Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu niliijaribu kuomba kazi, na kufanya interview

Mkuu hongera sana kwa ku turndown hiyo offer ,huo mshahara mdogo sana kwa engineer mwenye uzoefu angalau wangekupa hata 2.5-3m nina uhakika ungeenda. Guys don't burgain to cheap hawa watu ukiajiriwa wanakutumia ipasavyo. Usiombe a survival salary kama una experience ya 5years. All the best
 
Nipo nje ya mada kidogo mtanisamehe!

Ila mkuu mimi nataka nikupongeze kwa hili pia wale waliosomea mambo haya wakipita hapa wachukue technique hii inasaidia sana.nitatoa kisa kimoja;hapo nyuma kidogo nikifanya biashara ya spare za magari za used sasa siku moja nikapata mteja mmoja ni mtu mzima kiasi nikamuuzia starter ya gari yake alikuja na kijana wake but nikamwambia lazima nimpe fundi wangu ninaemuamini akaifunge coz vitu vya used havipo guaranteed kinaweza kifanye kazi au kisifanye so ikitokea mazingira hayo mimi naweza nisiamini kutokana na kuna mafundi mitaani huvitia matatizo makusudi vitu ili wapewe hela na boss wakanunue wao wapate cha juu.

Yule mzee akaniambia kwa hilo usijali huyu mwanangu amehitimu chuo mechanical engineering upande wa magari so ataifunga mwenyewe we nipe no ya simu nitakufahamisha itavyokuwa,baada ya saa moja yule kijana ananipigia simu ananiuliza “hivi bro hii starter inakaa sehemu gani kwenye engine” nilishangaa sana maana mwanzo nilimuona ni mzoefu kumbe ni mzoefu kwenye picha za kwenye makaratasi tu so kama ingekuwa ndo ameulizwa hili swali kwenye interview nadhani kazi angeikosa ni vizuri mtu ukitoka chuo uingie mtaani kile ulichokisoma ukifanye kwa vitendo zaidi ili kuboresha mazingira mazuri ya kujieleza pale inapobidi kufanya hivyo.
 
Sijui kama umeelewa ulichoulizwa kisha ukajibu kwa ufasaha.
 
Una busara, hilo neno dunia inazunguka ni pana sana.
 
Mkuu una ujuzi mkubwa sana na uwezo mkubwa ila kama ulichokiandika hapa kinaakisi mtazamo wako basi bado una safari ndefu sana ili kufikia full potential yako.Ile nafurahi kwamba umejfunza viru vingi sana na unavifanyia kazi ila naendelea kukusitiza uwajulishe kwamba you are not interested na uwashukuru kwa kukupa fursa
 
Education wamepanick.
Hatari mkuu, raia wanataka kunimeza. Kitukikubwa nilichojifunza
Sijui kama umeelewa ulichoulizwa kisha ukajibu kwa ufasaha.
Mkuu nimeelewa, rudia tena ukasome swali lamuulizaji na namna nilivyomjibu. Reason nikuwa biashara sasa hivi ningumu,kwahio kuna Muda unaweza tamani ukafanye shughuri zingine zakuingiza kipato, ili ziendelee kusapoti biashara yako, lkn mwishoni unaona mawazo yakwanza hayakuwa bora utafanyaje mkuu?. Utaenda tu kwasababu unaogopa kukasirisha watu?.
 
Sawa mkuu. Thanks for your advice.
 
Herion nimewaona jana wanataka kuipa upinzani Tesla. Jamaa anapata upinzani kabla hata hajakomaa kwenye biashara
 
Hii issue iliwahi kunitokea. Kuna jamaa yangu aliacha shule form 2 nilikuwa namsaidia kimasomo. Miaka miwili badae akafanya interview nikamsaidia kuijibu, tukapoteza mawasiliano. Siku moja nimetoka six nikakutana naye mwendokasi akienda kazi ileile niliyomsaidia kujibu interview.

Aliniunganisha nikapige kibarua nikapata pesa ya maana ila nikakacha nije chuo. Sasa wakati naondoka nikamuita jamaa kapiga diploma aje kukaba nafasi yangu kila kitu kikaenda poa. Siku anatakiwa aje na laki ya kufanikisha kwa supervisor akanikimbia. Mtoto wa mama yule alikwamisha watu watatu niliokuwa nishawaandaa nyuma na issue ya kuleta vibarua kinyemela na commission nikakosa.
 
Hayo mambo ya calibration yanafundishwa na chuo gani mkuu?
 
RUSTEM PASHA
Kwanza Big Up sana.
Binafsi mie ni Electrical Eng. Hayo mambo unayoyaongelea hapa watu hawawezi kuelewa hata kidogo.
Mwaka 2015 nilikuwa nimeajiriwa kampuni A. Nikapata kazi kampuni B yenye mshahara mkubwa zaidi ya A. Kabla sijaanza kazi kampuni B maana ilikuwa baada ya miezi miwili nikaitwa kampuni C kufanya interview na baada ya kufanya nikapata ila mshahara ulikuwa chini ya wa kampuni B ila zaidi ya wa kampuni A.
Ukiwa Eng fursa ni nyingi sana za kujiajiri au hata kuajiriwa.
 
bei ya kusoma hiyo certificate ni bei gani?na inachukua muda gani kuimaliza?
Nilisoma short course, kucalibrate tank nililipa laki 4 kwa week 2, mizani nililipa laki 2 kwa siku 5. Flow meter laki 4.
 
Tuendelea kupambana, mfano hapa bongo hakuna kampuni inayocalibrate troxler, iwe government au private lkn kuna troxler kibao, watu wanatoka south Africa kuja kula hela bongo, kwa mambo ambayo hata sisi wabongo tunaweza kuyafanya.
 
Troxer ndio mashine gani mkuu?
Troxler nimachine fulani hivi inatumia radiatioactive material kama nuclear radiation, kupima density ya udongo. Barabara ikishashindiliwa kama inatengenezwa wanataka wapige lami, huwa kunakipindi wanapima density ya udongo ulioko barabarani, sasa machines inayotumika ndio inaitwa troxler.
 
hapo nimekuelewa nafikiri lengo ni kupima compaction ya barabara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…