Kwa Makala Hii ya Daraja la Kigamboni Mwanakijiji Kachemsha

Kwa Makala Hii ya Daraja la Kigamboni Mwanakijiji Kachemsha

You don't need to have followers, you need to feed hungry mind, mimi ni follower wake, ila kama chakule ni kile, basi kimechakachuliwa! lazima kuna emotional au saikolojiko problem somewhere! atapike tu kila kitu!
Mkuu Waberoya, MMKJJ ni mpishi, yeye anapika kwa utaalamu wake wa mapishi, liwe ni pilau, biriyani, wali mweupe, mseto etc, yote ni mapishi ya wali, na akishaivisha hupakua, akishapakua, mkataba wa mpishi ndio umeishia hapo, sasa jukumu la kula ni la walaji kina mimi wewe na sisi, katika ulaji ndipo utaamua ule pilau, biriani, wali mweupe etc kwa kadri moyo wako umependa nini, hata ukiweza kula vyote, huwezi kusema hili pilau la leo hamna kitu,mambo yote ni biriani, kisa tuu juzi ulikula pilau la pishori pale kwa Bakhresa!. Wakati wewe ukisifu biriani, wengine kwao biriani sii lolote bali kwao mambo yote ni pilau, ndio maana hata "ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno", sasa unaweza shangaa hilo hilo gazeti wengine wanafungia samaki na maandazi, wengine ndio unakuta wameibandika ukutani pale feri kwenye kile kibanda cha chipsi vumbi, na kwenye uchaguzi huo huo wa vyakula, wengine hata kulinunua gazeti hilo hawaligusi kabisa, wao gazeti la ni Uhuru/Mzalendo!. Ni mambo tuu ya mapishi, mlaji ndio huchagua ale nini!.
 
Hata mimi sijawahi kuona faida ya daraja hilo for sure,

Wangeweza kutumia fedha hizo kujenga mtandao wa reli au something else..

Nafikiri kuna mkono mkubwa wa investors;

Topical,

..kuna bandari ya DSM ambayo inahitaji kukarabatiwa na kupanuliwa.

..kuna kiwanja cha ndege ambacho kiko ktk hali mbaya.

..zaidi kuna reli ya kati na kuna kipande kingine cha kwenda Rwanda.

..sasa kwanini hawawekezi hayo mapesa kwenye miradi which will open up our country for more and better local and foreign investments??

..kwa mtizamo wangu tunahitaji kupeleka fedha zaidi mikoani na siyo kuanza kuzifuja hapa DSM.
 
Mwanakijiji na wewe unamkuza sana bana! aagh

Huyu hawezi kuandika story zake zaidi ya kulenga yafuatayo:-

a. Pro nyerereism b. Against wazanzibar (wanaopinga muungano) c. Against JK d. Islamophobia

Tangu aanze kuandika na atabaki hivyo kwasababu ni maradhi yake makubwa hana lolote..

Niliishamweleza kuwa hawezi kumtetea Nyerere, Nyerere anajitetea, ......washington anasemwa mpaka leo kwa mabaya na mazuri

kuna pressure ambazo huwa hazisaidii.....na bifu ambazo huwa hazijengi!

kwa wengine Nyerere is just a Mere Mortal, kwa wengine ni mtume!!
 
Ni simple sana kumlaumu magufuli kwa Kuuza nyumba lakini
  • Halikuwa wazo lake...( Nadhani watu wakijua ushauri huo k mwara ya kwanza ulitolea na kupewa msukumo na nann watashangaa)
  • kama waziri mwenye dhamana hakuwa na kura ya VETO
  • Zaidi ya hapo kabla ya kushinda uras jK mwenyewe alitumia gia kuwa atazirudiaha . Sasa ama Rais kameshndwa magufuli ni kumtoa kafafa
Kwangu kuuza hizo nyumba sio issue sana kama kungekuwa na mpango kuwa tunawauzia "wazee wetu"nyumba za masaki then serikali inatengeza masaki nyingine mbagala, tandika , ubungo, etc After ten years hivyo hivyo. Walau tungekuwa na "vimasaki" kibao na kila mkoa kungekuwa na so called "uzunguni" sehemu mbali mbali. Sio mpaka leo "uzunguni" tulizano ni zile za mkoloni .

Njia nyigine mbadala ingekuwa kuuza nyumba za masaki ili viongozi watawanyike. Nyunba mbili zijengwe au zinunuliwe sinza ,mbili ubungo, mbili tandika Mbili upanga., , mbagala etc.

Kwa stye hii viongzi wangekuwa karibu na jamii na hata matatizo na kero mbali mbali za maji, umeme, etc basi wangeya feeel au wageona labda impulse zao zingeshtuka wa act kwa haraka.
 
..mpaka sasa hivi sijui faida za ujenzi wa hili daraja ni zipi.

