Uchaguzi 2020 Kwa mambo haya 10, mimi kama Mtumishi wa Umma (mwalimu), John Pombe Magufuli sikupi kura yangu asilani

Jihu hoja zake wacha ujinga unamshambulia yy badala kuzishambulia hoja
 
Hongera Mwalimu unayejitambua , Meko apumzishwe tu kwenye sanduku la kura aende kwao chato akalime.
 
Nyongeza,sector binafusi imefilisiwa,kupunguzwa kazi kila kona,wakulima kutolipwa mda muhafaka,wafugaji kunyanganywa mifugo,wavuvi mateso hayapimiki.Kilio kilio kila kona ya nchi hii.
 
Ni wakati mzuri ajabu kuitoa ccm madarakani.
 
Jibu hoja zote basi, maana zingine hata sisi mama ntilie tunaziona japo sio walimu
 
mshahara ghafi kwenye ngazi ya TGTS D ndo kiasi gani?
 
Ila walimu naombea awamu hii mbanwe maradufu maana hamjielewi kabisa
 
Ccm mbele kwa mbele
 
*HAWA NDO CHADEMA WANAOTAKA KUCHUKUA NCHI*

Ni hivi, tangu wameingia madarakani, Chadema wamekuwa wakipokea ruzuku ya Shilingi Milioni 336,000,000/= kwa mwezi. Kwa mwaka (336,000,000/= x 12) = 4,032,000,000/=. Kwa miaka mikano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya Shilingi *20,160,000,000/= (Bilioni Ishirini na Milioni Mia Moja na Sitini).*

Chadema walikuwa na jumla ya wabunge 70, kati ya hawa 34 wa kuchaguliwa, na 36 wa Viti Maalum. Kila mbunge wa kuchaguliwa alikuwa anachangishwa Shilingi Milioni Moja 520,000/= kwa mwezi na kila mbunge wa Viti Maalum alikuwa anachangishwa Shilingi Laki Tano (1,500,000/=) kwa mwezi.

Hivyo, idadi ya michango ya wabunge wa kuchaguliwa kwa mwezi ilikuwa (520,000/= x 34) = 17,680,000/=; na idadi ya michango ya wabunge wa Viti Maalum kwa mwezi ilikuwa (1,500,000/= x 36) = 54,000,000/=. Kwa ujumla wake, Chadema walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi 71,680,000/= kwa mwezi kutokana na michango ya wabunge. Kwa mwaka (71,680,000/= x 12 = 860,160,000/=. Kwa miaka mitano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya *Shilingi 4,300,800,000/= (Bilioni Nne Mia Tatu Milioni na Laki Nane)*

Twende sawa hapa

Ruzuku 20,160,000,000/=
Michango ya wabunge 4, 300,800,000/=

Jumla 24,460,800,000/= *(Bilioni Ishirini na Nne Milioni Mia Nne na Sitini na Laki Nane)*

Licha yah hii;
· Chadema wanakusanya fedha kutoka kwenye ada za wanachama kila mwaka,
· Chadema wamefanya harambee ya nchi nzima mara kadhaa, nakumbuka ipo iliyofanyika Dar es Salaam (Serena hotel) na Arusha (hotel ya Mrema nimeisahau jina), na Mwanza kwa kuwataka Watanzania kuwachangia electronically. Hata mara moja hawajawahi kutoa ‘feedback’ kwa Watanzania hawa waliochanga. Kama wanabisha na ni wawazi kama wanavyojinasibu, watoe taarifa kwa kila tukio.

Hapo hatujaweka michango ya wanachama nchi nzima kila mwaka, Hivyo haya ni sehemu ya makusanyo yao ya miaka 5 tu kama Chama ambacho kimekuwa Chama kikuu cha upinzani nchini kwa miaka takribani 20, bado hii leo:

i. Hakina ofisi yao kama jengo, pamoja na kununua eneo miaka ya nyuma ili kuweka jengo la ghorofa 11kwa minajili ya kujenga ofisi yenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani na kupangisha maeneo mengine. Ni kama Milioni 150 zilizotumika kununua eleo zilitupwa tu. Ofisi hii ya Chama inayotumika leo ilinunuliwa na Bob Makani. Kina Mbowe na Lissu wanaojinasibu kuwaletea Maendeleo Watanzania hawajawahi kufanya lolote pamoja na kujikusanyia mabilioni ya pesa kila mwaka.
ii. Makatibu wake wa wilaya wengi (kama sio wote) nchi nzima hawalipwi mishahara wala posho,
iii. Leo hii kampeni zinaendelea Chama hakina pesa za kuendesha kampeni, badala yake wanapitisha kofia kuwachangisha wananchi katika mikutano ya kampeni.

Hii pesa yote iko wapi? Kama imewekezwa, imewekezwa wapi? Mbona wabunge wao wanalalamika wakihoji haya wanaambiwa hakuna kuhoji?

