Kwa mara ya kwanza nathubutu kugombea Ubunge

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ndio nilikua nimemaliza tu chuo kikuu, na nilikua na kiasi cha tsh laki5 tu, cash in hand, fedha ambazo nilikua nikijibana bana na kudunduliza nikiwa chuo kwa madhumuni haya haya ya kugombea ubunge. Nikajitosa katika mchakato wa ndani ya chama, kuomba ridhaa ya wanachama nipeperushe bendera ya chama kwenye uchuguzi mkuu....

Nakumbuka mtihani wa mwisho chuo, mwaka wa tatu semester ya mwisho ulikua tarehe za mwanzo za mwezi July mwaka huo wa uchaguzi, na fomu kura za maoni kwenye chama nilichokusudia kuomba ridhaa yake, zilianza kutolewa katikati ya mwezi huo huo July. Lakini pia na kampeni zilianza mwisho mwa mwezi huo huo July, mwaka ule wa uchaguzi...

Basi bana,
Dhamira na nia ya dhati kwenda kuomba ridhaa ya wanainchi iliuteka na kuutawala sana mutima wangu.

Matumaini ya kushinda uchaguzi huo yalinizidi kipimo. Vipaumbele vyangu, mipango na mikakati ya kuwakomboa wanainchi katika changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo pale jimboni, ilikua wazi sana, na ilinipa ujasiri sana nafsini mwangu. Na kwamba kivyovyote vile nitafaulu kupata ridhaa hiyo....

Nilikuwa nashauku, nguvu, ari, na moyo wa kipekee sana, kwenda kuwaongoza wanainchi.
Nilikua nikifanya maombi kama dose ya masaa, kila nilipopata wasaa, nilimuomba na kumshukuru Mungu anionyeshe njia...

Bas,
siku ikafika,
Baada ya tu kumaliza paper chuoni, nikaenda kuwaaga ndugu zangu pale mjini, na kuwaeleza safari yangu kuelekea mkoani kijijini.

Kesho yake asubuhi nikanyaka ndinga, huyo moja kwa moja mpaka kijijini, nilifika mapema tu jioni.. ...

Nilipofika, siku pumzika, nilielekea moja kwa moja kijiweni na katika baadhi ya maeneo ya mikusanyiko ya watu, na baada ya kuzurura kidogo pale kijijini jioni ile, na kuwaarifu viongozi wa chama, ndugu na wanainchi wa pale kijijini kwamba nimefika, lakini pia kusisitiza kuhusu nia yangu ya kuwawakilisha mjengoni, japo ilishafahamika hivyo tangu mapema kwamba nitatangaza nia.

Kila niliekutana nae aliniambia wewe umepita bana, wewe ndie mbunge wetu, usiwe na wasi, wala usiogope tutakuchagua. Nilipata, ujasiri na matumaini zaidi.
wanainchi kijijini pangu walinitia moyo sana.....

Usiku ukaingia tukapumzika. Pakakucha salama asubuhi.
Pale home kwetu kuna Baja, ule mpikipiki flani mkubwa, upo tu store, asubuhi ile nikaucheki kama uko sawa, nikakuta uko sawa, nikaupiga full tank mafuta, nikamtafuta dereva mzuri ninae mfahamu tukakubaliana posho, na nikamuelekeza mzunguko utaanzia wap na nitamlipaje, kisha tukaanza safari, kuzunguka katika baadhi ya kata nilizokua nime zitageti kuvuna na kupata kura nyingi za maoni na ambazo ninafahamika vizuri..

Kwa siku3 mfululizo, nilikua nimezunguka kwa uhakika sana na baja, katika kata 7, miongoni mwa kata zaidi ya 20 jimboni. haikua rahisi aise. kuna vitu vya kuvunja moyo sana, kuna vitu vya kukupa ujasiri na nguvu sana.

Ila kitu muhimu zadi kwangu, sikukata tamaa wala kubabaika hata chembe, bali nilisonga mbele na daima nikimtanguliza na kumshukuru Mungu. Mara zote nilimshirikisha nilipo ona ugumu au uzito wa jambo fulani anifanyie wepesi na anionyeshe njia ya kusonga mbele..

Tarehe ya kuchukua fomu ikawadia.
kama kawaida, na usafiri wangu wa baja, siku ya kwanza kabisa ya utoaji fomu, mapema saa5 asubuh nikafika ofisi za chama kuchukua fomu, huku baja tukiwa tumelipaki nje kidogo ya mji, kwasabb halikua na kibali, kadi au kitu chochote cha utambulisho, na kwahivyo tukapaki kwa kificho kukwepa manjagu yaani traffic wasituotee.

