Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu niliijaribu kuomba kazi, na kufanya interview

Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu niliijaribu kuomba kazi, na kufanya interview

Kwa mara yakwanza siku ya ijumatatu niliomba kazi. Kuna rafiki yangu alinifowardia message WhatsApp, kuwa kunamahala wanatafuta Mechanical engineer, wakufanya kazi za maintenance katika machines kiwandani. Pamoja nakufanya installation za baadhi ya machines. Basi nikatuma cv, siku hiohio usiku, kesho yake jumanne wakanitumia email kuwa nijiandae na interview siku ya jumamosi kwa njia ya Skype. Sikuijibu ile email, Jumatano wakanipigia kuniuliza kama niliona email ,nikawajibu sijaangalia email,nikasemaa ngoja niangalie.

Nikaangalia nikakuta kweli email yao inayonipa maelekezo namna interview itavyokuwa nikwajibu ndio nimeiona hakuna shida. Jmosi saa nne na nusu asubuhi ( jana) wakanitext Skype nikawajibu, wakaomba wanipigie kwa ajili ya interview nikawambia ok. Wakapiga alikuwa madam wakizungu na muhindi mmoja mshikaji tu.

Wakaniuliza masuali yote nikajibu, interview ilichukua saa moja na dk 47, tukarbagain mshahara wakasema wanipe laki 9 take home. Lkn kazi nimkoani. Wakaniambia basi week hii inaanza kesho nijiandae ,halafu Ile week nyingine niende. Sasa nimekaa nimetafakari nimeona siwezi kwenda kulingana nashughuri zangu binafsi nazofanya. Kwahio kama kuna mtu anauzoefu na.

Callibration of mass, pressure, temperature and underground tanks. Pia awe nacheti cha EIT au OSHA kinachohusu mambo ya safety.

Ana uwezo wakudesign kutumia
Solidworks, AutoCAD, ANSY, CATIA.
Anaweza kutumia microsoft word, power point, Excel ,na unauwezo wakufanya maintenance kwenye steam boiler, feeding machines, pamoja na printing machines ,napia yuko registered na ERB kama GE au PE. Basi ani Dm cv yake nimpe jamaa alieniambia niombe pale halafu atajua namna yakufanya maana mimi sintoenda.

Cv itayokidhi vigezo ndio ntakayoituma.

.........
Naona wadau kwenye comments wamemeza nyembe, naomba atakaekuja pm awe navigezo ntamp email ya wahusika atume moja kwa moja .
Mkuu hongera sana kwa ku turndown hiyo offer ,huo mshahara mdogo sana kwa engineer mwenye uzoefu angalau wangekupa hata 2.5-3m nina uhakika ungeenda. Guys don't burgain to cheap hawa watu ukiajiriwa wanakutumia ipasavyo. Usiombe a survival salary kama una experience ya 5years. All the best
 
Mkuu nikikuambia baada yakumaliza chuo ,nimekaa garage zaidi yamiezi 5 nikijifunza maintenance za magari(kwakulipia tena), nikaanda kujifunza maintenance za mashine bila kulipwa miezi 6, baada yahapo nikaanza issue za calibration miezi 7, nimesoma certificate za kucalibrate matank, weigh bridge,mizani,force ,mass, pressure, temperature. But all in all kwa Sasa naofisi yangu ambayo inadeal na issue baadhi nilizosotea baada yakumaliza chuo.
Nipo nje ya mada kidogo mtanisamehe!

Ila mkuu mimi nataka nikupongeze kwa hili pia wale waliosomea mambo haya wakipita hapa wachukue technique hii inasaidia sana.nitatoa kisa kimoja;hapo nyuma kidogo nikifanya biashara ya spare za magari za used sasa siku moja nikapata mteja mmoja ni mtu mzima kiasi nikamuuzia starter ya gari yake alikuja na kijana wake but nikamwambia lazima nimpe fundi wangu ninaemuamini akaifunge coz vitu vya used havipo guaranteed kinaweza kifanye kazi au kisifanye so ikitokea mazingira hayo mimi naweza nisiamini kutokana na kuna mafundi mitaani huvitia matatizo makusudi vitu ili wapewe hela na boss wakanunue wao wapate cha juu.