..je, ktk madaraja yote yanayotakiwa kujengwa, hili la kigamboni lina umuhimu kuzidi hayo mengine?
Mkuu Joka Kuu, tafuta master plan ya Kigamboni New City, hakuna mji kama huo bara zima la Afrika, kama umepita Doha hivi karibuni its something like that!, ukishaona ndipo utaliona hilo daraja umuhimu wake, Oysterbay na Masaki ni cha mtoto!.
 
Topical,

..kuna bandari ya DSM ambayo inahitaji kukarabatiwa na kupanuliwa.

..kuna kiwanja cha ndege ambacho kiko ktk hali mbaya.

..zaidi kuna reli ya kati na kuna kipande kingine cha kwenda Rwanda.

..sasa kwanini hawawekezi hayo mapesa kwenye miradi which will open up our country for more and better local and foreign investments??

..kwa mtizamo wangu tunahitaji kupeleka fedha zaidi mikoani na siyo kuanza kuzifuja hapa DSM.

Reli ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote kwa sasa hivi.

Magufuli ameingia kwenye mtego wa ule mradi wa 'mji wa kimataifa'

NSSF wakishajenga daraja, watajenga majengo mengi sana kigamboni, that is where the direction is.......
 
Mwanakijiji na wewe unamkuza sana bana! aagh

Huyu hawezi kuandika story zake zaidi ya kulenga yafuatayo:-

a. Pro nyerereism b. Against wazanzibar (wanaopinga muungano) c. Against JK d. Islamophobia

Tangu aanze kuandika na atabaki hivyo kwasababu ni maradhi yake makubwa hana lolote..

Lol Topical japo mimi si mwanakijiji ebu tufafanulie U
Unatakiwa uwe Pro nani ili usiwe na maradhi makubwa au usiwe na maradhi kabisa. Au unatakiwa uwe against nani ili dunia ikuone mzima na utende haki.

otheriwise kila mtu na upande una maradhi yake makubwa kinachobaki ni yepi yenye hoja
 
Mkuu Joka Kuu, tafuta master plan ya Kigamboni New City, hakuna mji kama huo bara zima la Afrika, kama umepita Doha hivi karibuni its something like that!, ukishaona ndipo utaliona hilo daraja umuhimu wake, Oysterbay na Masaki ni cha mtoto!.

Yes Pasco, it is a nice city, do we need it now?? kwa nini tutake 'ukisasa' wakati uhalisia badon hatujafika hata karne ya 18?? wakoloni walikuja kutafuta malighafi miaka ya 1700s kwa sababu ya industrial revolution? tumefikia hatua hiyo? nchi ambayo hatuwezi kuzalisha hata toothpick, tunawaza ukisasa!!! kule zitajaa hotel na gest tu na dada wa ohio wata hamia kule, HAKUNA FAIDA YA MRADI HUU KWA MTANZANIA WA KAWAIDA....this is what I expected mr. mwanakiji to point out!! hata kama litajengwa..let them know that other Tanzanians think higher than them!!
 
Lol Topical japo mimi si mwanakijiji ebu tufafanulie U
Unatakiwa uwe Pro nani ili usiwe na maradhi makubwa au usiwe na maradhi kabisa. Au unatakiwa uwe against nani ili dunia ikuone mzima na utende haki.

otheriwise kila mtu na upande una maradhi yake makubwa kinachobaki ni yepi yenye hoja

Friend..just have an open mind! mwanakiji hata ule uozo wa wazi wa Nyerere atautetea tu!! unajua unaweza kumpenda mtu ukawa kichaa, MM is mad about Nyerere! ukimchukulia Nyerere kama binadama aliyekuwa na uwezo mzuri na mapungufu mengi tu, hutapata shida kufanya evaluation!
 
This guy Magufuli is the Greatest fake politician Tanzania has ever experienced. Watch this space as this Saga unfolds!
 
Ni simple sana kumlaumu magufuli kwa Kuuza nyumba lakini
  • Halikuwa wazo lake...( Nadhani watu wakijua ushauri huo k mwara ya kwanza ulitolea na kupewa msukumo na nann watashangaa)
  • kama waziri mwenye dhamana hakuwa na kura ya VETO
  • Zaidi ya hapo kabla ya kushinda uras jK mwenyewe alitumia gia kuwa atazirudiaha . Sasa ama Rais kameshndwa magufuli ni kumtoa kafafa
Kwangu kuuza hizo nyumba sio issue sana kama kungekuwa na mpango kuwa tunawauzia "wazee wetu"nyumba za masaki then serikali inatengeza masaki nyingine mbagala, tandika , ubungo, etc After ten years hivyo hivyo. Walau tungekuwa na "vimasaki" kibao na kila mkoa kungekuwa na so called "uzunguni" sehemu mbali mbali. Sio mpaka leo "uzunguni" tulizano ni zile za mkoloni .

Njia nyigine mbadala ingekuwa kuuza nyumba za masaki ili viongozi watawanyike. Nyunba mbili zijengwe au zinunuliwe sinza ,mbili ubungo, mbili tandika Mbili upanga., , mbagala etc.

