Kwa mara ya kwanza nimemkumbuka Hayati Magufuli tokea afariki dunia

Kwa mara ya kwanza nimemkumbuka Hayati Magufuli tokea afariki dunia

Sasa huo mfumo wako imara utatengenezwa na akina nani walio imara?

Najua utasema chama fulani,hebu ni tajie chama chochote unachokiona wewe imara kuanzia ngazi ya chama chao tu humo humo.

Mtu mmoja imara anaweza kutengeneza mfumo imara kutokana na misimamo yake wengine wakaiga kutoka kwake.

Mfano (sijui dini yako),ila kwangu Yesu pekee kupitia misimamo yake na matendo yake aliweza kutengeneza imani iliyo imara ya kikristo.

Mohamed kupitia yeye aliweza kutengeneza na kuisimika imani ya Kislam na wengine wakaiga kutoka kwake.

Mao ndiye aliye itransform China kwani misimamao na mawazo yake ndio leo imeifanya China kuwa vile.

So kitu chochote imara lazima kianze na mtu imara,so kupitia yy wale anaofanya kazi wataiga kile akifanyacho na ndipo mfumo imara huanza kusimikwa.
Magufuli alikuwa mtu imara na alishaanza kuweka mifumo imara ambayo watu wanahangaika kuiharibu Leo hii. Lakini legacy yake ipo na itaendelea kuwepo na nina Imani tutampata kiongozi mwingine atakayeiga mtindo wa utawala kama wa Hayati JPM.
 
Sikuwahi kumkubali huyu mwamba kipindi chake chote Cha utawala mpaka anakufa.

Akili imenikaa sawa sawa, kama binadamu ni kweli alikuwa na mapungufu yake hakuna mkamilifu.

Nakubali huyu mwamba alikuwa na nia ya dhati ya kulipigania hili taifa. Nahisi labda njia tu ndo zilitukwaza baadhi yetu nimemsahe pale ambapo alinikwaza kama mwananchi wa kawaida.

Nampa udhuru pia kwasababu naamini ilitakiwa iwe vile, kwa namna ambavyo Watanzania tulivyo ilimlazimu awe vile. Kubembelezana na kulambanalambana kumetufanya tuchelewe Sana. Kama kiongozi alikuwa sahihi kuwa mkali hasa Kwa mafisadi, wahujumu uchumi, mabeberu na vibaraka wa mabeberu.

Kwa haya yanayoendelea nchini ni dhahiri tunarudishwa nyuma mnoooo haina ubishi. Kama mtanzania nimeona nisiwe mnafki, nasema kweli kutoka moyoni mwangu.

Alisema Magufuli "mutanikumbuka, tena sio Kwa ubaya mtanikumbuka Kwa mazuri" Nakiri kumkumbuka Magufuli Kwa mazuri yake.

Mnisamehe Watanzania wenzangu ambao niliwakwaza Kwa namna yoyote ile hasa wale ambao walibahatika kuwa na maono ya haraka juu ya uzuri wa Magufuli. Nakiri nilitenda kosa la kumzungumza vibaya mzee wetu.

Magufuli ametenda, kwa hali iliyopo Sasa hivi Kila mtu anashuhudia. Na huko tuendako tutaimba nyimbo moja.

Ahsanteni sana.
Wale wanyevyeti feki na wezi watakujibu nenda kazikwe nae chato.. ukweli ni kwamba hata Yesu mazuri yake yalikubalika mpaka kwa wayahudi baada ya kuondoka duniani kifo kilichosababishwa na mikono ya binadamu..

Lakini vile ambavyo ilikuwa iwe vile ili ukweli usambae duniani basi Mungu akaruhusu iwe vile..

Sahivi duniani tunakumbukizi ya kufa kwake mpaka mateso yake.. na damu yake kiroho hutumika kusafisha na kutakasa chochote...

[emoji23] [emoji23] [emoji23].. huwa najiuliza ingekuwaje Yesu angekufa kwa kisukari.. ile kauli yake ya hii ndio damu yangu na mkate huu ndio mwili wangu tungeituimia wapi???