Yule mzee akaniambia kwa hilo usijali huyu mwanangu amehitimu chuo mechanical engineering upande wa magari so ataifunga mwenyewe we nipe no ya simu nitakufahamisha itavyokuwa,baada ya saa moja yule kijana ananipigia simu ananiuliza “hivi bro hii starter inakaa sehemu gani kwenye engine” nilishangaa sana maana mwanzo nilimuona ni mzoefu kumbe ni mzoefu kwenye picha za kwenye makaratasi tu so kama ingekuwa ndo ameulizwa hili swali kwenye interview nadhani kazi angeikosa ni vizuri mtu ukitoka chuo uingie mtaani kile ulichokisoma ukifanye kwa vitendo zaidi ili kuboresha mazingira mazuri ya kujieleza pale inapobidi kufanya hivyo.
 
Mkuu watu tunaofanya biashara tunapitia mambo magumu sana, kuna Muda unaweza tamani umpe biashara yako mtu mwingine asimamie ili wewe ukakomae sehemu nyingine ili maisha yaende. Lakini nimekaa nimetafakari sana, nimeona heri niendelee kukomaa mwenyewe nawatu wangu.
Sijui kama umeelewa ulichoulizwa kisha ukajibu kwa ufasaha.
 
Okay sawa,ila itakua ni busara zaidi kama utawajulisha wahusika kua wewe haupo tayari kwenda kuifanya hiyo kazi ili nao waangalie utaratibu wao mwingine,kupiga kimya tuu sidhani kama ni jambo jema,Dunia inazunguka,huwezi kujua pengine siku za mbele wewe unaweza kuja kuwahitajia zaidi kuliko wao wanvyokuhitajia kwasasa.
Una busara, hilo neno dunia inazunguka ni pana sana.
 
Mkuu nikikuambia baada yakumaliza chuo ,nimekaa garage zaidi yamiezi 5 nikijifunza maintenance za magari(kwakulipia tena), nikaanda kujifunza maintenance za mashine bila kulipwa miezi 6, baada yahapo nikaanza issue za calibration miezi 7, nimesoma certificate za kucalibrate matank, weigh bridge,mizani,force ,mass, pressure, temperature. But all in all kwa Sasa naofisi yangu ambayo inadeal na issue baadhi nilizosotea baada yakumaliza chuo.
Mkuu una ujuzi mkubwa sana na uwezo mkubwa ila kama ulichokiandika hapa kinaakisi mtazamo wako basi bado una safari ndefu sana ili kufikia full potential yako.Ile nafurahi kwamba umejfunza viru vingi sana na unavifanyia kazi ila naendelea kukusitiza uwajulishe kwamba you are not interested na uwashukuru kwa kukupa fursa
 
Education wamepanick.
Hatari mkuu, raia wanataka kunimeza. Kitukikubwa nilichojifunza
Sijui kama umeelewa ulichoulizwa kisha ukajibu kwa ufasaha.
Mkuu nimeelewa, rudia tena ukasome swali lamuulizaji na namna nilivyomjibu. Reason nikuwa biashara sasa hivi ningumu,kwahio kuna Muda unaweza tamani ukafanye shughuri zingine zakuingiza kipato, ili ziendelee kusapoti biashara yako, lkn mwishoni unaona mawazo yakwanza hayakuwa bora utafanyaje mkuu?. Utaenda tu kwasababu unaogopa kukasirisha watu?.
 
Mkuu una ujuzi mkubwa sana na uwezo mkubwa ila kama ulichokiandika hapa kinaakisi mtazamo wako basi bado una safari ndefu sana ili kufikia full potential yako.Ile nafurahi kwamba umejfunza viru vingi sana na unavifanyia kazi ila naendelea kukusitiza uwajulishe kwamba you are not interested na uwashukuru kwa kukupa fursa
Sawa mkuu. Thanks for your advice.
 
