Uchaguzi 2020 Kwa mara ya kwanza CCM wamefanya kampeni kinyonge na bila agenda za chama bali agenda za mtu mmoja

Uchaguzi 2020 Kwa mara ya kwanza CCM wamefanya kampeni kinyonge na bila agenda za chama bali agenda za mtu mmoja

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
CCM mwaka huu wameonyesha walilala zaidi ya wapinzani kipindi chote siasa zilipokatazwa. Awakujipanga kuanzia juu Hadi kwenye tawi na kibaya zaidi hata UCHAGUZI wa serikali ya mtaa awakufanya bali waliteuana na walioteuliwa awakuwa chaguo la wananchi hivyo walijitengenezea kukataliwa toka ngazi ya shina. Waliokuwa wanakubalika walitemwa wakapewa wanaofahamiana na wakubwa.

Ni kipindi ambacho badala chama kifanye kampeni kimekwama na mgombea ameingia kuzindua mirafi ambayo baadhi ilishazinduliwa au haina haja yakuzindua.

Ni kipindi pekee ambacho wenye chama wamekaa pembeni wanaleo na kula bata wakati waliokabidhiwa chama wakitapatapa kukusanya watu wakushiriki mikutano.

Nikipindi ambacho nguo za chama zimegawiwa kwa wanafunzi na watoto na wakimaliza zinakusanywa na kupelekwa sehemu nyingine yote hii nikubana matumizi bila kuangalia afya za vaaji.

Ni kipindi ambacho chama kinafika kwenye UCHAGUZI kikiwa hakina mawakala wakueleweka.

Nikipindi ambacho kimegubikwa na watumishi wa Umma kujiandalia safari za uchaguzi huku wakibadilishana mikoa kwa lengo lakupata fedha zakuanzia maisha awamu ya sita.

Nikipindi ambacho walimu awaaminiki Tena Bali vijana wa lumumba. Inshort nikipindi kigumu kwa chama kinachotokana na chama kuruhusu watu kuhodhi chama.
 
CCM ilikuwa ya Mzee Kinana, busara tele.

Sio hii ya Pole pole anayejivunia ma VX kama sera ya kuwavutia wapiga kura

Sio hii ya Bashiru aliyeishiwa nguvu kiasi anatangaza wazi kuwa ccm itatumia dola kushinda. Bashiru anayelia wana ccm kuisaliti

Mzee Mangula ameamua kujikalia kimya!!
 
Ccm imemdharau mpinzani kutoka ubeligiji

Ndio maana hawatumii nguvu kubwa

Msaliti wa Nchi hana madhara kwa Ccm
 
Kila siku tunawaambia chama lishajifia siku nyingi mno mnabisha...Mwenyekiti wao kutumia dola kuminya wapinzani 5 years bila aibu sasa ime m-backfire...
Huwezi kujenga chama kwa kununua viongozi wa upinzani, madiwani na wabunge...hii siyo siasa huu ni ujambazi...

Sasa kwa mara ya kwanza CCM wanashuhudia matunda ya kazi yao.

Mambo ni magumu watanzania wamewagomea!!
 
Waache waendelee na kiherehere wakati msaliti wa Nchi Lissu ameshakata tikiti ya kurudi kwao ubeligiji

Wataachwa wanateseka wodini
"Maalim Seif akutana na walioshambuliwa kwa Mabomu"

 
Waache waendelee na kiherehere wakati msaliti wa Nchi Lissu ameshakata tikiti ya kurudi kwao ubeligiji

Wataachwa wanateseka wodini
Sheikh Ponda Issa Ponda amemuumbua John Pombe kwa kusema Raisi hapaswi kuwa Muongo kwani Allah huchukizwa na Mtu muongo
 
Back
Top Bottom