Kuna siku tulipo kua tunazunguka kwenye zile kata ilikua siku ya mnada, kuna afande aliwahi kutupiga mkono, dereva wangu wa baja alikua mkorofi kidogo, akampuuza, halafu akamlenga na baja yule askari alie tupiga mkono, afande akakwepa, tukampita kwa kasi ya ajabu, tukatokomea zetu na safari zetu, hakuthubutu kutufuata..
na kwahiyo siku ya kwenda kuchukua fomu tulihofia anaweza kuwepo maeneo ya mjini ikawa shida, coz ndio kituo chake cha kazi.

Bas,
Nikaenda nikachukua fomu kwenye ofisi za chama, kwa gharama ya wazi kabisaaaa ya tsh laki1.

Baada ya kupokea fomu na kusaini kwamba nimeshachukua fomu, katibu mkuu wa chama alienipa fomu, akanielekeza niende kwa katibu msaidizi, nikafanye malipo na kupewa risiti ya malipo na kisha nitapewa maelekezo mengine.

Nikafanya hivyo, na nikaelezwa na katibu msaidizi kwamba, nje ya gharama za fomu, natakiwa kuchangia tsh million3.5 kama gharama za usafiri, tutakapokua tunawazungukia wanainchi kwa usafiri wa pamoja na watia nia wengine. Tulikua watia nia zaidi ya 10.

Kumbuka nimetoka chuo na laki 5 pekee cash in hand. hiyo hiyo nauli, hiyo hiyo mafuta ya baja, hiyo hiyo nilipie fomu ya kugombea, chakula na malazi. Nilipoambiwa million 3.5 tena nilichoka kabisa 🐒...

Ila kamwe sikukata tamaa hata chembe.....

Nia, dhamira na shauku ilikua bado juu mno, Imani ilikua tele kwamba I'm going to win the election na kua mbunge wa wanainchi..

Basi, nikamuuliza naibu katibu mkuu, hiyo million3.5 ni Lazima au hiyari? na naweza kutoa kiasi kisha nikamalizia baadae?

Akasema gharama hizo ni Lazima na naweza lipa kidogo kisha ukamalizia badea.

Nikachangia laki1 nyingine kutoka kwenye ile laki5 yangu..
Baada ya kufanya malipo hayo, nikaaga nikaondoka.

Nikatoka nje ya jengo la chama, kuna washroom nikaingia huku kichwa kinawaka moto, najiuliza hiyo 3.4m ntaitoa wap? Maana nimepunguza laki 1 tu.

Nikaingiza mkono mfukoni kucheki kiasi nilichobaki nacho, nikajikuta nina elfu 75,000 pekee, na safari ya kampeni bado haijaanza. Maana niliambiwa kula, kunywa na kulala kwa kila mtia nia anajitegemea mwenyewe kwa gharama zake.

Nikarudi nyumbani, nikajaza fomu vizuri, kesho yake nikairudisha na ikapokelewa. Siku2 baada ya zoezi la kurejesha fomu kwisha, wakanipigia simu kwamba ntahitajika ofisini kutakua na kikao cha watia nia wote, kupewa muongozo wa kampeni zitakavyokua. basi, siku husika ilipofika nikaenda, tukafanya kikao na kupeana utaratibu pamoja na watia nia wenzangu zaidi ya 10....

Mpaka kampeni za kura za maoni zina anza nina elf35 mfukoni....

You know what happened.

Stay tuned nakuja kumalizia.

Wacha nipate tama la maji kwanza 🐒
 
Umenikumbusha mjomba wangu stori zake enzi za NCCR ya Bwana Mrema ya moto.Ananiamba unaiona ile hotel ? Mule ndimo tulikuwa na bwana Mrema tunagawiwa vyeo .Eti yeye alipewa ukuu wa mkoa wa Shinyanga😄😄😄.
 
Umenikumbusha mjomba wangu stori zake enzi za NCCR ya Bwana Mrema ya moto.Ananiamba unaiona ile hotel ? Mule ndimo tulikuwa na bwana Mrema tunagawiwa vyeo .Eti yeye alipewa ukuu wa mkoa wa Shinyanga[emoji1][emoji1][emoji1].
Haahhahah vyama vya upinzani mara nyingi huwa vinanipa raha wanadesturi ya kugawa vyeo hata kabla hawajaunda serikali.

