TANZIA Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha ndugu yetu Mtanzania mwezetu Michael a.k.a Mike kilichotokea Afrika Kusini

TANZIA Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha ndugu yetu Mtanzania mwezetu Michael a.k.a Mike kilichotokea Afrika Kusini

Tamaa, uchu, chuki, husuda, ni mambo yakiutawala moyo wako ubinadamu lazima ukutoke na ufanye mambo ya ajabu mpaka binadamu wenzako tukushangae. Roho ya marehe ipate pumziko la milele apumzike kwa amani Amina.
 
Bora ukutane na mnyama kuliko binadamu; sijui walikuwa wanamaanisha nini kwenye huu msemo.
 
Anaandika Mohamed Msangi, Mtanzania anayeishi SA
__________
Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha ndugu yetu, Mtanzania mwezetu Michael aka Mike mzaliwa wa Kinondoni. Mwaka 1999 Mike alihamisha makazi yake kutoka Tanzania kuelekea Mozambique akijishughulisha na biashara mbalimbali zikiwemo za magari na electronics.

Alifanya biashara na Mtanzania mwezetu wa kuitwa Misheli, aliyekua anaishi Johannesburg SA maeneo ya MyFay. Mike na Misheli wamesoma pamoja shule ya msingi Kumbukumbu, Kinondoni, na Mike ndiye aliyemsaidia Misheli kuja SA.

Katika biashara zake Mike alikuwa akimdai mishali pesa, lakini Misheli alishindwa kulipa kwa muda mrefu, ikabidi amwambie Mike amfate South Africa ili ampe gari wamalizane. Mike akakubali. Akatoka Mozambique na kufika South Africa na wakakutana na Misheli.

Wakakabidhiana gari na kumaliza deni. Lakini baada ya muda mchache Mike hakupatikana tena kwenye simu. Baadhi ya Watanzania tunaoishi SA tulikua na miadi ya kukutana nae kabla hajarudi Mozambique. Tulipompigia mchana alisema yuko na Misheli lakini baadae akawa hapatikani. Tulipompigia Misheli akasema waameshaachana.

Tukaanza zoezi la kumtafuta hapa Johannesburg. Kwa zaidi ya wiki 1 tulimtafuta bila mafanikio, hadi asubuhi ya tarehe 18/3/2024 tulipoupata mwili wake katika mochwari ya Hilbrow iliyopo Johannesburg. Ripoti inaonesha Mike aliuwawa kwa kupigwa bunduki. Mwili wake ulikutwa Twist/Plain street, jijini Johannesburg tar.11/3/2024.

Mamlaka jijini Johannesburg zilichukua mwili na kuuweka Mochwari hadi tar.18 March tulipoukuta. Polisi wanamshikilia Misheli kwa tuhuma za mauaji ya Mike. Inadaiwa kuwa Misheli alimkabidhi Mike gari halafu akatuma vijana wampige risasi na kumpora gari hiyo wairudishe kwake.

Hivi ndivyo binadamu tulivyokosa utu. Fikiria rafiki yako mmesoma wote shule ya msingi. Anatangulia kwenda nje ya nchi, baadae anakusaidia na wewe uende. Unafika lakini unafanya biashara unakwama, anakukopesha mtaji. Unashindwa kumlipa kwa wakati. Mnakubaliana umpe gari. Baadae unatuma vijana wamuue ili wachukue gari. Huu ni zaidi ya unyama. Halafu tukikutana huko nje mnasema diaspora hatupendani. Tutapendanaje kwa hali hii? Rest easy Mike.!
MAYFAIR
 
Wasubiri uchunguzi ukamilike inawezekana kauliwa na watu wengine tofauti na rafiki yake, SA wahalifu wengi sana
 
Back
Top Bottom