Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,021
- 79,710
Uli overdose mjani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Big up kwa ushuhuda,ushuhuda unasaidia Sana kuamini kwa wengineNilikuwa nasikia tu na kusoma vitabu kwamba malaika wapo, na kwamba kuna watu wametokewa na malaika, lakini sikuelewa sana. Sasa na mimi kwa mara ya kwanza nimethibitisha malaika wapo.
Mwezi uliopita niliugua sana nikawa katika hali ya kufa. Nilikuwa sina hamu ya kula chakula, nilikuwa nasikia joto kali, mara baridi kali. Kichwa kilikuwa kinauma sana. Mwili wote ulikuwa umelegea, kwa sababu hiyo nilikuwa natamani kulala tu kila wakati. Nikahisi labda ni uchovu kwa sababu ya shamba nililokuwa nimelima siku kadhaa kabla ya kuanza kuugua. Hali ilivyozidi kuwa mbaya nilienda hospitali, wakanipima vipimo vyote muhimu lakini hawakuona tatizo lolote. Siku hiyohiyo kama saa saba hivi usiku niliamka kitandani nikaenda “toilet.” Taa ya umeme ilikuwa imeungua humo, ikanibidi nitumie tochi ya kwenye simu yangu inimulikie. Mara baada ya kujihudumia, nikiwa bado nimesimama pale, nilipatwa ghafla na kizunguzungu kikali sana. Nilikuja kutambua baadaye kumbe muda huohuo nilipoteza fahamu, na simu niliyokuwa nimeishika mkononi niliiachilia, bila kutambua, ikaangukia chooni(choo cha kukalia). Baada ya kupoteza fahamu kumbe nilidondoka chini; lakini kabla kichwa hakijagusa chini kwenye sakafu ya choo, kuna mtu alitokea ghafla akanidaka kichwa na kunisogeza nje ya mlango wa choo. Nikiwa bado chini fahamu zilirejea,nikamuona mtu huyo amenishika na kuniinua. Nikapata nguvu kidogo nikapanda tena kitandani kulala. Kabla sijalala nilitafuta simu yangu ili niwapashe habari ndugu na jamaa, yaliyonitokea. Simu sikuiona, kumbe ilikuwa imeangukia chooni ikajaa maji na kujizima!
To cut a long story short, nilihisi huenda udhaifu huo ni dalili ya Coronavirus(Covid-19) kwakuwa nilikuwa nimesikia kwamba dalili za wimbi la pili zinatofautiana kidogo na zile za wimbi la kwanza. Kwa sababu hiyo nikaanza kula sana matunda: malimao, vitunguu saumu, tangawizi, asali, nk. Namshukuru Mungu nimepona, na nimehakikisha kuwa ni kweli Mungu yupo na malaika wake wapo na wanawahudumia wanadamu. Huyo aliyenidaka alikuwa malaika japo mimi nilimuona katika umbo la kawaida tu la kibinadamu kama ilivyotokea kwa Ibrahimu. Asante Mungu kwakuwa sawasawa na ahadi yako katika Zab 91:11-12 uliniagizia malaika wako anilinde na mkononi mwake alinichukua, kichwa changu kisiumie sakafuni.
Huo ushuhuda usikawie kuuleta hapa, pleaseMalaika ni halisi, Yesu ni Halisi na Mungu Baba ni Halisi na Roho Mtakatifu ni halisi. Shetani na mapepo ni halisi, Mbingu ni halisi na Jehanamu ya moto ni Halisi. Binafsi nina shuhuda za hivyo vitu. Malaika nawajua nimewaona wawili kwa macho ya kiroho. Nimewahisi na kushuhudia uwepo wao kwangu zaidi ya miezi sita kwa jinsi ya kimwili. Kuna siku nitaleta shuhuda kuhusu Mungu Baba na muonekano wake, Yesu Kristo na Muonekano wake akiwa kwa Jinsi ya mwili na Jinsi ya uungu alionao kwa sasa. Usidanganyike na wapumbavu wanaosema hakuna Mungu, hao walikuwepo toka kizazi na kizazi. Kuna wanaosema hakuna Mungu wala uchawi wakijua wanachofanya kwa kiwa ni Mawakala na wengine ni kufuata mkumbo tu.
Malaika wapo na Ulimwengu usioonekana kwa macho ya nyama ipo tena una nguvu sana.