtandio kichwani na gauni refu jekundu,alikuwa kama shombe wa kiarabu nilipomkaribia zaidi mwili wote ukasisimka ndo nikajikuta nazidisha mwendo kwa hofu,niliendesha kwa spidi ya kifo hadi Igunga,sikuendelea na safari nililala igunga ,hadi Leo huwa najiuliza sana juu ya mwanamke huyo wa ajabu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Duh hiyo ni kweli mkuu,sijawahi ona mwanamke mzuri vileJini hilo linawatokea wengi hapo sekenke hasa pale magari yanapoharibika
Wewe sio DEREVA.. huwezijuwa mambo ya MADEREVAUsingizi na mwendo kasi + mbuyu uko karibu na barabara = imani potofu!
Ukiwa sio DEREVA huwezi kujuwa mambo haya MKUU,,,Mawenge yake tu. Unafanya mchezo na usingizi vikichanganyika na giza!
Sawa MKUU,,, ila endelea kuranda usiku wa manane,,,utakutana na WENYE USIKUJamaa ni mzembe kabisa. Alifika kwenye korongo pikipiki ikaruka dada wa watu akadoka bila yeye kujua.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] huyo jamaa aliyepatwa mara mbili Nimecheka mpaka basiHahahahahhahahaaaa Huu uzi umenikumbusha kitu. Siko upande wa mauza uza ila nilifahamiana na dereva mmoja wa malori wa kukatiza nchi kama 4 hivi barani Africa. Siku moja tukiwa Bukoba akawa ananisimulia vitu anavyokutana navyo barabaeani kama dereva mchana na usiku.
Kikubwa wizi, majambazi na majangiri kuna eneo ukiacha kioo wazi wanakutupia kopo la nyuki au nyoka. Ndani ya Salina kadhaa lazima usimamishe gari kama so kulidondosha. Kifuatacho ni kupakua mizigo kisha wanakuacha uwe mzima ah umeumia hawana habari na wewe kisha wanapotelea maporini.
Kuna moja hiyo nilicheka nusura nijikojolee, naomba nisimulie kisa chenyewe kama alivonisimulia.
Jamaa yangu miaka hiyo aliajiriwa kwenye kampuni ya usafirishaji mizigo ya mwarabu mmoja wa mwanza japo alikuwa dereva tayari na alijua kuendesha. Wakiondoka na mzigo tajiri aliwaasa njiani kuna majambazi na majangiri na hawaishii kuiba tuu wanabaka pia aka kuwasodomise. Kweli wakaondoka na dreva wake kufika katikati ya pori wakawekewa kizuizi na majangiri dereva akashuka kujaribu kuwasihi wawaachie wapite na Yule utingo alibaki kwenye gari. Wakaja wakamshusha utingo wakawaambia mkitaka muende na mzigo tunachukua roba moja na tunambaka mmoja wenu. Daah wakiwa na hamaki wakasema tumshughulikie dereva utingo Rudi kwenye hadi fastaa. Kweli dereva akashughulikiwamaana aliendesha kwa tabu sana mzigo ukafika salama lakini hawakupata mzigo wa kurudi nao hivi hawakuwa na hela Yaani lori lilirudi tupu.
Siku wanarudi na mwanza yule dereva alimwambia utingo, endesha wewe mimi nipumzike kufika pori lilelile wakasimamishwa na majangiri walewale wakasema, mnarudi haya leo tumshughulikie utingo dereva pumzika, bila kusubiri wakaenda upande wa abiria wakamshusha yule jamaa na kumsodomise tena......(wakati ananisimulia nilicheka hatariii)
Yule dereva kufika kwa mwarabu akarudisha funguo kazi imemshinda.
Kisa kingine alichokutana nacho huyo jamaa yangu safari za mwanza bukoba hadi mpakani Uganda akiwa bado utingo alipata dereva ambae mkewe alikuwa na wivu balaa halafu mzigo na mtata. Maana siku majangiri wanaobaka wakiwepo kwenye pori mojawapo huwa malori wanaambiana na kukaa vituo eneo kabla ya pori na wakiondoka basi safari huendelea. Ilimpa wakati mgumu maana alimuaga mkewe naondoka jumatatu tunarudi alhamis Ila wakikutana na changamoto kama hizo za kuwakwepa majangiri wabakaji anakaa muda mrefu zaidi matokeo yake mkewe anahisi amepita nyumba ndogo. Akirudi hata na zawadi bado anakuwa na kibarua cha kumuelewesha mkewe kuwa kazi yao ni ngumu na mambo wanayokutana nayo barabarani hawezi kuelezea yote.
