Kwa Mara ya Mwisho nimeamua kuwa support CHADEMA, Watanzania wenzangu 2025 ni Mwaka wa kujisahihisha "say NO to CCM"

Alitamka kww mdomo wake na tulimsikia kwa masikio yetu, ifahamike tulikuwa tumefikia hatua ya kura ya maoni akagomea. Wakati wake hakukuwa na CCM, yeye ndio alikuwa CCM.
Kura ya maoni ilikuwa na maana Gani Kwa Taifa ikiwa CCM ilihakikisha imevuruga Rasimu ikawa mbovu kuliko Katiba iliyopo?

Huo mchakato Unadhani kwann haukumaliziwa na aliyekuwa madarakani wakati Ule?

CCM ndo haitaki Katiba mpya, msimsingizie Magu pekee.
 
Nimekatazwa, nimefunzwa na nimeaswa ni haramu kushiriki mchezo wowote wa kuiondoa CCM, mimi ni nani nisisikilize wosia huo
Natamani ujumbe huu Kila Mtu ausome.ili Ajue ni jinsi Gani CCM Ina Nguvu katika hii nchi na CCM haitokuja Kutoka madarakani.
Kidumu Chama
 
Ndio nimekuambia anzisha chama uongee unachotaka, yeye Mbowe na chama chake wameamua kuongea hayo usiyoyapenda.
Mbowewe ni mtu mmoja, kama ameamua kuunga juhudi apishe, aje mkt mwingine.
 
Labda hujui unaongea nini, bunge la katiba lilimalizika muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, hivyo ikabidi ufanyike uchaguzi kwanza, kisha utawala unaofuata usimamie kura ya maoni. Lakini dhalimu alikataa waziwazi. Kura ya maoni ingefanyika ndio wananchi wangeweza wazi wakitakacho. Kwahiyo kama unataka kupotosha ubaki kwenye mstari huo.
 
Mbowewe ni mtu mmoja, kama ameamua kuunga juhudi apishe, aje mkt mwingine.

Anzisha chama mkuu ukae nafasi uitakayo. Mbowe atatoka, tena ni kama amechelewa, lakini kumsema yule kiongozi muovu yuko sahihi.
 
Mchakato ulianza mara tu baada ya kuingia madarakani 004, miaka 5 haikutosha kukamilisha mchakato?

Na ikiwa aliyepo anataka Katiba mpya, Kwann alimpeleka Mbowwee gerezani,

Adui yetu ni CCM, tusipoteze target.
 
Anzisha chama mkuu ukae nafasi uitakayo. Mbowe atatoka, tena ni kama amechelewa, lakini kumsema yule kiongozi muovu yuko sahihi.
Amseme Kwa MABAYA na akiri MAZURI yake pia.

Mtu ambaye ktk utawala wake tulinunua Mchele 1000 Kwa kilo, umtukane na kushukuru kiongozi anaesababisha tunanunua Mchele 3500?
 
Chadema ni CCM B
Mkt anakera sn,

Unaweza shangaa Hadi inafika 2025 mkt anamsema Magu na kumshukuru sa100,

Mwananchi ataona ni Bora amchague Sa100 maana ameungwa mkono na Mpinzani.

Yaani hii inaitwa, mzamiaji hodari anafia ufukweni.🙃🙃
 
Mchakato ulianza mara tu baada ya kuingia madarakani 004, miaka 5 haikutosha kukamilisha mchakato?

Na ikiwa aliyepo anataka Katiba mpya, Kwann alimpeleka Mbowwee gerezani,

Adui yetu ni CCM, tusipoteze target.

Mchakato wa katiba huwa unapaswa kuchukua muda gani boss? Alimpeleka Mbowe gerezani maana hizo ndio siasa alizorithi toka kwa dhalimu.

Ni wapi umeonyeshwa CCM sio adui yetu?
 
Amseme Kwa MABAYA na akiri MAZURI yake pia.

Mtu ambaye ktk utawala wake tulinunua Mchele 1000 Kwa kilo, umtukane na kushukuru kiongozi anaesababisha tunanunua Mchele 3500?

Hayo mazuri yake nani amekuzuia ww kuyasema? Sio wajibu wa Mbowe kusemea matamanio yako. Kama bei ya chakula ni ghali, huu si ndio muda sahihi wa kuanzisha chama ili uongelee hiyo bei ndogo maana uungwaji mkono upo wa kutosha?
 
Wewe acha kupotosha mbona kasema Kanda ya Nyasa inailisha nchi kwa 70% ila ndio Ina umaskini wa kutosha. Na akasema 2025 uchaguzi utakua mrahisi maana CCM wamefeli Kila kitu. Ameenda mbali zaidi na kusema yeyote chini ya miaka 40 akiipigia kura CCM akatolewe mapepo!!

Tatizo hamfuatilii mikutano mnakimbilia tu kupost humu!!
 
Mnataka mumzunguke mmiliki wa Chama? Mbowe fukuza hao watakuharibia chama chako.
 
Hayo mazuri yake nani amekuzuia ww kuyasema? Sio wajibu wa Mbowe kusemea matamanio yako. Kama bei ya chakula ni ghali, huu si ndio muda sahihi wa kuanzisha chama ili uongelee hiyo bei ndogo maana uungwaji mkono upo wa kutosha?
Vyama vya siasa vinatakiwa visizidi 3.

Why Kila anaekuwa na mawazo tofauti aanzishe chama?

Viongozi wapokee tu ushauri, ni Kwa Nia njema.
 
Mchakato wa katiba huwa unapaswa kuchukua muda gani boss? Alimpeleka Mbowe gerezani maana hizo ndio siasa alizorithi toka kwa dhalimu.

Ni wapi umeonyeshwa CCM sio adui yetu?
Mnapompongeza sa100 Kwa kuruhusu mikutano aliyoifungia Kwa miaka 2 ambayo haikuwahi kukatazwa na KATIBA.
 
Yaani anavyomtukana Magu na kumshukuru sa100 waeza Dhani Magu alikuwa kiongozi Kutoka ACT wazalendo.

Mabaya ya Magu yaungwe na kutupiwa CCM Kwa ujumla maana ndiyo ilomchagua.
Hawatakuelewa
 
Tatizo chama hiki ni Cha wale LGBTQ, chini ya Makamu mwenyekiti wa chama..ambaye ni LGBTQ mwandamizi.....hahahahah..wajameni mnataka kuharibu inchi hii
 
Alitamka kww mdomo wake na tulimsikia kwa masikio yetu, ifahamike tulikuwa tumefikia hatua ya kura ya maoni akagomea. Wakati wake hakukuwa na CCM, yeye ndio alikuwa CCM.
Katiba mpya ilikwamishwa na Magufuli?Hivi umeanza kufuatilia siasa 2015?
 
Mataga mna vituko sana, nyie ni jokers[emoji1787]
 
Vyama vya siasa vinatakiwa visizidi 3.

Why Kila anaekuwa na mawazo tofauti aanzishe chama?

Viongozi wapokee tu ushauri, ni Kwa Nia njema.

Kwakuwa ushauri wako haupokelewi na hivyo vyama, anzisha chako uwe unachukua ushauri boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…