Nakumbuka Freeman Mbowe 2020 alijiteua Waziri mkuu wa JMT
 
Ndio nilikua nimemaliza tu chuo kikuu, na nilikua na kiasi cha tsh laki5 tu, cash in hand, fedha ambazo nilikua nikijibana bana na kudunduliza nikiwa chuo kwa madhumuni haya haya ya kugombea ubunge. Nikajitosa katika mchakato wa ndani ya chama, kuomba ridhaa ya wanachama nipeperushe bendera ya chama kwenye uchuguzi mkuu....

Nakumbuka mtihani wa mwisho chuo, mwaka wa tatu semester ya mwisho ulikua tarehe za mwanzo za mwezi July mwaka huo wa uchaguzi, na fomu kura za maoni kwenye chama nilichokusudia kuomba ridhaa yake, zilianza kutolewa katikati ya mwezi huo huo July. Lakini pia na kampeni zilianza mwisho mwa mwezi huo huo July, mwaka ule wa uchaguzi...

Basi bana,
Dhamira na nia ya dhati kwenda kuomba ridhaa ya wanainchi iliuteka na kuutawala sana mutima wangu.

Matumaini ya kushinda uchaguzi huo yalinizidi kipimo. Vipaumbele vyangu, mipango na mikakati ya kuwakomboa wanainchi katika changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo pale jimboni, ilikua wazi sana, na ilinipa ujasiri sana nafsini mwangu. Na kwamba kivyovyote vile nitafaulu kupata ridhaa hiyo....

Nilikuwa nashauku, nguvu, ari, na moyo wa kipekee sana, kwenda kuwaongoza wanainchi.
Nilikua nikifanya maombi kama dose ya masaa, kila nilipopata wasaa, nilimuomba na kumshukuru Mungu anionyeshe njia...

Bas,
siku ikafika,
Baada ya tu kumaliza paper chuoni, nikaenda kuwaaga ndugu zangu pale mjini, na kuwaeleza safari yangu kuelekea mkoani kijijini.

Kesho yake asubuhi nikanyaka ndinga, huyo moja kwa moja mpaka kijijini, nilifika mapema tu jioni.. ...

Nilipofika, siku pumzika, nilielekea moja kwa moja kijiweni na katika baadhi ya maeneo ya mikusanyiko ya watu, na baada ya kuzurura kidogo pale kijijini jioni ile, na kuwaarifu viongozi wa chama, ndugu na wanainchi wa pale kijijini kwamba nimefika, lakini pia kusisitiza kuhusu nia yangu ya kuwawakilisha mjengoni, japo ilishafahamika hivyo tangu mapema kwamba nitatangaza nia.

Kila niliekutana nae aliniambia wewe umepita bana, wewe ndie mbunge wetu, usiwe na wasi, wala usiogope tutakuchagua. Nilipata, ujasiri na matumaini zaidi.
wanainchi kijijini pangu walinitia moyo sana.....

Usiku ukaingia tukapumzika. Pakakucha salama asubuhi.
Pale home kwetu kuna Baja, ule mpikipiki flani mkubwa, upo tu store, asubuhi ile nikaucheki kama uko sawa, nikakuta uko sawa, nikaupiga full tank mafuta, nikamtafuta dereva mzuri ninae mfahamu tukakubaliana posho, na nikamuelekeza mzunguko utaanzia wap na nitamlipaje, kisha tukaanza safari, kuzunguka katika baadhi ya kata nilizokua nime zitageti kuvuna na kupata kura nyingi za maoni na ambazo ninafahamika vizuri..

Kwa siku3 mfululizo, nilikua nimezunguka kwa uhakika sana na baja, katika kata 7, miongoni mwa kata zaidi ya 20 jimboni. haikua rahisi aise. kuna vitu vya kuvunja moyo sana, kuna vitu vya kukupa ujasiri na nguvu sana.

Ila kitu muhimu zadi kwangu, sikukata tamaa wala kubabaika hata chembe, bali nilisonga mbele na daima nikimtanguliza na kumshukuru Mungu. Mara zote nilimshirikisha nilipo ona ugumu au uzito wa jambo fulani anifanyie wepesi na anionyeshe njia ya kusonga mbele..

Tarehe ya kuchukua fomu ikawadia.
kama kawaida, na usafiri wangu wa baja, siku ya kwanza kabisa ya utoaji fomu, mapema saa5 asubuh nikafika ofisi za chama kuchukua fomu, huku baja tukiwa tumelipaki nje kidogo ya mji, kwasabb halikua na kibali, kadi au kitu chochote cha utambulisho, na kwahivyo tukapaki kwa kificho kukwepa manjagu yaani traffic wasituotee.

