Kwa masikitiko makubwa, mwandani wangu ananisaliti na wanaume zaidi ya wa 5

mwanzo nilikuwa sijuiiii,,
niliyasoma kwa vitabu...
mwanzo nilikuwa sijui mapenziiii...
nilihadithiwa na mababuu....
sasa nimekuwa nimejua mapenzi uchizi...
yule unaempenda ndio anakunyma usingizi,,,,,
 
Sina kinyongo wala sina mpango wa kumdhuru mtu.!

Utadhurika wewe kiroho na kimwili... Sio kwa mixer hiyo aisee
 
Huu ndiyo uanaume ,Hapa amelala, nimerudisha simu kama ilivyokua. Sina kinyongo wala sina mpango wa kumdhuru mtu.

Nb. Nenda kapime ukimwi hatakama unaogopa wewe pima tuu, majibu yakiwa fresh achana nae
 
Screen shot hizo msg jitumie kwako kisha futa sent item kwenye simu yake, niamin mimi anaweza kuja kukuruka hadi ukashangaa, atazifuta shwaaa na kusema unatunga maneno ya uongo ili muachane uende kwa mademu zako.
Point ya msingi hii.

Nilikua na manzi mshenzi sana. Nilimfuma live na mteja dukani wanaongea kimahaba mida ya jioni. Baadae nikafuma sms za chatting na wanaume kibao.

Nikamkalisha chini kumpa makavu akaanza kupanic na kujiliza. Wakati huo alishazifuta zile sms zamani na wale wanaume akawalima block kimya kimya. Likamtoka neno lilionikera nikamzaba kofi moja matata.

Msala ukanigeukia mimi kua nimempiga, namnyanyasa. Akaenda kunishtaki kwa ndugu zake na dada zangu mwisho ikaonekana mimi ndio nimemkosea na vikao vikaamua nimuombe msamaha!!! Ujinga mtupu.
 
Tatizo vijana mapenzi yanawasumbua sana, oeni acheni uzinzi mtu anaongea anasalitiwa utafikiri ni mkeo huna aki ya kisheria kumsema chochote unamlalamikia mtu hata uchumba nae huna!
Kwahiyo akimuoa ndio huyo mwanamke atatulia.

Wewe jamaa kuna tusi kubwa sana nimekutukana kimoyo moyo nahisi nikiliandika hapa ntapigwa ban ya maisha [emoji848][emoji848][emoji848]. Acha nikae kimya tu!!!
 
Achana nae kiroho Safi tu mwanangu, atakuua huyo.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Pole sana Mkuu, mwanamke mjinga anaweza kukuvuruga, wakaingia ndugu na ukoo wakavurugwa, akaenda kwenye vyombo vya sheria akawavuruga kisha anakaa chumbani kuwacheka.

Na huyu alieleta uzi nadhani kayatimba timba timba..timbaaa (in diamond platnum voice)
 
Mbona hujamalizia, ulimuomba msamaha? Au uliendelea nae?
 
Jambo la ajabu kuhusu wanawake wa hivyo, huwa wanaona ni kawaida tu yani. Not a big deal to have all the people around
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…