Sasa na Magufuli bila kufa kipindi ambacho taifa lilimuhitaji tungejuaje kwamba kweli alijitoa maisha yake kwa watanzania.. na kubwa zaidi tungejuje kwamba akifa tutamkumbuka kiasi hiki?? [emoji23]

Mungu hajawahi kukosea.. na wala hatuwezi sema amejitenga na sisi.. binafsi ninaamini anatupangia jema zaidi.

R.I.P JPM

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Sasa na Magufuli bila kufa kipindi ambacho taifa lilimuhitaji tungejuaje kwamba kweli alijitoa maisha yake kwa watanzania.. na kubwa zaidi tungejuje kwamba akifa tutamkumbuka kiasi hiki??
emoji23.png

Mungu hajawahi kukosea.. na wala hatuwezi sema amejitenga na sisi.. binafsi ninaamini anatupangia jema zaidi.

R.I.P JPM
Nina Imani kweli mazuri yanakuja, Magufuli ameonesha njia na kweli inawezekana.
 
Sikuwahi kumkubali huyu mwamba kipindi chake chote Cha utawala mpaka anakufa.

Akili imenikaa sawa sawa, kama binadamu ni kweli alikuwa na mapungufu yake hakuna mkamilifu.

Nakubali huyu mwamba alikuwa na nia ya dhati ya kulipigania hili taifa. Nahisi labda njia tu ndo zilitukwaza baadhi yetu nimemsahe pale ambapo alinikwaza kama mwananchi wa kawaida.

Nampa udhuru pia kwasababu naamini ilitakiwa iwe vile, kwa namna ambavyo Watanzania tulivyo ilimlazimu awe vile. Kubembelezana na kulambanalambana kumetufanya tuchelewe Sana. Kama kiongozi alikuwa sahihi kuwa mkali hasa Kwa mafisadi, wahujumu uchumi, mabeberu na vibaraka wa mabeberu.

Kwa haya yanayoendelea nchini ni dhahiri tunarudishwa nyuma mnoooo haina ubishi. Kama mtanzania nimeona nisiwe mnafki, nasema kweli kutoka moyoni mwangu.

Alisema Magufuli "mutanikumbuka, tena sio Kwa ubaya mtanikumbuka Kwa mazuri" Nakiri kumkumbuka Magufuli Kwa mazuri yake.

Mnisamehe Watanzania wenzangu ambao niliwakwaza Kwa namna yoyote ile hasa wale ambao walibahatika kuwa na maono ya haraka juu ya uzuri wa Magufuli. Nakiri nilitenda kosa la kumzungumza vibaya mzee wetu.

Magufuli ametenda, kwa hali iliyopo Sasa hivi Kila mtu anashuhudia. Na huko tuendako tutaimba nyimbo moja.

Ahsanteni sana.
Hiyo nyimbo moja sasa..........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maza is beating bigger
Kwa alivyo kuwa yule bwana, ni bora kuishi haya maisha ya sasa hivi! Sitaki kuwa na kumbukumbu za wanawake za kusahau kila uchungu wa kuzaa! Wangekuwa wanakumbuka, wengine wangeishia mtoto mmoja tu!
 
Habarini ndugu zangu! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Tangu kutokee kwa msiba wa Raisi wetu kipenzi MAGUFULI ni miaka miwili imepita nimekuwa nikimkumbuka sana MAGUFULI hasa zile speech zake na namna alivyokuwa akiwajibika hasa kwenye kutumbua majipu ambao leo ndio viongozi wa juu kwenye awamu hii ambayo imejaa ufisadi na unafiki. Hakika MAGUFULI ulikuwa mchapakazi ulituhamasisha tufanye kazi tuinue uchumi wa nchi yetu nakumbuka msemo wako baba kuwa " uchumi wa Tanzania utajengwa na watanzania wenyewe". Hakika MAGUFULI hakupenda tuonekani wanyonge ukasema "sisi watanzania ni matajiri" .
Upumzike kwa amani Raisi wetu mpendwa MAGUFULI
Nuru ya bwana iwe na wewe kwenye makazi yako ya milele
Ameen Ameen [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom