Kwa matatizo ya gari

Naomba kujua Kati ya Rav4 old model 1998CC na Harrier old model 2160CC,nini changamoto ya kila gari, uimara,upatikanji wa vipuri,comfortability, fuel, na Kama ungepewa kuchagua unge opt ipi?
 
Shukran kwa majibu yako mazuri Mkuu,nna swali kidogo nna gari yenye engen ya 7A_FE huwa ninaifanyia service kila baada ya km 3000 na natumia oil ya bp gastrol ila nimegundua oil imepungua kidogo kama robo sijajua tatizo haina leakage,na nimezidisha km kama 700 je yaweza kuwa sababu lkn kabla nilitembea km 900 safari ndefu je yaweza changia?gari haitoi moshi ni Maji kwenye exhaust iwe asbh na kutwa nzima na nguvu ipo je shida ni nini?asante.
 
MKUU Nina passo inagonga sana taili za mbele kwenye rough road nimebadirisha ball joint na shorkup wapi tatizo linaendelea utakuwa tatizo ni nini?
 
Naomba unipe ABC ya Toyota prius, kama hapa bongo zipo, na changamoto zake
 
VP bw relis,
Kwanza pole kw kukawia kujibu swali, pia asante sana kw swali zuri.
Upungufu ulioona ni sababu ya oili - au kimimini kwenye oili, kuchemka hadi kuhepa (evaporate). Hili huwa na hatari kubwa kwa mfumo kwani oili iliyobaki ni nzito na yenye chembechembe za carbon.
Magari ya kisasa hupata joto kubwa kwa engine kw kawaida na kwa hivyo hutumia oili za synthetic zinazostahimili joto na pia zina ubora na huduma ndefu - kilometa elfu 7 hadi 10.
 
MKUU Nina passo inagonga sana taili za mbele kwenye rough road nimebadirisha ball joint na shorkup wapi tatizo linaendelea utakuwa tatizo ni nini?
Hebu angalia bushes za arm za chini
 
Shukran mkuu kwa ushauri ila sijaulewa vzr ktk hilo nililouliza na ukanijibu,nilichoelewa kama zipo oil nyingine tofauti na na ninayotumia ambazo hazievaporate je ni zipi au unanishauri nitumie aina gani ya oil ambayo no bora zaidi ya niitumiayo(gastrol Bp) shukran
 
Oili za synthetic kama vile Total Quartz 9000, Mobil 1, Shell Ultra na zinginezo ndio mwafaka na mitambo ya kisasa.
Naamini hapa Bongo katika sheli za Total pekee ndio kuna uwezekano mkubwa wa kupata Total Quartz 9000, maduka ya spea kw kawaida hayaweki bidhaa hii.
 
Nina shida kidogo kwenye gari yangu aina Mazda demio... kuna wakat nakuta kama unga mweupe umeganda kwenye battery(terminal). Sijajua hasa tatizo nini. Naomba mnijuze
Shukran
Slimmyweezy, vipi mkuu, smhni kw kuchelewa kujibu swali lako.

Unga unaopata kw terminal ni aina ya chumvi itokanayo na umeme kwenye chuma, yaani reaction flani. Unga/chumvi hii inaadhiri pale izuiapo umeme kupita, ina weka insulation kati ya battery terminal na ile connector/terminal ya wiring.
Kuepukana na tatizo hili, osha pale na maji tele au pia miminia soda ya coke na suza na maji. Kisha chukua mafuta ya kujipaka kama vaseline (NA SIO grease) na paka ile terminal na uifinike vizuri lakini sio kupindikia.
 
Naomba unisaidie system charge ya Gali ndogo Mimi ni mwanafunzi wa umeme wa magari madogo mwaka wa kwanza
Niaje devo,
Nakuelewa kabisa dogo! Pia mimi charging system iliniweka tension mbaya.
Ikalie chini poa na uelewe pale kuna circuit kadhaa, kw mfn control, charging na field.
 
Msaada, toyota wish cc1780 imeanza kula mafita. pia nikitaka kwenda speed zaidi ya 80 inatetemeka na kuvuma. sijui itakuwa na tatizo gani
Mambo Ilogelo,
Kunywa mafuta, anzia na engine, na uweke oil ya synthetic tafadhali, plugs na filter genuine pia kisha nieleze kuendavyo!
Kuvuma kw kasi zaidi ya 80km/hr, cheki wheel balance, computerized alignment, tie-rod ends na ball joints. Zitakua/kutakua na kasoro kw moja ya hizi, rekebisha na genuine part na sio kufinya ball joints au kupuuza alignment ya computer. You'll see a difference!
 
Habar mkuu, naomba darasa kwa gar Noah box watoto wa mjin huita ila c voxy nina mwezi tangu ninue. Ahsante
Jambo Mabala family,
Unapata ugumu upi na gari hii? Kama ni matunzo/ maintenance, tumia oil ya synthetic pekee na filters genuine. Lingine tu ni kuitumia kw care.
 
Naomba msaada wa toyota nadia, inakunywa sana mafuta, inakuwa mzito kuondoka na kuchanganya na inachelewa kubadili gear, pia ukiweka gear ya kuondoka huwa kama inajikita kidogo ...
Fatilia service hapa. Tumia oil ya synthetic, ATF ya Toyota na hakikisha filters ni genuine. Usisahau spark plugs!
 
Vipi Chilubi,
Pole sana kw kero hilo la battery. Nina uhakika problem ni battery. Weka battery ya Chloride Exide kisha nambie matokeo.
 
Aliosema mkuu hapo ni kweli, diagnosis ndio la kwanza katika urekebishaji na utunzaji was gari kw kua hii ndio njia ya kuwasiliana na mifumo.
Tatizo na vifaa vinavyotumika kw kawaida havina uwezo wa kuwasiliana kamili. Tafuta fundi mwenye mfumo wa Techstream!
 
Jambo Mabala family,
Unapata ugumu upi na gari hii? Kama ni matunzo/ maintenance, tumia oil ya synthetic pekee na filters genuine. Lingine tu ni kuitumia kw care.
Asante mkuu nimekupata, kwenye swala la service nazingatia sana kwa kila 3000 km lazima nimwone fundi na matengenezo madogo madogo. Vp katika matumizi ya mafuta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…