Siku ya siku mkewe akamwambia leo tutasafiri wote nione hizi changamoto mnazokutana nazo. Akamsihi sana mkewe bakii mkewe kagoma basi kishingo upande jamaa akakubali mkewe wasafiri wote. Hamad kati ya pori majangiri wabakaji hasa hapa, wakawashusha wote, wakasema leo mna mwanamke.... Basi nyie rudini kwenye gari leo acha tufaidi mbele na nyuma. Dereva machozi yalimtoka akiahidi day la hela kubwa Hata akope waapi sanasana aliambulia kupigwa na ubapa wa mapanga mgongoni. Mkewe kuona mmewe anataka kuuwawa, analogs kelele, basi muacheni navua nchi zote, walipomaliza mke karudi kwenye gari hoiii. Walipofika walikokuwa wanapeleka mzigo, mke akamwambia dereva, mume wangu nisamehe kweli kazi yenu in a changamoto, pole sana. Naomba nirudi na basi nyie hata mkikaa wiki mbili sina wivu tena. Alikuwa mpole maana alihisi jamaa atamuacha. Dereva akamwambia tulia tunarudi wote uzuri saa ya kurudi pori lilikuwa shwari.
Safari moja kwenye vilima vya iringa kuna maiti ya mwizi mmoja wa mizigo ya malori walimkamata wamapiga hadi akafa halafu wakamuweka kwenye kilima chenye kina kali yaani ukija na gari unastukia huyu hapa alikanywagwa na magari hadi akapotelea kwenye lami. Hilo eneo pakajaa mafuta meusiii.....
Kasinde.
Huu mtindo wa kusimamisha gari na kushuka kwenda kushuhudia ndio mnajitafuutia matatizo, wakati unaenda kutafuta ushahidi kamili, unafungua mlango unaenda unatizama, huku jini na yeye anaingia kwenye gari. Unarudi unawasha gari mpaka kwako, jini lishaingia kwako na linaanza vitimbi!Hapa jukwaani nani anavifahamu vyombo vya kioo? Ni Vitombe na Sahani za kioo! Basi siku moja natoka SHY kwenda Mhunze, kabla ya daraja nikakuta katikati ya barabara hivyo vyombo vimewekwa ugali ndani yake na kufunikiwa kama mtu ametengewa chakula, kikombe kimejaa maziwa! Cha ajabu kabla ya eneo hilo nilipishana na lori lakini halikuvigonga vile vyombo, sasa Mimi nikapunguza mwendo nikapita pembeni. Kama hatua ishirini hivi nikasimama nikarudi kucheki tukio, hamaaadi.sijakuta kitu chochote!!
Hukumuomba namba ya simu?Kuna siku natoka Mtwara nakuja Dar,,,kibabu kimoja,kikiwa na tenga kimeweka bata wawili,Akatuomba lifti anashuka mbagala,,tukamchukua,,chakushangaza ndio safari pekee ambayo nimesafiri bila kukaguliwa hata mara moja,na mbaya zaidi nilikuwa nimebeba MBAO NA Magunia ya Mkaa,,na hii njia yakusini,,ndio inaongoza kwa ukaguzi ,,hasahasa mageti ya maliasili,tulikuwa tukifika kwenye geti la maliasili,tunafunguliwa geti kama waheshimiwa,,,,tunaruhusiwa tu,,,natamani sana huyu babu niwe nambeba kila siku,,,mwisho wa safari babu akatuambia,,msiwe mnazarau watu,,hamjui wanamsaada gani kwenu,,haya safari njema,
Ungesimama labda alikuwa malaika mahaba yule umepoteza BahatiKuna siku ilikuwa 2007. Nikitoka Arusha kwenda Dar saa Saba Nane usiku nilikuwa napita maeneo ya kwedikwazu. Kuna mahala Barbara imenyooka Sana Basi nikawa natembea speed 100-120.
Kuna mrembo mmoja mdada akawa anasimamisha gari akiomba lift. Nikapiga taa kubwa kumwona vizuri mrembo haswaa, sikusimama nikanuoosha goti, huku najiuliza huyu anaenda Wapi saa hizi,. Bwana ile nampita kwa speed ile alinipiga busu Mara tatu hapo dirishani. Maana sikuwa nimefunga madirisha ili nipigwe upepo nisilale. Nilifika dar Sina raha kutwa nzima.
Sent using Jamii Forums mobile app
Walipitia hapo wangapi? na alisalimika na ngwengwe uyo mke?Aliendelea nae na wivu akaacha Ila ndo mke akajua ugumu wa kazi ya mumewe....
Usibishe usibishe ndg vitu hivyo vipo, hata baharini... Dunia ni kubwa na ina mambo na viumbe tofautiNdoto, usingizi na imani za kishirikina.
Hakuna kitu. Why usiku na si mchana??
Why barabarani tu na si njia ya train, Angani au Majini??.
Story za abunwasi na changamsha genge.
Nishasafiri Barabara nyingi, masaa yote kuspan 24 hours sijashuhudia hayo.
Ulongo tu na kutiana woga, kuwapa ulaji waganga wa kienyeji wafanye zindiko.