Kuna siku tulipo kua tunazunguka kwenye zile kata ilikua siku ya mnada, kuna afande aliwahi kutupiga mkono, dereva wangu wa baja alikua mkorofi kidogo, akampuuza, halafu akamlenga na baja yule askari alie tupiga mkono, afande akakwepa, tukampita kwa kasi ya ajabu, tukatokomea zetu na safari zetu, hakuthubutu kutufuata..
na kwahiyo siku ya kwenda kuchukua fomu tulihofia anaweza kuwepo maeneo ya mjini ikawa shida, coz ndio kituo chake cha kazi.

Bas,
Nikaenda nikachukua fomu kwenye ofisi za chama, kwa gharama ya wazi kabisaaaa ya tsh laki1.

Baada ya kupokea fomu na kusaini kwamba nimeshachukua fomu, katibu mkuu wa chama alienipa fomu, akanielekeza niende kwa katibu msaidizi, nikafanye malipo na kupewa risiti ya malipo na kisha nitapewa maelekezo mengine.

Nikafanya hivyo, na nikaelezwa na katibu msaidizi kwamba, nje ya gharama za fomu, natakiwa kuchangia tsh million3.5 kama gharama za usafiri, tutakapokua tunawazungukia wanainchi kwa usafiri wa pamoja na watia nia wengine. Tulikua watia nia zaidi ya 10.

Kumbuka nimetoka chuo na laki 5 pekee cash in hand. hiyo hiyo nauli, hiyo hiyo mafuta ya baja, hiyo hiyo nilipie fomu ya kugombea, chakula na malazi. Nilipoambiwa million 3.5 tena nilichoka kabisa 🐒...

Ila kamwe sikukata tamaa hata chembe.....

Nia, dhamira na shauku ilikua bado juu mno, Imani ilikua tele kwamba I'm going to win the election na kua mbunge wa wanainchi..

Basi, nikamuuliza naibu katibu mkuu, hiyo million3.5 ni Lazima au hiyari? na naweza kutoa kiasi kisha nikamalizia baadae?

Akasema gharama hizo ni Lazima na naweza lipa kidogo kisha ukamalizia badea.

Nikachangia laki1 nyingine kutoka kwenye ile laki5 yangu..
Baada ya kufanya malipo hayo, nikaaga nikaondoka.

Nikatoka nje ya jengo la chama, kuna washroom nikaingia huku kichwa kinawaka moto, najiuliza hiyo 3.4m ntaitoa wap? Maana nimepunguza laki 1 tu.

Nikaingiza mkono mfukoni kucheki kiasi nilichobaki nacho, nikajikuta nina elfu 75,000 pekee, na safari ya kampeni bado haijaanza. Maana niliambiwa kula, kunywa na kulala kwa kila mtia nia anajitegemea mwenyewe kwa gharama zake.

Nikarudi nyumbani, nikajaza fomu vizuri, kesho yake nikairudisha na ikapokelewa. Siku2 baada ya zoezi la kurejesha fomu kwisha, wakanipigia simu kwamba ntahitajika ofisini kutakua na kikao cha watia nia wote, kupewa muongozo wa kampeni zitakavyokua. basi, siku husika ilipofika nikaenda, tukafanya kikao na kupeana utaratibu pamoja na watia nia wenzangu zaidi ya 10....

Mpaka kampeni za kura za maoni zina anza nina elf35 mfukoni....

You know what happened.

Stay tuned nakuja kumalizia.

Wacha nipate tama la maji kwanza 🐒
Wewe endelea kupiga blaa blaa tu wakati Rufiji imeshazama huko. Mnakurupuka kuanzisha miradi ambayo haijafanyiwa full EIA matokeo yake ndio hayo.
 
Na mwakani unapita tena watake wasitake 🤣🤣🤣
N’wei mama mbunge nipo hapa wadada nafasi ishajaa mumsubiri Manara labda amuache Zay mkajiweke 🤣🤣🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
 
we tuliza ball tu,
hii mambo ni aste aste, slow but sure 🐒

na sasa situmii tena Baja, natumia mkoko wa maana, wewe acha tu 🐒
 
🤣 halafu bana baja lipo tu store mtumishi ila vile vikanyagio kwa ajili ya abiria nilivikata vyote wakati ule nazunguka kwenye kata dah,

barabara zilikua mbovu sana aise 🐒
Sasa hizo barabara mbovu umewarekebishia wananchi au ndio karibu na uchaguzi unaenda kuwachongea na greda afu watajiju!! 🤣🤣🤣🤣
Hao wananchi walikuwa na imani kubwa na wewe usiwaangushe sasa.!!
 
Back
Top Bottom