Kwa maisha ya kawaida ya Mtanzania, angalau awe na kipato cha shilingi ngapi kwa mwezi ndio aweze kuoa?

umetisha Ratio analysis inahusika hapo, no.3 inabeba vyote
 
Wengine walioa ndio wakafilisika na kuongea wenyewe barabarani na wengine wakavuka mpaka na kuokota makopo!

Kwa upande wa kipato Jitahidi ukidhi mahitaji ya familia mengineyo ni majaaliwa
 
Kuoa kunakuja na majukumu. Baada ya hapo utaitwa baba.Jitathmini kama unaweza kuimudu familia kwa chochote kitu maana mbali na mapenzi ndoa ni majukumu.
 
Mbona tulisha kubaliana humi kwamba wanaume tusioe...??
 
Muuza Genge - ana mke!
Konda - ana mke!
Kuli sokoni - ana mke
 
Wengine wameoa kwa mkopo maisha yanaendelea,Usifanye mambo kuwa magumu wakati hujajua ugumu wake.
 
Huu ni uzinifu. Usiharalishe dhambi. #kataa dhambi inaua mapema
 
Ukweli utabaki palepale ndoa nidaraja la kukuingiza kwenye majukumu. Jambo la kutia moyo ni kwamba baraka za maisha ni zawadi ya Mungu. Hivyo, usiogope kuoa kisa kipato bali ogopa kuoa ikiwa mind Yako haijawa tayari kubeba majukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…