Kwa matamshi haya kuhusiana na uchaguzi mdogo huko Zanzibar, Makamu wa Raisi Zanzibar kutoka ACT-Wazalenido kujiuzulu wakati wowote?

Tukiwaachia tu na wao hawaaminiani, Pemba itakuwa nchi huru pia Unguja nayo, sasa hayo yoote ya nini?
 
Kitu ambacho sipendi ni muungano kuvunjika. Utawasikia baadhi wanaomba msaada na kulalamika kwa nchi za Ulaya ambazo nazo zimeungana. Ujerumani, Uingereza, Marekani bila kuungana zingekuwa na uwezo mdogo kuliko sasa
Muungano wao utaulinganisha na huu wa kwetu?, ambayo kiongozi wa huko lazima achaguliwe toka bara, usilinganishe muungano wa huko, na muungano huu wa ajabu ajabu tu.
 
Tukiwaachia tu na wao hawaaminiani, Pemba itakuwa nchi huru pia Unguja nayo, sasa hayo yoote ya nini?
Neno "tukiwaachia" halipendezi maana lina maanisha kuwa ni matakwa yetu ndio yenye umuhimu kuliko ya raia wa Unguja na Pemba.
Kwani kuna ubaya gani kama hicho ndicho wanachokitaka? Hiyo ni heri kuliko Tanganyikakuweka majeshi yake huko kuwalazimisha wakae pamoja.


Amandla...
 
Muungano wa Tanzania hauna tija kwa pande zote 2.
Pande zote 2 hazitaki Muungano. ZNZ wanasema tunawakalia kimabavu na tunawachelewesha kupata maendeleo yao wakati Tanganyika wanadai wanabeba gharama za kuiendesha Serikali ya ZNZ.

Muungano umefeli upigwe chini tu kama miungano mingine tu duniani mfano USSR, Yugoslavia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…