Mkuu unakumbuka issue za 2017?. Uko vizuri, kuna mmarekan mmoja kawa billionea baada yakuhitimu degree yake ya mechanical, akaanzisha kampuni nafikiri inaitwa herion, mtu aliemuispaya ni TESLA, Sasa mkuu nawewe be inspired nahuyo jamaa kwenye Avatar yako, uanzishe SPACE TZ.
Herion nimewaona jana wanataka kuipa upinzani Tesla. Jamaa anapata upinzani kabla hata hajakomaa kwenye biashara
 
Sasa
hadi anakupa,
Hadi unapangiwa siku ya interview Serikali kuu ya kichwa chako ilikuwa wapi..,

Pia umemfanya mwenzako aonekane si mwaminifu, next time ikitokea mtu ambaye seriously anahitaji kuunganishwa na kazi kama hivyo..hiyo nafasi hatopatiwa tena coz umeshamuangusha.
Hii issue iliwahi kunitokea. Kuna jamaa yangu aliacha shule form 2 nilikuwa namsaidia kimasomo. Miaka miwili badae akafanya interview nikamsaidia kuijibu, tukapoteza mawasiliano. Siku moja nimetoka six nikakutana naye mwendokasi akienda kazi ileile niliyomsaidia kujibu interview.

Aliniunganisha nikapige kibarua nikapata pesa ya maana ila nikakacha nije chuo. Sasa wakati naondoka nikamuita jamaa kapiga diploma aje kukaba nafasi yangu kila kitu kikaenda poa. Siku anatakiwa aje na laki ya kufanikisha kwa supervisor akanikimbia. Mtoto wa mama yule alikwamisha watu watatu niliokuwa nishawaandaa nyuma na issue ya kuleta vibarua kinyemela na commission nikakosa.
 
Hayo mambo ya calibration yanafundishwa na chuo gani mkuu?
Mkuu nikikuambia baada yakumaliza chuo ,nimekaa garage zaidi yamiezi 5 nikijifunza maintenance za magari(kwakulipia tena), nikaanda kujifunza maintenance za mashine bila kulipwa miezi 6, baada yahapo nikaanza issue za calibration miezi 7, nimesoma certificate za kucalibrate matank, weigh bridge,mizani,force ,mass, pressure, temperature. But all in all kwa Sasa naofisi yangu ambayo inadeal na issue baadhi nilizosotea baada yakumaliza chuo.
 
RUSTEM PASHA
Kwanza Big Up sana.
Binafsi mie ni Electrical Eng. Hayo mambo unayoyaongelea hapa watu hawawezi kuelewa hata kidogo.
Mwaka 2015 nilikuwa nimeajiriwa kampuni A. Nikapata kazi kampuni B yenye mshahara mkubwa zaidi ya A. Kabla sijaanza kazi kampuni B maana ilikuwa baada ya miezi miwili nikaitwa kampuni C kufanya interview na baada ya kufanya nikapata ila mshahara ulikuwa chini ya wa kampuni B ila zaidi ya wa kampuni A.
Ukiwa Eng fursa ni nyingi sana za kujiajiri au hata kuajiriwa.
 
bei ya kusoma hiyo certificate ni bei gani?na inachukua muda gani kuimaliza?
Nilisoma short course, kucalibrate tank nililipa laki 4 kwa week 2, mizani nililipa laki 2 kwa siku 5. Flow meter laki 4.
 
RUSTEM PASHA
Kwanza Big Up sana.
Binafsi mie ni Electrical Eng. Hayo mambo unayoyaongelea hapa watu hawawezi kuelewa hata kidogo.
Mwaka 2015 nilikuwa nimeajiriwa kampuni A. Nikapata kazi kampuni B yenye mshahara mkubwa zaidi ya A. Kabla sijaanza kazi kampuni B maana ilikuwa baada ya miezi miwili nikaitwa kampuni C kufanya interview na baada ya kufanya nikapata ila mshahara ulikuwa chini ya wa kampuni B ila zaidi ya wa kampuni A.
Ukiwa Eng fursa ni nyingi sana za kujiajiri au hata kuajiriwa.
Tuendelea kupambana, mfano hapa bongo hakuna kampuni inayocalibrate troxler, iwe government au private lkn kuna troxler kibao, watu wanatoka south Africa kuja kula hela bongo, kwa mambo ambayo hata sisi wabongo tunaweza kuyafanya.
 
Troxer ndio mashine gani mkuu?
Troxler nimachine fulani hivi inatumia radiatioactive material kama nuclear radiation, kupima density ya udongo. Barabara ikishashindiliwa kama inatengenezwa wanataka wapige lami, huwa kunakipindi wanapima density ya udongo ulioko barabarani, sasa machines inayotumika ndio inaitwa troxler.
 
hapo nimekuelewa nafikiri lengo ni kupima compaction ya barabara.
 
Back
Top Bottom