Kwa stye hii viongzi wangekuwa karibu na jamii na hata matatizo na kero mbali mbali za maji, umeme, etc basi wangeya feeel au wageona labda impulse zao zingeshtuka wa act kwa haraka.

kuna kota ambazo magufuli aliwajengea mawaziri, kwani walizikubali?? nyoo walizikataa kuwa hazina hadhi yao! magufuli alitaka kuadopt system za asia, lakini tunavyopenda starehe tukakataa , hili huwa hawalisemi!
 
Yes Pasco, it is a nice city, do we need it now?? kwa nini tutake 'ukisasa' wakati uhalisia badon hatujafika hata karne ya 18?? wakoloni walikuja kutafuta malighafi miaka ya 1700s kwa sababu ya industrial revolution? tumefikia hatua hiyo? nchi ambayo hatuwezi kuzalisha hata toothpick, tunawaza ukisasa!!! kule zitajaa hotel na gest tu na dada wa ohio wata hamia kule, HAKUNA FAIDA YA MRADI HUU KWA MTANZANIA WA KAWAIDA....this is what I expected mr. mwanakiji to point out!! hata kama litajengwa..let them know that other Tanzanians think higher than them!!

Mkuu Wabe, nadhani hakuna ubaya tukithink 100years ahead!. Walalii wote sasa wataishia Tanzania, mimi Venice nimeiona kwenye picha tuu na ule ukanda wa mahoteli kule Rio, ndio Kigamboni its like a dream!.
 
Kuna ubaya sana mkuu! hizo nyumba zikijengwa leo miaka 100 ijayo hazitafurahishahata spanlife ya concrete structures in 30 yrs to 120 yrs!! tulitakiwa kuweka base fulani ya maisha na uchumi.....baada ya hapo tunaanza kupaa kama DUBAI, ambayo sasa inaongoza duniani kwa boom in construction, architects zake are best worldwide, technology is admirable...........hizo dream structures are similar to what it is in NY now!! aren't they?
 
Reli ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote kwa sasa hivi.

Magufuli ameingia kwenye mtego wa ule mradi wa 'mji wa kimataifa'

NSSF wakishajenga daraja, watajenga majengo mengi sana kigamboni, that is where the direction is.......
Nyie wote mnchoshindwa ni uvivu wa kusoma na kutafuta infos.
Daraja la kigamboni ni investment ya maana kwa bandari ya Dar
Expansion of container terminal kurasini, na daraja la kigamboni vinahusiana na Southern corridor initiatives under SADC.
Hilo daraja ni source of forex a.k.a hard currency.
 
This guy Magufuli is the Greatest fake politician Tanzania has ever experienced. Watch this space as this Saga unfolds!

sure he is!!

what should we do?? just talk and talk?? he is fake...yet he is a minister! what a joke, are all of us fake???
 
Vita ya Mwanakijiji kwa Magufuli sio ya kwanza, kuna thread alishawahia anzisha baada ya Magufuli kutoa lugha chafu kwa wakazi wa Kigamboni. Wataalamu wa mambo tunajua nini maana yake. So long as JF ni mchanganyiko wa watu wengi wanaoweza kuchambua mambo kwa upana zaidi, pumba na mchele vitatenganishwa kadri zitavyokuwa zinaletwa. Ni kazi ndogo kujua kalamu ya mwandishi inatumia wino wa aina gani especially kipindi hiki ambacho mapema kabisa kuna watu walishaanza kunyosha shingo zao na kupasha misuri kuelekea magogoni
Uvivu wa kufikiri ndio unatufanya tuamini kuwa Mafuguli ndio mwanzilishi hasa wa zoezi la kuuza nyumba za serikali wakati wa serikali ya awamu ya tatu. Na tunakuwa wavivu zaidi napoamini kuwa ni Magufuli tu, kwa uwezo wake wa hoja aliweza kuliconvice baraza la mawaziri lilidhie uzwaaji wa nyumba za serikali. Itakuwa ni busara kufikiria mchakato mzima kabla ya kufika Cabinet huanzia wapi. Kuna mwanafilosia mmoja alishawahi kusema "IN ANY DECISION THERE IS ONLY ONE WHO THINK, OTHERS JUST SURPPORT THE DECISION". To be able to think one must have a social capital eneugh to convice others in the cohort. Sifa kubwa ya Magufuli anapokuwa waziri ni kuwa askari wa mwamvuli mzuri, hii ndio inayomtafautisha na mawaziri wengi.
Hii ngoma bado mbichi sana
 
Nyie wote mnchoshindwa ni uvivu wa kusoma na kutafuta infos.
Daraja la kigamboni ni investment ya maana kwa bandari ya Dar
Expansion of container terminal kurasini, na daraja la kigamboni vinahusiana na Southern corridor initiatives under SADC.
Hilo daraja ni source of forex a.k.a hard currency.

