Kwa madudu anayoanika CAG, kumbe Magufuli uongozi wake ulikuwa sifuri tu

Kwa madudu anayoanika CAG, kumbe Magufuli uongozi wake ulikuwa sifuri tu

Ndiomaana alikua anahangaika na kufungia wanaharakati na vyombo vya habari ili uozo wake usijulikane yaani kaaibika hata hajaoza vizuri shwenzyyy
Yule haozi anateketea mzima mzima kama barafu inavyoyeyuka
 
Ukiwa dikteta na sheria sahihi wizi unaweza kuisha bana,,ila shida wapi uliona mtu aliyeiba pesa nyingi akafungw tz, unaiba mamilioni unafungwa miezi au,kifungo cha nje na kufagia mhimbili
Kwenye bold hapo tafadhali ushike adabu yako kabisa 😅 😅 😅
 
Mama Aanze Na CAG Huyu Afutwe Kazi Haraka
Alifumbia Maovu Wakati Aliyaona Hadharani
😣😏🤔💣🕶💦💨💫
Ukisema hivyo mama mwenyewe ataondoka kwa sababu yeye ndo alifuata baada ya aliyekuwa rais
 
Tulieni na bado, hapa mtamwelewa Lissu alipokuwa anasema jamaa ni FISADI mkasema anaichafua nchi !! CAG akianika yote mtabakia midomo wazi.
 
Ilani ya ccm 2020 - 2025 inasema tutaendelea kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote.


Haisemi ufisadi umeisha.

Hata Ulaya kina Morinyo, Messi, Ronaldo mara kwa mara tunasikia aamepelekwa mahakamani kwa kukwepa kodi.

Hata Chadema wabunge wengi walihama mwaka jana sababu ya ufisadi michango yao. Kinachotakiwa ni kuendelea kupambana na ufisadi
Watatusaidia kama watasema mahela waliyo hongwa kuhamia huko ambayo payment zake hazikulipiwa taxi
 
Tatizo la jiwe aliminya uhuru wa vyombo vyote vya habari ambavyo vingesimama kidete kufichua maovu kama haya,infact hata taasisi kama ya CAG aliminya kias kwamba wasingeweza kutoa madudu kama haya,leo hayupo uozo wote tutaujua,kumbe Naye alikuwa mpigaji tuuh
 
Mimi alipomkataa Prof Asad kwa kupitia ndugai walimvua viatu kwenye kamati yao ya kihuni niliumia sana kwa kweli nikajua hapa hakuna biashara tushapigwa ingawaje mwanzo nilikua naona Kama kuna kazi inafanyika mara sijui bunge live hakuna mara taarifa habari za itv ziungwe kutoka TBC nikajua kazi tunayo hapa watu wapo milion ya 60 harafu unagawa hela kama sandakalawe barabarani kwa wachache baada ya kutengeneza mazingira kwa wote ndio kwanza matajiri unawachukia...
 
Tatizo la jiwe aliminya uhuru wa vyombo vyote vya habari ambavyo vingesimama kidete kufichua maovu kama haya,infact hata taasisi kama ya CAG aliminya kias kwamba wasingeweza kutoa madudu kama haya,leo hayupo uozo wote tutaujua,kumbe Naye alikuwa mpigaji tuuh
Kitambo tu tangu ujenzi tulijua mbona.
Zile mbwembwe za kukataa kupokea barabara mbona alikuwa atupi mrejesho anapiga kimya.
Umewahi ona amewahi toa mrejesho kwamba hii niliikataa wamerekebisha.
Alikuwa ni janja janja propagandist Mkubwa huku akiminya uhuru wa habari.
 
Huwezi ukawa msafi kisha ukazuia bungelive.ukamuondoa Assad,ukauwa upinzani hali vyoote hivi ni tools za kufichua maovu.
 
mama hajawahi kuamrisha CAG asome kipi na aache kipi anataka unga umwagike wote
Wewe unafikiri ni kitu gani kilimuondoa CAG Prof. Assad???
Ni baada ya KUANIKA UPOTEVU WA Tshs. TRILLION MOJA( 1 T)......!!
 
Kitambo tu tangu ujenzi tulijua mbona.
Zile mbwembwe za kukataa kupokea barabara mbona alikuwa atupi mrejesho anapiga kimya.
Umewahi ona amewahi toa mrejesho kwamba hii niliikataa wamerekebisha.
Alikuwa ni janja janja propagandist Mkubwa huku akiminya uhuru wa habari.
Alizuia BUNGE LIVE kwa muktadha huohuo wa KUFICHA UOZA NA MADUDU YA SERIKALI YAKE YA HOVYO...!!!
 
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumechezewa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu
Tumehomolwa Sana Ndugu Zangu
Vyovyote Mtakavyosema Najua Mmenielewa!!😂😁


Nitapambana Na Rushwa Bila Kiguguzi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua 😅😄
Nimejipa Kazi Ya Mtumbua Jipu
Kumbe Anatupiga
 
Kule maliasili sheria za fedha ndo zilikuwa hazifuatwi kabisa, ni kana kwamba mtu analipa pesa kutoka mfukoni mwake.....hadi wasanii walikuwa wanajipatia pesa kiulaini pale.....hapo mtumishi wa umma unasota miaka sita huna hata nyongeza na kila siku unaamka alfajiri kuwahi kazini, dah! haya mambo...
 
Mtanikumbuka Siyo Kwa Mabaya Lakini Kwa Mazuri
Haa 😂😁😀😀
Tanzania Ni Tajiri
Walikuwa Wanapiga Tu. Sheria Ipitiwe Upya
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
CAG Alikuwa Wapi Wakati Wa Jiwe 👄
Naamini kama angekuwepo, basi haya yote tusingeyasikia! Ingeandaliwa ripoti nyingine kabisa yenye masifu mengi na kika aina ya pongezi.

Prof. Assad na uswahilina wake, alipoulizwa swali la papo kwa papo kama kuna hela kiasi cha trillion 1.5 zimepotea na hazijulikani zilipo, alikataa kata kata! "Hapana Mheshimiwa Rais" 😁😁😁
 
Kama unabisha nenda huko Facebook kila post ninazosoma wananchi wamecharuka balaa.

Ukitaka ucharukiwe basi mzushie baya JPM.

Wakuu hakika huyu alikua ni mtu wa Mungu. Na nilichogundua wananchi hawatoweza kuelewa chochote yaani ni wanampenda JPM.
Ngoja niendelee kusoma post Facebook.
 
Back
Top Bottom