Ni kwa mara nyingine Trump anaukataa mshahara wa Urais, dola 400,000 kwa mwaka (shilingi bilioni 1 na milioni 40) ili usaidie wenye uhitaji na shughuli za kimaendeleo.
Kama ilivyokuwa katika muhula wake wa kwanza (2916 - 2020) mshahara wake utaendelea kusaidia wahitaji kwenye idara ya afya, marekebisho ya makumbusho ya kitaifa, kusaidia wanafunzi wa vyuo vya sayansi, kuwadaidia waathirika wa majanga ya asili na wastaafu wa jeshi la Marekani
kukataa mshahara wa urais ni hatua nadra katika historia ya Marekani, na Trump aliungana na viongozi wachache waliowahi kufanya hivyo, akiwemo Herbert Hoover na John F. Kennedy.
Wafuasi wa Trump wameona ni hatua ya kihistoria ya kujitolea kwa taifa, huku wakosoaji wakisisitiza kwamba lengo lake ni kutafuta kuungwa mkono na kuimarisha nafasi yake kisiasa.