Kwa madudu anayoanika CAG, kumbe Magufuli uongozi wake ulikuwa sifuri tu

Labda ni akina Mama wapika vitumbua ambao walidanganywa na Propaganda za CCM bashiru.
 
Utawala wa Hayati Magufuli hakika ULIJAA MAIGIZO NA USANII MKUBWA ULIOKUWA UKIRATIBIWA KWA UMAKINI MKUBWA SANA!!
Hapa ndipo Watz tunapoanza kuelewa kwanini Jiwe hakutaka haya yafanyike:
  1. BUNGE LIVE kuficha hoja na ukosoaji wa Wabunge wa KUB.
  2. Timuatimua ya Wabunge wa Upinzani Bungeni wasionekane Bungeni.
  3. Kamatakamata ya Wabunge na kuwafungulia Kesi za kughushi.
  4. Kupiga marufuku na kuzuia mikutano ya Wapinzani au Vyama vya siasa.
  5. Jaribio la kumwua Tundu Lissu kunyamazisha ukosoaji.
  6. etc, etc.
Bado kuna mengi yajayo yatashangaza na kuwaacha Watz midomo wazi!!!
Huu ni wakati wa Watz kutafakari na kuchukua maamuzi sahihi kwamba UTAWALA WA CCM HAUAMINIKI TENA....!!!
LAZIMA TWENDE NA TUNDU ANTIPAS 2025, ENOUGH IS ENOUGH!!!
 
Inabidi mama asafiri kwenda Rwanda kujifunza kutoka kwa kagame!
 
Assad na yeye ana makando kando yake mengi sana pale NSSF alivyokuwa mjumbe wa bodi. Hata Kichere anaye rap rap sasa hivi kuna madudu kibao kafanya TRA. Kwa sisi tunaojua Audit inafanyika vipi, haya yanayotokea tunaona porojo tu. Na ndiyo maana conclusion ya audit report huwa inasema opinion ya Auditor haiwezi kutumika kama ushahidi mahakamani. Unadhani kwa nini huwa wanasema hivyo???
 
Kwa huu ushahidi wa ripoti ya CAG Magufuli alikuwa mwizi,fisadi,mzembe na mtu asiejali maslahi ya wanamchi.
 
Wewe unayejua kwanini wanasema hivyo ungetuambia ambao hatujui...

Kicheere na Assad kuwa na makando haiondoi ukweli kuwa mtetezi wa wanyonge na kinara wa kutumbua mafisadi naye alikuwa fisadi aliyekubuhu....

Tunamshukuru Mungu kwa mapenzi yake...
 
"NAAAM....!

Miradi yake mingine inaleta foleni na mingine hasara? Ni rahisi tu, kwa nini tuendelee na Ma-foleni na Ma-hasara? ...Nashauri Vunjeni Madaraja na Flyovers zote, Ng'oeni reli zote especilly SGR, uzeni Ndege zote na vivuko vyote nchini, Uza Meli zote Mpya zilizozinduliwa, kule Ziwa nyasa, simamisheni Ujenzi wa Bwawa la umeme, Gaweni Migodi yote, Binafsisheni Milima, Maziwa na Mbuga.

Bomoa Bandari zote zilizoboreshwa ikiwemo Mtwara, Tanga na Dar, Jengeni moja ya Wachina kwa mkataba wa miaka 100...rudisheni Ada shuleni tukuze uchumi, Wapeni Matajiri Exemptions za kodi, Ruhusuni Makinikia kwenda nje, Vunjeni Masoko mapya ya Madini mikoani, ...Charaza Bakora Machinga mjini, Mwaga wali wa Mama Ntilie.

Vunja vyama vya wakulima na utaratibu wa stakabadhi ghalani, Ruhusuni Uhuru wa Mashoga, Mateja kwa wingi mtaani, madawa ya kulevya n.k....pia Msisahau kuifunga ile Mahakama ya Mafisadi,....kwa uchache tu Hakika hapo sasa pengine Tanzania itakuwa kama ULAYA, Tanzania ya Asali na Maziwa!.

Vunjeni makao makuu Dodoma mrudishe serikali Dar.

Hapo sasa mtakuwa mmemkomoa Magufuli na watoto wake watashinda njaa ili anyooke kabisa.



Nawasilisha
 
Mzee akifufuka leo anaweza kuzimia tena kwa hasira za watu
Jiwe namfananisha na bossi mmoja aliyekuwa akiwabana wa chini yake wasile Ili wakija kuchunguza wamkute ni msafi kumbe anawabana sana wa chini wengi huku anazipiga na wajuu wachache.
 
Tulieni na bado, hapa mtamwelewa Lissu alipokuwa anasema jamaa ni FISADI mkasema anaichafua nchi !! CAG akianika yote mtabakia midomo wazi.
Hayo tu yanatosha maana hatukuyajuwa awali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…