Kwa mara ya kwanza nimehisi kuwa na umuhimu

Kwa mara ya kwanza nimehisi kuwa na umuhimu

Baada ya kumaliza Chuo mwaka jana life ikapiga vibaya mno, kila muda nilikuwa nawaza jinsi gani nitasaidia familia yangu (Ni mtoto wa kiume mkubwa) Ilikuwa inauma sana pale ambapo unaamka asubuhi huna cha kufanya hadi kuna muda unahisi kama kifua kinabana.

Kuna muda nakaa najitafakari naona kama ni mzigo home, but hakuna aliyewahi niambia, sister kuna muda mshahara ukitoka ananitoa laki basi maisha yanaenda.

Mwanzoni mwa mwaka huu kuna mchongo nikaupata katika harakati za kushughulikia ili utiki, nikawa naingia katika mzozo sana na mzee maana mara nyingi nilikuwa narudi usiku anamind, ananisema ila kwa upande wangu inaniuma lakini nakaza ili isionekane kama imeuma (akaanza kuona kama namdharau) sasa kuna muda huna nauli kuomba siwezi so nachukua bike kutoka home hadi kwenye michakato as usual narudi usiku.

Kwenye kuhangaika hivyo mchongo ukatiki nikatumiwa mkataba nikasign nikaenda kazini, nikaona afadhali nimetoka home, mchongo unalipa fresh tu, silipi kodi wala bills kama maji, umeme na utilities zingine, na ni apartment nzuri unyama ni mwingi.

Leo account imesoma kwa newhires wote mzigo umesoma almost M 8, nikatoa M2 nimewatumia home, bi mkubwa ameshukuru mnooo, kuna ile feeling ya kuwa Now na wewe ni wa muhimu, sijawahi jisikia vizuri kama leo, ameninenea maneno ya Baraka hadi nikahisi zinajaa physically. Leo na mimi nimehisi ni wa muhimu.

m8 mkuu,

sijawai shika iyo pesa….
 
maisha yanaogopesha sana kwa sisi watoto wa kiume wakubwa😬

sijui nikimaliza chuo itakuwaje
Hata usiwaze kaka mambo hua yanakaaga sawa yenyewe kikubwa ww nae uwe unajitosa 🤔🤔shule ina njia zake na mtaa una njia zake, atakaekusaidia sio unayeamini atakusaidia ukimaliza shule utakutana na watu wengn kbs
 
Usisahau zaka na sadaka hapo tenga kama millioni 1.. then hIyo million 5 iliyobaki nunua uwanja mkubwa sana hata wa million 3 then 2 nenda nayo taratbu kwa mambo mengine

NB; USISAHAU KUJIPONGEZA KWA KUFANYA JAMBO LINALOKUPA FURAHA SANA
Zaka na sadaka ni WIZI.

Mleta mada usipeleke hata Mia kanisani.

Bora hiyo hela ukawape yatima wasio jiweza au walemavu barabarani.
 
Wengi mnajaribu kumbishia mleta mada kuwa account haiwezi kusoma M8 lakini labda yeye alichokosea ni kuweka story yake nusu nusu au kutoiweka vizuri.


Yawezekana hizo M8 ni limbikizo tokea huko mwanzo wa mwaka aliposema kuwa ndio hiyo mishe imetiki. Pia amesema anaishi bila cost yoyote so hebu mpeni nafasi amalizie story au arekebishe kabla hamjambishia.
Amesema ni Mwl.
Fanya kaanza kazi mwezi wa Kwanza
Fanya hakatwi bodi Wala chama sijui Cha walimu.
Fanya pesa anayolipwa hata kumi hakatwi.
Na huu ni mwezi wa nane.
Jibu ni kuwa Mwl analipwa 1m kwa mwezi na toka mwezi wa Kwanza hajatumia hiyo hela hata Mia
Ndio hiyo 8m ilivokuja Au sio !
 
Amesema ni Mwl.
Fanya kaanza kazi mwezi wa Kwanza
Fanya hakatwi bodi Wala chama sijui Cha walimu.
Fanya pesa anayolipwa hata kumi hakatwi.
Na huu ni mwezi wa nane.
Jibu ni kuwa Mwl analipwa 1m kwa mwezi na toka mwezi wa Kwanza hajatumia hiyo hela hata Mia
Ndio hiyo 8m ilivokuja Au sio !
Akikujibu nitag
 
Back
Top Bottom