Kwa maisha wanayoishi ndugu zake Harmonize halafu nikimuona anatoa mil 9 kwa wengine, inaniuma sana

Kwa maisha wanayoishi ndugu zake Harmonize halafu nikimuona anatoa mil 9 kwa wengine, inaniuma sana

Kwa wanaowafahamu ndugu zake na Konde boy Mtwara halafu Dogo akifika Dar anagawa Pesa kwa wengine inaniuma sana hata kama siyo ndugu zangu! Ingefaa dogo aanze kuwasaidia ndugu zake kwanza wote watoke kimaisha, ndipo umwage pesa ovyo ovyo kuliko kufanya hivi wakati ndugu zake walio wengi tunaowafahamu bado wanapambana na hali zao kwa kulima mhogo huko Mtwara

Kwa watu wa Mtwara mtaelewa ninachokisema na kukimaanisha hapa, tofauti na wanaume wa Dar


Kick za wasanii wa bongo fleva ni za kijinga sana....ndiyo maana mimi huwa sina muda nao hata kidogo.
 
Akiwapa ndugu zake hatutajua,wcb wanaishi kwa kiki
 
Mkuu kumsaidia mtu hata kama ni nduguyo si lazima ni hiari sasa wote wa mwangalie yeye kwa nini na wao wasijitahidi angalau wakatoka ki vingine? Nitamlaumu tu kama atakuwa kasahau mama basi
Itikadi za ubinafs ndugu yako huwez kumuacha kumsaidia ikiwa unauwezo wa kumsaidia..ndio mana wahindi wanawatuma coz ya ubinafsi
 
Ye mwenyewe anasaidiwa tu pale alipo. Ndio akili zetu waafrika hizo, ubashikwa mkono kusaidiwa tu then unaanza kujiona una uwezo saaana unataka kuwashika mikono na watu wengine. Tufanyeni kazi sio kutegemea jasho la mtu mwingine tu.

Na wengine ndio hawasaidiki hata ungefanya nini yaani wanakuwa kama makinda ya ndege kazi kuachama midomo kila kinachotua kiotani. Ungewashauri wapambane wafanye jazi kwa bidii ili wawe na muonekano kama wa huyo mayonaizi.
 
Kwa Mimi ukiwatoa baba na mama, kaka zangu na dada zangu! Hao ndugu wengine wapambane na hali zao
Kwanza ni baba na mama tu hawa dada na kaka wanaingia kwenye equation sababu ya baba na mama.Wafanyekazi nao wanisaidie khaa kwa hiyo mtu asifurahie maisha kwa sababu ya wavivu wengine alah!
 
Itikadi za ubinafs ndugu yako huwez kumuacha kumsaidia ikiwa unauwezo wa kumsaidia..ndio mana wahindi wanawatuma coz ya ubinafsi
Una uhakika gani kwamba hawasaidii ulitaka aite vyombo vya habari ili watoe akiwahudumia? Hao ndugu wamelalamika? Kumbuka aliyeleta huu Uzi si ndugu, pia narudia msaada si lazima ni hiari, wewe kama unajilazimisha kuhudumia ndugu endelea kujilazimisha lakini Mimi nitasaidia pale ninapojisikia na kamwe sitojilazimisha
 
Umeambiwa wanalima NA wako hai, inamaanisha wanajitahidi. Huyu ndugu H angeweza kuwasaidi kuwekeza kwenye hicho kilimo chao, kuwanunulia trekta NA kuongeza mashamba, hiyo familia ingebadilika kimaisha.

yeye aliwezeshwa na ndugu gani
 
Kwani kulima mihogo ni ufukara?hebu acha dharau basi kwa wakulima!
 
Wabongo bado mmelala
Huu sio wakati wa kusubiri usaidiwe na mjomba
Tafuta chako kwa nguvu zako
Huyo Harmonise amepambana hadi kufika hapo,na huwezi kumpangia mtu mzima matumizi ya pesa alioipata kwa jasho lake
 
Back
Top Bottom