Kwa maneno ya Rais Samia nyaraka zilizovuja mtandaoni kuhusu tuhuma za Ufisadi ni za kweli

Unstaka JWTZ wachukue hatua gani?
 
Mbona kina Nyerere mwenyewe hakutaka kujilimbikizia mali na perhaps hakuna kijukuu Wala kitukuu kitakacho kuja kuwa Raisi wa TANZANIA
Nadhani kati ya maraisi wa Tanzania amabao hakupenda kujilimbikizia Mali ni Nyerere japo sianuhakika kwa 100%.

Hawa wengine walijilimbikizia kimtindo japokuwa kwa viwango tofauti tofauti.

Hata mkinichagua mimi kuwa raisi wenu lazima nijilimbikizie kimtindo😎.
 
Hata mimi nadhani ndiko tunakoelekea. Samia amepoteza senses zote za kibinadamu na hajali tena chochote. Halafu wanatukejeli wananchi. Makonda kaposti kejeli ya kuwa eti ''hakuzaliwa kuja kuwa maskini''
Uzuri ni kwamba, MUDA ni mwamuzi asiye na upendeleo
 
Hivi hapa Mwanza tuna mtu kweli anayeamini eti JWTZ wachukue hatua kulinda Katiba? Kweli huyu mtu anajua hata anachoandika? I wish kama kweli uko Mwanza basi unaishi Gamboshi!
 
Kuiondoa Serikali hii ya kidhalimu madarakani na kusimamia mchakato wa kisimikwa kwa Katiba Mpya iliyojitosheleza na Mfumo mpya wa Uchaguzi. Then kurudisha Serikali ya kiraia.
Hakuna sehemu hata moja Africa ambako jeshi limefanikiwa kufanya hivyo.

Kila sehemu jeshi lilipochukua madaraka kwa minajili ya kuondoa uongozi mbovu liliharibu zaidi.

Angalia Zaire ya Mobutu.

Angalia Nigeria tangu Johnson Aruiyi-Ironsi.

Angalia Liberia tangu Samuel Doe.

Hata pale tawala za kijeshi ziliposifiwa, muziki ni ule ule.

Angalia Misri na Gamal Abdel Nasser. Matatizo ya uongozi wa kijeshi yanaiandama mpaka leo.

Angalia Burkina Faso na Thomas Sankara. Matatizo ya uongozi wa kijeshi yanaiandama mpaka leo.

Tatizo letu Waafrika wengi, tunapenda majibu ya mkato, utatuzi rahisi kwa maswali magumu.

Badala ya ku focus kuwa na jamii inayojitambua, tunataka viongozi fulani watufanyie kazi ya kujitambua kwa ajili yetu.

Ndiyo maana wengi tunapenda uongozi wa kijeshi. Uongozi ambao mtu anayejitambua hatakiwi kuushabikia.

Najua uongozi wetu mbovu unatushawishi tupende njia ya mkato ya kupata uongozi wa kijeshi. Lakini uongozi wa kijeshi hauna guarantee ya kuwa mzuri. Worse still, historia inatuonesha uongozi wa kijeshi umeiharibu sana Africa.

Kuanzia mapinduzi ya kwanza ya kijeshi yaliyomuondoa Sylvanus Olympio Togo January 13 1963.

Sasa, kwa rekodi hiyo, kwa nini mtu yeyote mwenye akili atake uongozi wa kijeshi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…