Haya matumizi mabaya yote ya pesa yanafanyika wakati Tundu Lissu (eti mpenda haki huyu, na mtetezi dhidi ya ukandamizaji, na mwanademokrasia) akiwa ‘amebandikwa’ nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama, na Makamu Mwenyekiti wa Chama. Wanachama wanalalamikia haya yote, mwanasheria anateyakiwa kuwatetea, Bwana Tundu Lissu ametulia tulii kama vile hakuna kilichotokea yaani! Eti leo anaimba uhuru, haki na maendeleo wakati Chadema yake hakuna Uhuru, Chadema yake hakuna Haki, Chadema yake hakuna Maendeleo!, nay eye ni Kiongozi mwandamizi wa Chadema.

Ni huyuhuyu Tundu Lissu na Chadema wake wanataka Watanzania wawape ridhaa ya kusimamia utajiri wote wa nchi, waratibu matumizi ya matrilioni ya kodi zote zinazokusanywa nchini, wasimamie miradi yote ili eti walete ustawi kwa Watanzania.

Ni huyu huyu Tundu Lissu na Mbowe ambao ni viongozi wakuu wa Chadema miaka nenda rudi bado wanapanga makao makuu ya chama taifa kwenye nyumba ya mtu (mtaa wa Ufipa-Kinondoni), ndo wanasema eti watawasomesha bure Watanzania, eti watawatibu bure Watanzania wote.


Sasa ona hii, Lissu anajiita eti ni mwanasheria anayesimamia katiba na sharia. Hivi hiyo nafasi ya Mwanasheria wa Chama aliyonayo ndani ya Chadema iko kikatiba? Atoke huko atuonyeshe kwenye katiba kama kuna nafasi ya mwanasheria wa Chama kikatiba. Huyu huyu ameshindwa kusimamia haki ndani ya Chama, ameshindwa kutetea uhuru wa wanaokandamizwa ndani ya chama kiasi cha anayehoji tu anafukuzwa uanachama, ameshindwa kusimamia na kuheshimu katiba ya chama; eti leo hii anataka kusimamia haya akiwa Rais wa Tanzania?

Wahenga walisema “sumu haijaribiwi kwa kuionja”, Chadema hii ya Lissu na Mbowe ni sumu kwa Watanzania.
 
Mkuu uko sahihi 100%
 
Wapo walimu kibao watampigia wanaipenda CCM na JPM wewe kura yako moja haitabadili kitu!
Huna akili, watampigia kwa lipi? Au unadhani wanaugonjwa wa kupenda Kama wewe?
 
Unazungumzia kazi ipi? Hii ambayo mtu anapata 100k kwa mwezi? Halafu kaacha kadi yake ya benki huko Faidika?
Mmh mwalimu anapata 100k? Sasa si heri anaweza kuacha hata kadi, asipokuwa na hiyo card ataacha nini?
 
Namba 6 ujue kajiona ye jiniaz sana kahamisha magoli kwa sababu ya uchaguzi.Katuona sisi watoto yaani
 
Na mimi nimekumbuka watumishi walivyokuwa wamegeuza ofisi za umma kama mali yao, kwa Magu thubutu tena uone kazi! Halipo tena Magu mitano tena tunampa

2. Walimu waliokuwa wanafundisha kijijini walipofuata mishahara walioamua kulewa takribani wiki mbili bila kurud shuleni wakisingizia foleni mishahara kuchelewa wanafunzi wetu walibaki wakifundishana wenyewe hilo kwa Magu limekomeshwa,wananchi watoto wetu hamzururi ovyo lazima tunamchagua

3. Walimu walitumia michango ya shule ,kuwaambia wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza kwenda na limu,majembe, fyekeo nk. Kisha vyote waliviuza kwa wafanyabiashara baadaye kwa manufaa yao ,leo hayo mambo Magu kayamaliza lazima mchukie lakini kwetu wananchi tunamchagua tena

4. Watumishi walitumia lugha za matusi tulipotaka watuhudumie leo watumishi wanatuheshimu kwa sababu Magu hataki watumishi wasiowajibika kwa wananchi lazima mchukie lakini kwetu wananchi tunamchagua katujali sana

5. Nakumbuka mawaziri ,makatibu wakuu ,wakurugenzi na wakuu wa idara na walivyoshirikiana kutupiga kwenye miradi mbalimbali na kuanzisha semina zilizofanyikia kwenye majengo yao morogoro,Arusha,Mwanza leo hayo hayapo kweli lazima mchachamae lakini tunaowajua leo tunafaidi wote kodi zetu watanzania usifikiri hawaoni watamoatia kura za kishindo magufuri hadi mchanganyikiwe!!!

Ebu ongezea mengine kama unakumbuka vituko vya watumishi
 
Kila kundi lina hoja zake,wafanyabiashara, vijana wasio na ajira ,huduma duni za afya bora hata JK walitoa tip dawa zikapatikana sasa ni orodha kuanzia gloves,nyuzi,drip nk mbali ya bima za kawaida,Lissu tuokoe.
Ubabe wa Magufuli una lengo la kukanyaga kila mmoja anayepinga, hata kama dai lako ni sahihi likikinzana na matakwa yake hugeuka na kuwa kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…