1. kuliko reli? describe!
 
Vita ya Mwanakijiji kwa Magufuli sio ya kwanza, kuna thread alishawahia anzisha baada ya Magufuli kutoa lugha chafu kwa wakazi wa Kigamboni. Wataalamu wa mambo tunajua nini maana yake. So long as JF ni mchanganyiko wa watu wengi wanaoweza kuchambua mambo kwa upana zaidi, pumba na mchele vitatenganishwa kadri zitavyokuwa zinaletwa. Ni kazi ndogo kujua kalamu ya mwandishi inatumia wino wa aina gani especially kipindi hiki ambacho mapema kabisa kuna watu walishaanza kunyosha shingo zao na kupasha misuri kuelekea magogoni
Uvivu wa kufikiri ndio unatufanya tuamini kuwa Mafuguli ndio mwanzilishi hasa wa zoezi la kuuza nyumba za serikali wakati wa serikali ya awamu ya tatu. Na tunakuwa wavivu zaidi napoamini kuwa ni Magufuli tu, kwa uwezo wake wa hoja aliweza kuliconvice baraza la mawaziri lilidhie uzwaaji wa nyumba za serikali. Itakuwa ni busara kufikiria mchakato mzima kabla ya kufika Cabinet huanzia wapi. Kuna mwanafilosia mmoja alishawahi kusema "IN ANY DECISION THERE IS ONLY ONE WHO THINK, OTHERS JUST SURPPORT THE DECISION". To be able to think one must have a social capital eneugh to convice others in the cohort. Sifa kubwa ya Magufuli anapokuwa waziri ni kuwa askari wa mwamvuli mzuri, hii ndio inayomtafautisha na mawaziri wengi.
Hii ngoma bado mbichi sana

sasa mabifu hayo yanamnyima uwezo wa yy kufikiri
 
kuna kota ambazo magufuli aliwajengea mawaziri, kwani walizikubali?? nyoo walizikataa kuwa hazina hadhi yao! magufuli alitaka kuadopt system za asia, lakini tunavyopenda starehe tukakataa , hili huwa hawalisemi!

Mimi kwa kweli sielwi hi kasumba ya nyumba za viongzoi kujengwa sehemu moja kama kambi . hii yote labda matatzo halisi yanayokumba jami kama imgao wa maji na umeme usiwaathiri so called "viongozi" Lakini wao wanatoa hoj nyepesi ya "Usalama".

NI hizo kota kuona haziwafa ni i sababu tayari mtu akiwa waizir anaona ni first class citzen. Si umesikia nyumba ya spik ina swimming pool. Sijui hata kama ikulu ipo . Ina maana hata hakuna standard maalum Nyumba za viongozi ziweje. Kuna mwingine alikataa nyumba akw anaishi Hotelini( New africa). Kwa hiyo mtu ndo anaamua hii inanifaa hii hainifai. yenye vyumba vitatu ni ndogo yenye vyumba sita ni kubwa. lol.

Unakuta nyumba ya mkurugenzi wa halamashauri ni ya Miliono 500 ya RC ni ya Mill 250
 
Magufuli na daraja la Kigamboni, tushangilie?: Na M.M. Mwanakijiji

Nina uhakika katika siku za usoni Dar es Salaam watu watakuwa wanakuja kuangalia madaraja na mabarabara badala ya kuja kuangalia msongamano – Dk. John Magufuli (wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigamboni).

Siku ya Jumatatu kile kinachoitwa "ndoto ya daraja la Kigamboni" kilioneshwa kuwa kitaanza kutimia baada ya makubaliano ya ujenzi wa daraja hilo ambayo yatashirikisha serikali ya Tanzania, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kampuni ya China kutiwa saini. Watu wengi ambao labda kutokana na kutokujua historia au kutokutaka kujua historia wameonekana kushabikia kwa furaha hatua hii ya sasa kana kwamba ni zawadi na neema ya Mungu kwa Watanzania.

Dk. Magufuli, Waziri wa Ujenzi akizungumza katika hafla ya kutia sahihi makubaliano hayo alizungumza na kujaribu kushawishi watu waamini kuwa hatua hii imefikiwa baada ya uongozi mzuri wa Rais Jakaya Kikwete na hivyo wananchi waunge mkono na inaonekana wafanye hivyo bila kuuliza maswali!

Daraja la Kigamboni si zao la fikra za Kikwete

Katika kitu cha kushangaza kabisa ni kuwa Jina la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere halikutukuzwa katika hafla hiyo. Ni katika kile ambacho nimekiita kuanzia mwaka jana kuwa ni "juhudi dhaifu za kulifuta jina la Nyerere" katika mchango wa maendeleo. Katikati ya miaka 1970 ni uongozi wa Mwalimu Nyerere uliofanya upembuzi yakinifu wa kina wa ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Wazo la ujenzi wa daraja hili haukutokana na serikali ya awamu ya nne kama Magufuli anavyotaka watu waamini! Ni wazo ambalo lilikamilika na kufanyiwa utafiti miaka karibu arobaini iliyopita.

