Kwa maisha ya kawaida ya Mtanzania, angalau awe na kipato cha shilingi ngapi kwa mwezi ndio aweze kuoa?

Kwa maisha ya kawaida ya Mtanzania, angalau awe na kipato cha shilingi ngapi kwa mwezi ndio aweze kuoa?

Joined
Jul 21, 2013
Posts
13
Reaction score
13
Amini kwamba unaweza kua na kibarua cha kawaida tu ambacho kinakupa walau laki 6, 7 - 8 kwa mwezi na ukakosa mke. Wasi wasi ukiwa ni kipato hakitoshi.

Je mliofanikiwa hapa mlianza vipi?

1645781329123.png
 
Mkuu budget hutofautiana kutokana na;
1. Makazi sijajua unaishi wapi kijijini, mjini, uswazi au ushuani.
2. Uko bachela au una familia yenye idadi ya watu wangapi.
3. Je, kama familia mnaproject au lengo gani la muhimu mnalotekeleza iwe ujenzi, ununuzi wa gari au biashara.
 
Ukioa kupe a.k.a slay queen jiandae kutoa kilio chenye kamasi. Hata kama una kipato cha 3M kwa mwezi kamwe usidiriki kuoa mwanamke anayebinua makalio TikTok utakuja kujuta.

Mwanaume mwenye uhakika wa kuingiza fedha kiasi chochote ana uwezo wa kuwa na familia. Suala la kuoa ni utayari.
 
No money no marriage

At least uwe na kipato Cha 300k kwa mwezi na uwe nakichwa chaku scan icho kipato chako vizuri ili ujue namna yakukitumia .. vinginevyo utagombana na watu bure .. siyo kila kitu ni kwaajili ya kila mtu . Wengine pambaneni mpate watoto tu Kwanza na akina mwajuma then tafuteni pesa NDOA IPO TU...

Ndoa zimewashinda adi kina billgate uko

Ndoa isiwe sababu ya wewe kuishi Kama mjusi (kupauka from January to December .)

NB: never risk your life for anyone..
 
Kabla ya kuoa angalia sana mwenza wako kama ana hofu ya Mungu, angalia tabia zake, usipuuzie vitu vidogo ukiamini utambadilisha.

Ni vyema kuoa mtu ambae utaweza kumtolerate kwa hali yoyote, unaweza ukampenda mtu sana lakini ukashindwa kuishi nae huyu hufai kumuoa.

Ndoa ni zaidi ya mapenzi na zaidi ya pesa, Ndoa ni kitu ambacho kinatakiwa kikupe amani, utulivu wa nafsi, baraka na furaha.
 
Exactly
 
Kuoa Ni kumuomba mungu tu akuwekee mkono wake.

Ukisubiri upate pesa ndio uoe, Unaweza ukafa na useja wako mpk unaingia kaburini.

Wengine pesa au Riziki wamezipata baada ya kuoa.
Na wengine tumefilisika baada ya kuoa
 
Back
Top Bottom