mediaman
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 451
- 688
- Thread starter
- #61
AminaAmina , ukipata bahati ya hivyo nikujitahidi kuwa na MUNGU sana.
Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AminaAmina , ukipata bahati ya hivyo nikujitahidi kuwa na MUNGU sana.
Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Akiaanzisha kanisa we utakuwa wa kwanza kukuokotaBig up kwa ushuhuda,ushuhuda unasaidia Sana kuamini kwa wengine
Mi si mtu wa kupelekwa pelekwa tu mkuu na sisi tunaongozwa na roho atuenend enendi tu kwa stlye za ulimwengu huuAkiaanzisha kanisa we utakuwa wa kwanza kukuokota
Mkuu wewe kweli una imani timilifu.Nilikuwa nasikia tu na kusoma vitabu kwamba malaika wapo, na kwamba kuna watu wametokewa na malaika, lakini sikuelewa sana. Sasa na mimi kwa mara ya kwanza nimethibitisha malaika wapo.
Mwezi uliopita niliugua sana nikawa katika hali ya kufa. Nilikuwa sina hamu ya kula chakula, nilikuwa nasikia joto kali, mara baridi kali. Kichwa kilikuwa kinauma sana. Mwili wote ulikuwa umelegea, kwa sababu hiyo nilikuwa natamani kulala tu kila wakati. Nikahisi labda ni uchovu kwa sababu ya shamba nililokuwa nimelima siku kadhaa kabla ya kuanza kuugua. Hali ilivyozidi kuwa mbaya nilienda hospitali, wakanipima vipimo vyote muhimu lakini hawakuona tatizo lolote. Siku hiyohiyo kama saa saba hivi usiku niliamka kitandani nikaenda “toilet.” Taa ya umeme ilikuwa imeungua humo, ikanibidi nitumie tochi ya kwenye simu yangu inimulikie. Mara baada ya kujihudumia, nikiwa bado nimesimama pale, nilipatwa ghafla na kizunguzungu kikali sana. Nilikuja kutambua baadaye kumbe muda huohuo nilipoteza fahamu, na simu niliyokuwa nimeishika mkononi niliiachilia, bila kutambua, ikaangukia chooni(choo cha kukalia). Baada ya kupoteza fahamu kumbe nilidondoka chini; lakini kabla kichwa hakijagusa chini kwenye sakafu ya choo, kuna mtu alitokea ghafla akanidaka kichwa na kunisogeza nje ya mlango wa choo. Nikiwa bado chini fahamu zilirejea,nikamuona mtu huyo amenishika na kuniinua. Nikapata nguvu kidogo nikapanda tena kitandani kulala. Kabla sijalala nilitafuta simu yangu ili niwapashe habari ndugu na jamaa, yaliyonitokea. Simu sikuiona, kumbe ilikuwa imeangukia chooni ikajaa maji na kujizima!
To cut a long story short, nilihisi huenda udhaifu huo ni dalili ya Coronavirus(Covid-19) kwakuwa nilikuwa nimesikia kwamba dalili za wimbi la pili zinatofautiana kidogo na zile za wimbi la kwanza. Kwa sababu hiyo nikaanza kula sana matunda: malimao, vitunguu saumu, tangawizi, asali, nk. Namshukuru Mungu nimepona, na nimehakikisha kuwa ni kweli Mungu yupo na malaika wake wapo na wanawahudumia wanadamu. Huyo aliyenidaka alikuwa malaika japo mimi nilimuona katika umbo la kawaida tu la kibinadamu kama ilivyotokea kwa Ibrahimu. Asante Mungu kwakuwa sawasawa na ahadi yako katika Zab 91:11-12 uliniagizia malaika wako anilinde na mikononi mwake alinichukua, kichwa changu kisiumie sakafuni.
Bado, mkuu.Mkuu wewe kweli una imani timilifu.
Endelea hivyo hivyo sio wale wanaenda kwa Kakobe na Mwamposa.
Hujijui lakini Roho Mwema yupo ndani yako.Bado, mkuu.
Natamani nimjue sana Mwana wa Mungu; niwe mtu aliyekomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe. Ili nisiwe tena kama mtoto, nikitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila. Waefeso 4:13-14
AmenMungu akipenda kukufanyia Jambo Ni kwa upendo wake tu. Mimi hapa nyumbani kwangu hiyo Beena tumepewa na imekuwa Ni wakati nzuri kwa familia yangu maana wote tumepata neema hiyo na si Mara moja au mbili ni Kila Mara. Utukufu Ni kwa Mungu muumba wa vyote.
Amina mileleGlory to God,.
Mungu anajidhihirisha kwetu kwa namna nyingi thus way kila mtu ana namna yake(miujiza) ya kumjua Mungu.Kwa nini makanisa ya kilokole mafundisho yao huegemea juu ya miujiza? Na ushuhuda wa miujiza?
Miujiza ipo toka Mwanzo hadi sasa ni muujiza, uwepo wako na uimbaji wako tu ni muujiza. Kimsingi, miujiza ipo kwa ajili ya kutujenga kiimani. Yesu aliponya, alilisha watu, alifufua watu n.k hiyo yote ni miujiza. Sema kosa la kanisa la sasa ni kufanya muujiza ni muhimu kuliko Neno na maisha ya kumpendeza/kujitoa kwa ajili ya Mungu. Yesu alifundisha Neno na kuhubiri sana kuliko kutenda miujiza.Kwa nini makanisa ya kilokole mafundisho yao huegemea juu ya miujiza? Na ushuhuda wa miujiza?
Mungu amekuonekania, usimwacheAsante Mungu kwakuwa sawasawa na ahadi yako katika Zab 91:11-12 uliniagizia malaika wako anilinde na mikononi mwake alinichukua, kichwa changu kisiumie sakafuni