Ubunifu wa michoro ya daraja ilikuwa imekamilika mwaka 1977 miezi michache kabla ya nchi kwenda vitani na kabla ya ukame uliofuatia mapema miaka ya 1980. Kwa wanaokumbuka watahusisha kuwa ni utawala huo huo wa Nyerere uliofikiria na kufanyia upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Stielger's Gorge ambalo lingeweza kuzalisha umeme wa zaidi ya MW 2000 na kuliondoa taifa katika tatizo la umeme. Gharama ya ujenzi wa Stielgers wakati ule ilikuwa kama dola bilioni 1.2 wakati ujenzi wa Kigamboni kwa fedha za wakati ule na kwa michoro iliyotolewa wakati ule ilikuwa ni kama dola milioni 28.6.

Kwa hiyo, tuweke rekodi kwa usahihi kwanza – huwezi kutenganisha mpango wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni au baadaye Stielger's George na mawazo ya Rais wetu wa Kwanza – Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Najua wengine watachukia, wengine watakereka lakini ukweli ni kuwa hawakuja na mawazo mapya! Hata hilo daraja la "Mkapa" si wazo la Mkapa!

Gharama ya ujenzi haijabadilika sana

Kama kweli – na sina shaka ni kweli – kwamba wazo la ujenzi wa daraja la Kigamboni ni wazo la miaka karibu arobaini iliyopita basi leo hii kusainiwa kwa mkataba huu kumekuja kukiwa kumechelewa sana. Ni wazi kuwa mazingira ya mebadilika na hivyo upembuzi yakinifu mpya ulihitajika.

Sasa hivi katika mpango wa sasa daraja litakuwa na njia sita (si mbili kama ilivyopendekezwa zamani) na urefu wake ukiongezwa kwa karibu mita mia moja zaidi na ikitumia bila ya shaka teknolojia na utaalamu ambao haukuwepo miaka arobaini iliyopita (japo kanuni za fizikia na uhandisi nyingi ni zile zile).

Leo hii tunaambiwa gharama ya ujenzi wa daraja hii inakadiriwa kuwa kati ya dola milioni 130-200. Tukichukulia fedha za mradi wa wakati wa Nyerere za dola milioni 28.6 na kuzileta kwenye fedha za leo ni sawasawa na dola milioni 107.7 Hivyo ni wazi kuwa kiasi hicho cha fedha kinachopendekezwa leo hii si kibaya sana ukizingatia ukubwa na teknolojia ambayo itatumika.

Mojawapo ya tafiti nyingine za Benki ya Dunia za miaka ya karibuni zaidi zilionesha kuwa daraja la Kigamboni lingegharimu karibu dola milioni 46 hivi (karibu sawa na kiasi kilichokombwa na Kagoda Agriculture katika kashfa ya EPA!) Lilichelewa kwa sababu ya umaskini au kukosekana uwezo?

Naomba nipendekeze kwa wasomaji wangu kuwa kuchelewa kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni hakukutokana na ukosefu wa fedha au uwezo wa kitaalamu hasa katika miaka hii kumi na tano hivi. Wakati mradi huu umebuniwa miaka ya sabini nchi ilikuwa katika hali ngumu ya kiuchumi. Hata hivyo, baada ya mafanikio ya kampeni ya kusamehewa madeni yasiyolipika ambayo pia iliongozwa na Mwalimu Nyerere kabla ya kifo chake mwaka 1999 Tanzania ilikuwa katika nafasi ya kutumia neema hiyo kujenga miundombinu yake.

Kwa baadhi yetu tulitegemea kuwa mradi wa Kigamboni na ule wa Stielgers ingekuwa ni miradi mikubwa ya kwanza kufanyika. Wa Kigamboni ungeweza kutekelezwa mapema zaidi kwa sababu hauna gharama kubwa zaidi na ni rahisi zaidi kutekelezeka. Lakini haikuwa hivyo. Kilichotokea ni kuwa ni miaka hii kumi iliyopita tumeshuhudia ufisadi wa hali ya juu katika taasisi mbalimbali za serikali huku miradi ambayo ilikadiriwa kidogo ikila mabilioni ya fedha na watumishi wa umma wakiendelea kunufaika kwa migongo ya maskini wa taifa letu.

Ndani ya miaka hii kumi (ya 2000 hadi 2010) Tanzania imepoteza kwa njia ya ufisadi zaidi ya dola bilioni 10 (zaidi ya shilingi trilioni 11) huku Rais Kikwete akitudokeza kuwa karibu asilimia 30 ya fedha za bajeti ya taifa huishia mikononi mwa mafisadi.

Ndugu zangu, kuchelewa kwa ujenzi wa miradi hii mikubwa ambayo ingeweza kubadilisha maisha ya watu wetu ni matokeo ya moja kwa moja ya ufisadi uliokubuhu. Kiasi kilichopotezwa kwa ufisadi katika sekta mbalimbali kingeweza kujenga daraja la Kigamboni, Stielger's na miradi mingine mikubwa bila kuwaomba NSSF au taasisi binafsi!

Leo Magufuli anataka tushangilie kuwa NSSF wamefanya kazi nzuri ya kutoa fedha za wanachama wao kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati serikali yake imekuwa dhaifu kukabiliana na ufisadi mkubwa na kuwaacha mafisadi waendelee kupeta?

NSSF na kuficha madhara ya ufisadi

Hili sitaki kuliandika sana kwa sababu watu wanaofuatilia wanaweza kuona mtindo mmoja ukijitokeza miaka ya karibuni. Pale ambapo serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza na kusimamia fedha za umma kutekeleza miradi mbalimbali inakimbilia fedha za wanachama wa mashirika ya hifadhi ya jamii. Tumeliona hili kwenye kashfa ya Kiwira ambapo serikali iliruhusu ufisadi wa hali ya juu ya mmoja wa waliowahi kuwa viongozi wake lakini badala yake NSSF ikataka iwekeze bilioni 400 za fedha za wanachama; tumeona pia kwenye barabara ambazo Waziri Magufuli na serikali yake wamepata shida kuzisimamia na fedha za walipa kodi wakikaribisha NSSF kuingia na kuwekeza huko; tumeshuhudia hili kwenye ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma vile vile ambapo NSSF na PPF wamewekeza fedha za wanachama wao katika miradi hiyo.

Leo hii NSSF inakaribishwa tena kwenye daraja la Kigamboni na iko tayari kubeba gharama ya karibu asilimia 60 ya ujenzi na baadaye uendeshaji wa daraja hilo kurudisha fedha zake.

Sasa kinadharia hili halina tatizo hata kidogo. Pote duniani mashirika mbalimbali ya umma na hata ya hifadhi ya jamii yamewekeza kwenye miundo mbinu. Lakini kuna tofauti moja inapokuja Tanzania. Wanasiasa wanapoingiliana sana na watendaji wa taasisi hizi maamuzi ya baadhi ya taasisi hizi yanakuwa ni ya kisiasa zaidi. NSSF imekuwa ni shirika ambalo liko karibu zaidi na wanasiasa wa CCM kiasi kwamba nikiliita kuwa ni shirika la uwekezaji la CCM sitakuwa nawaita jina baya. Liko kwa ajili ya kuficha udhaifu wa uongozi, maono na usimamizi wa fedha za umma wa serikali ya CCM.

Popote pale penye mradi mkubwa ambao Serikali imeshindwa kuutekeleza kwa sababu "haina fedha" a.k.a fedha zimeliwa na mafisadi – NSSF itajitokeza kwa moyo mkunjufu kugawa fedha za wanachama kwenye miradi hiyo!

Wakati umefika kwa wanachama wa NSSF na mashirika mengine ya umma ambayo yanaingiza fedha kwenye miradi mikubwa ya serikali kuanza kudai mafao kutoka miradi hiyo. Hivi, mwana NSSF, PPF, au shirika jingine la hifadhi ya jamii anapata faida gani ya kifedha kwa shirika lake kuwekeza kwenye miradi mkubwa hii? Katika makampuni ya kawaida ya kibiashara kampuni inapowekeza kwenye miradi na kupata faida inagawa baadhi ya faida hizo moja kwa moja kwa wanahisa wake.

Je, mashirika yetu haya yanavyowekeza fedha hizi zote yanawagawia kiasi gani cha "faida" wanachama ambao fedha zao zinaingizwa huko? Mtu anayepata mafao ya shilingi elfu themanini kwa mwezi baada ya kustaafu anafaidika vipi na shirika kuwekeza mabilioni kwenye mafuta, barabara na madaraja au kuzalisha umeme? Je, wanachama wanaweza kudai kuwa asilimia kama 10 hivi kila mwaka ya faida yote ambayo NSSF inapata katika uwekezaji irudishwe kama "gawio" kwa wanachama wake? Au faida wataambiwa ni kuwa "na wao watatumia madaraja na barabara hizo"!

Nimeshawahi kusema huko nyuma kuwa mashirika ya umma kama NSSF ambayo yanawekeza mabilioni ya fedha za wanachama kwenye miradi hii mikubwa ambayo ni rahisi kuyumbushiwa na hali mbaya ya uchumi au matatizo mengine (fikiria daraja jipya likijengwa halafu likabomolewa na tsunami au tetemeko la ardhi!) yanahitaji kuwekewa utaratibu mkali sana wa uwekezaji. Hayapaswi kuachiliwa kuwekeza kana kwamba yao ni mashirika binafsi yenye lengo la faida tu!

