Kwa mara ya kwanza nimemkumbuka Hayati Magufuli tokea afariki dunia

Magufuli alikuwa mtu imara na alishaanza kuweka mifumo imara ambayo watu wanahangaika kuiharibu Leo hii. Lakini legacy yake ipo na itaendelea kuwepo na nina Imani tutampata kiongozi mwingine atakayeiga mtindo wa utawala kama wa Hayati JPM.
 
Wale wanyevyeti feki na wezi watakujibu nenda kazikwe nae chato.. ukweli ni kwamba hata Yesu mazuri yake yalikubalika mpaka kwa wayahudi baada ya kuondoka duniani kifo kilichosababishwa na mikono ya binadamu..

Lakini vile ambavyo ilikuwa iwe vile ili ukweli usambae duniani basi Mungu akaruhusu iwe vile..

Sahivi duniani tunakumbukizi ya kufa kwake mpaka mateso yake.. na damu yake kiroho hutumika kusafisha na kutakasa chochote...

[emoji23] [emoji23] [emoji23].. huwa najiuliza ingekuwaje Yesu angekufa kwa kisukari.. ile kauli yake ya hii ndio damu yangu na mkate huu ndio mwili wangu tungeituimia wapi???

Sasa na Magufuli bila kufa kipindi ambacho taifa lilimuhitaji tungejuaje kwamba kweli alijitoa maisha yake kwa watanzania.. na kubwa zaidi tungejuje kwamba akifa tutamkumbuka kiasi hiki?? [emoji23]

Mungu hajawahi kukosea.. na wala hatuwezi sema amejitenga na sisi.. binafsi ninaamini anatupangia jema zaidi.

R.I.P JPM

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Nina Imani kweli mazuri yanakuja, Magufuli ameonesha njia na kweli inawezekana.
 
Hiyo nyimbo moja sasa..........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maza is beating bigger
Kwa alivyo kuwa yule bwana, ni bora kuishi haya maisha ya sasa hivi! Sitaki kuwa na kumbukumbu za wanawake za kusahau kila uchungu wa kuzaa! Wangekuwa wanakumbuka, wengine wangeishia mtoto mmoja tu!
 
Habarini ndugu zangu! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Tangu kutokee kwa msiba wa Raisi wetu kipenzi MAGUFULI ni miaka miwili imepita nimekuwa nikimkumbuka sana MAGUFULI hasa zile speech zake na namna alivyokuwa akiwajibika hasa kwenye kutumbua majipu ambao leo ndio viongozi wa juu kwenye awamu hii ambayo imejaa ufisadi na unafiki. Hakika MAGUFULI ulikuwa mchapakazi ulituhamasisha tufanye kazi tuinue uchumi wa nchi yetu nakumbuka msemo wako baba kuwa " uchumi wa Tanzania utajengwa na watanzania wenyewe". Hakika MAGUFULI hakupenda tuonekani wanyonge ukasema "sisi watanzania ni matajiri" .
Upumzike kwa amani Raisi wetu mpendwa MAGUFULI
Nuru ya bwana iwe na wewe kwenye makazi yako ya milele
Ameen Ameen [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…