Magufuli bila kupiga vita ufisadi anatuaminisha uongo. Mojawapo na ninaweza kusema kwangu ni tatizo kubwa la Magufuli ni kuwa haamini kabisa kuwa ufisadi ndilo tatizo kubwa kabisa linalokabili taifa sasa hivi na kuwa mambo mengi anayoyapigia kelele (kutofuatwa sheria kwa mfano) ni zao la ufisadi huo.

Magufuli anaamini kabisa kuwa serikali yake ni safi, uongozi wake ni bora zaidi na kuwa chama chake ni safi kabisa! Amefumba macho kabisa kama mbuni hasikii wala haambiwi kuhusu ufisadi.

Matokeo yake ni kuwa anajikuta anarudia vitu vile vile. Mara afute mkandarasi, mara aagize Kajima warudie barabara, mara apigie kelele watu wabomolewe nyumba.

Anafikiri – kwa makosa – watu hawajui sheria. Bila kupambana na ufisadi na mazao ya ufisadi haijalishi ni mradi gani ataupigia debe kwa kutumia takwimu zote alizonazo na hata maneno ya vijembe vya kisiasa hawezi kabisa kusimama kama kiongozi kati ya wananchi.

Watanzania wanahitaji kiongozi ambaye anafahamu na anapambana na ufisadi. Bahati mbaya sana yeye mwenyewe ni mmoja watu wambao walihusishwa na ufisadi mkubwa wa uuzaji wa nyumba za serikali miaka kadhaa iliyopita. Hadi leo hajaomba radhi taifa kwa kuruhusu jambo hilo ambalo lilisababisha gharama kubwa kwa serikali kwani pale ambapo ilikuwa rahisi kwa kiongozi kuhamia kwenye mji na kukuta nyumba ya serikali palipogeuka kuwa serikali ianze kuhudumia watumishi wake kwenye mahoteli!

Ninaogopa uongozi huu wa aina ya Magufuli. Sihoji dhamira yake hata kidogo ya kupenda au kutaka mabadiliko au kuona jiji la Dar "watu wanaishi kwa starehe". Ninahoji kama anachosema kinawezekana bila kuwa shujaa wa kupambana na ufisadi.

Hadi leo hatujamsikia yuko upande gani kwenye kashfa za EPA, Meremeta, Kagoda, Mwananchi Gold, Richmond na Dowans! Sijui yuko upande gani kwenye kashfa ya ununuzi wa ndege ya Airbus 320 ambao wengine tuliipigia kelele miaka minne iliyopita. Magufuli yuko salama kwenye kiti chake cha enzi akiwa waziri lakini anapenda usalama tu wa ofisi yake. Hapendi kuudhi watu kwa kuchukua msimamo wa uthubutu. Binafsi sijali sana kama anasimamia barabara, daraja au jengo fulani kwani hayo yote yanaweza kufanywa hata na mafisadi na ukweli kuwa baadhi ya mafisadi waliokubuhu nchi hii ndio wasimamizi wenyewe wa miradi!

Binafsi nasubiri kwa hamu kumuona akichukua upande wa kupinga ufisadi katika serikali yake na siyo tu katika wizara yake. Nasubiri kumsikia akizungumzia ufisadi kama tishio la wazi la maisha na hali za wananchi wetu. Jiji la Dar-es-Salaam liko kama lilivyo si kwa sababu watu hawataki kufanya kazi bali kwa sababu hizo ajira zenyewe nyingi zimefungamana na ufisadi. Mtu asiyepiga magoti na kutoa sadaka kwenye madhabahu ya ufisadi habarikiwi!

Mtu akitaka kufanikiwa ni lazima aende kufanya hija kwa fisadi kiongozi au kuwadi wa ufisadi ili mambo yake yaende vizuri! Magufuli hatambui hilo anataka tuamini kuwa tatizo ni wananchi!

Nilikua ninaamini kuwa anaweza kuwa kiongozi mzuri lakini nimegundua kuwa bila ya madaraka Magufuli ni sifuli. Hana la kufanya, hana la kushawishi, na hawezi kusimamia kitu bila kuwa na madaraka. Ila anataka kuogopwa si kwa sababu anaweza kushawishi bali kwa sababu ana uwezo wa madaraka kufanya anayofanya. Binafsi nampa changamoto kuwa atoke kwenye kiti chake cha starehe na kusimama kupambana na ufisadi ambao Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliita ni "adui mkubwa wa nchi wakati wa amani kuliko vita!"

Kiongozi asiyetembua ukweli huo na asiyesimama kusimama na adui huyo mkubwa wa uhuru na utu wa Mtanzania haijalishi anatembea kwa miondoko gani au anafanya nini cha kusifiwa ni wa kuangaliwa kwa kuogopa. Mara zote uongozi ni uwezo wa kushawishi na siyo uwezo wa kutishia watu. Ni madikteta tu ambao wanaweza kuleta "maendeleo" kwa kulazimisha siyo kwa kushawishi. Matokeo yake ni kuwa "maendeleo" hayo ni ya picha!

Tanzania kuwa kama Nigeria

Tukikubali hili la kutukuza vitu na siyo utu na kuweka mkazo katika kupendezesha majengo badala ya utu wa mtu tunakubali kufuata njia ya Nigeria au nchi nyingine ambazo zina ‘vitu vizuri' lakini hazina utu. Jamani Nigeria ina mabarabara na madaraja ya kila aina. Daraja refu zaidi katika Bara la Afrika ni lile la Third Mainland Bridge ambalo lina urefu wa kilomita 11.8. Nigeria inayo mabarabara ya juu kwa juu (flyovers) na kwa hakika ina barabara nyingi tu za kisasa kulinganisha na Tanzania.

Lakini, Nigeria imejua amani na utulivu? Je Nigeria wana umoja zaidi?Je, Nigeria ufisadi umedhibitiwa? Je, Nigeria ingeweza kutulia na kushinda ufisadi leo hii ingekuwa wapi?

Ninachokiona ndicho ambacho Tanzania inakitaka na ndio maana maneno yaliyoniudhi ya Bw. Magufuli ni hayo ya kuonekana kutaka kujenga majengo ya kisasa ili watu waje kuyaona! Hatuhitaji daraja la kisasa ili watu waje kulishuhudia! Vinginevyo, tutajenga madaraja, tutajenga mabarabara na mabarabara ya juu kwa juu lakini watu wetu wataendelea kuwa maskini, utu wao ukidhalilika na wao wakiwa watumwa wa matajiri wachache ambao watapita kwenye mabarabara hayo huko mamilioni ya Watanzania wakijivunia picha za kwenye post cards - si mnakumbuka watu hupiga picha kwenye lile daraja la wenda kwa miguu la Manzese?

Ndugu zangu, tusikubali kuwa kama Nigeria. Tusikubali kujenga vitu kwa ajili ya sisi nasi kusema "tunavyo". Kabla hatujajenga hayo mabaraba ya kwenda mbinguni (nina uhakika wapo watakaoenda mbinguni kupitia barabara hizo) tuboreshe kwanza na kwa kiwango cha juu hivi vidogo vilivyotushinda hadi sasa.

Jamani, kama NSSF wanazo fedha hizo bwelele kwanini wasijenge mitaro ya maji machafu na maji ya mvua ili watu wa Dar waishi kwa heshima na siyo kutegemea huruma ya wingi wa mvua? Kama serikali ina mipango ya kuboresha jiji la Dar kweli kwanini tumeshindwa kujenga barabara nzuri za kawaida kwenye maeneo ya watu, kuwahakikishia umeme na maji safi huku viwanja na bustani za mapumziko zikiwepo karibu kila kwenye halmashauri!?

Ndugu zangu, tunaweza kushangilia hotuba, tunaweza kushangilia picha (nina uhakika kuna watu walikuwa wanasisimka wakiangalia picha za hilo ‘daraja'). Lakini ukweli tunapaswa kufunguliwa na kutaka kushangilia tunapoona maisha yetu yanaboreshwa zaidi na utu wetu unainuliwa zaidi.

Kama watu hawana mahali bora pa kuishi, kula au mavazi barabara za mbinguni zitawasaidia nini? Daraja la Kigamboni haliwahusu maskini wanaoishi Kigamboni linahusu matajiri wanaoishi Kigamboni! Kwa sababu maskini bado watalipa fedha kutumia daladala kuvuka; matajiri wataweza tu sasa kwenda kwa raha zao kwenye viwanja vyao na nyumba zao huko!

Siamini mpaka nione

Binafsi naomba mniruhusu niwe Tomaso! Siamini mpaka nione. Siamini kama gharama itakuwa ni hiyo bilioni kama 200 hivi hasa nikikumbuka mradi mwingine wa hii serikali waujenzi wa maghorofa pacha ya Benki Kuu.

Binafsi siamini kuwa hata daraja likijengwa litadumu kwani kama mfano wa ujenzi wa miundo mbinu mingi ukiangaliwa tunajua ni nini kinatokea mara wakishamaliza kukata utepe na kutoa hotuba za kupongezana.

Uharibifu huanza. Jamani, si tumeona kwenye daraja la Mkapa? Hili daraja likikamilika na baada ya kula fedha nyingi tusije kuja kuambiwa kuwa "daraja linafungwa kwa matengenezo makubwa". Si tumeona kwenye barabara hizi hizi za Magufuli! Nitatoa pongezi zangu za kwanza inshallah ujenzi wadaraja utakapoanza! Hatushangilii picha, hatupongezi maneno au kutukuza takwimu! Tunapongeza ubora ndugu zangu, tunapongeza ubora! Magufuli hajanishawishi hadi hivi sasa ni sifuli.

Chanzo: Mtanzania Daima: Magufuli na daraja la Kigamboni, tushangilie?
 
Back
Top Bottom