Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukran kwa majibu yako mazuri Mkuu,nna swali kidogo nna gari yenye engen ya 7A_FE huwa ninaifanyia service kila baada ya km 3000 na natumia oil ya bp gastrol ila nimegundua oil imepungua kidogo kama robo sijajua tatizo haina leakage,na nimezidisha km kama 700 je yaweza kuwa sababu lkn kabla nilitembea km 900 safari ndefu je yaweza changia?gari haitoi moshi ni Maji kwenye exhaust iwe asbh na kutwa nzima na nguvu ipo je shida ni nini?asante.Habari za masiku wanaJF,
Kwa mda flani sasa nimekua nikifatilia swala la matatizo ya magari, na vyombo vya moto kwa jumla hapa, kwa sababu za kutoa ushauri - sio kw malipo, na pia huduma - kw mapatano.
Hapa naanzia uzi wa kutoa msaada wa mawaidha, utakavyofanya au fatilia tatizo ili uelewe utakavyotatua na kujibu maswali yoyote kuhusu ufundi wa magari na vyombo vya moto.
Napendekeza kuweka issue/tatizo hapa kwa forum ili wengine waeze kusaidika ILA kuna mambo yatabidi tuyagange nyuma ya pazia.
So, karibuni nyote.
VP bw relis,Shukran kwa majibu yako mazuri Mkuu,nna swali kidogo nna gari yenye engen ya 7A_FE huwa ninaifanyia service kila baada ya km 3000 na natumia oil ya bp gastrol ila nimegundua oil imepungua kidogo kama robo sijajua tatizo haina leakage,na nimezidisha km kama 700 je yaweza kuwa sababu lkn kabla nilitembea km 900 safari ndefu je yaweza changia?gari haitoi moshi ni Maji kwenye exhaust iwe asbh na kutwa nzima na nguvu ipo je shida ni nini?asante.
Acha utaniSory mr mkuzi coka ya baridi au yamoto.
Nnamaana kubwa tuu kuuliza hivi na pia haijausiana na utani.Acha utani
OK sawa mkuu nimekuelewaNnamaana kubwa tuu kuuliza hivi na pia haijausiana na utani.
Shukran mkuu kwa ushauri ila sijaulewa vzr ktk hilo nililouliza na ukanijibu,nilichoelewa kama zipo oil nyingine tofauti na na ninayotumia ambazo hazievaporate je ni zipi au unanishauri nitumie aina gani ya oil ambayo no bora zaidi ya niitumiayo(gastrol Bp) shukranVP bw relis,
Kwanza pole kw kukawia kujibu swali, pia asante sana kw swali zuri.
Upungufu ulioona ni sababu ya oili - au kimimini kwenye oili, kuchemka hadi kuhepa (evaporate). Hili huwa na hatari kubwa kwa mfumo kwani oili iliyobaki ni nzito na yenye chembechembe za carbon.
Magari ya kisasa hupata joto kubwa kwa engine kw kawaida na kwa hivyo hutumia oili za synthetic zinazostahimili joto na pia zina ubora na huduma ndefu - kilometa elfu 7 hadi 10.
Oili za synthetic kama vile Total Quartz 9000, Mobil 1, Shell Ultra na zinginezo ndio mwafaka na mitambo ya kisasa.Shukran mkuu kwa ushauri ila sijaulewa vzr ktk hilo nililouliza na ukanijibu,nilichoelewa kama zipo oil nyingine tofauti na na ninayotumia ambazo hazievaporate je ni zipi au unanishauri nitumie aina gani ya oil ambayo no bora zaidi ya niitumiayo(gastrol Bp) shukran
Slimmyweezy, vipi mkuu, smhni kw kuchelewa kujibu swali lako.Nina shida kidogo kwenye gari yangu aina Mazda demio... kuna wakat nakuta kama unga mweupe umeganda kwenye battery(terminal). Sijajua hasa tatizo nini. Naomba mnijuze
Shukran
Niaje devo,Naomba unisaidie system charge ya Gali ndogo Mimi ni mwanafunzi wa umeme wa magari madogo mwaka wa kwanza
Mambo Ilogelo,Msaada, toyota wish cc1780 imeanza kula mafita. pia nikitaka kwenda speed zaidi ya 80 inatetemeka na kuvuma. sijui itakuwa na tatizo gani
Jambo Mabala family,Habar mkuu, naomba darasa kwa gar Noah box watoto wa mjin huita ila c voxy nina mwezi tangu ninue. Ahsante
Fatilia service hapa. Tumia oil ya synthetic, ATF ya Toyota na hakikisha filters ni genuine. Usisahau spark plugs!Naomba msaada wa toyota nadia, inakunywa sana mafuta, inakuwa mzito kuondoka na kuchanganya na inachelewa kubadili gear, pia ukiweka gear ya kuondoka huwa kama inajikita kidogo ...
Vipi Chilubi,Mimi naomba kusaidiwa kitu kimoja ambacho sasa katika gari kimekuwa kinanikera sana.
Tatizo ni battery kudrain bila ya chochote kuwa kinafanya kazi.
Battery indicator inaonesha green. Alternator ina charge battery.
Asubuhi niliamka kutaka kwenda kazini gari ikagoma, nikapandishia battery mnyama kawaka. Nikafunga safari ambayo ni kama lisaa moja ivi, battery guage kwenye dashboard inaonesha iko powa tu. nikasimamishwa na askari, walitaka mashirikiano nikawapa. Nikaingiza gari kituoni, nikaizima kwa ajili ya kwenda kuwapa mashirikiano. baada ya kumaliza hata dakika 5 hazikufika, nawasha gari imegoma kabisa. ikabidi niite msaada kuja kuboost.
Sasa sifahamu kama ndio battery imekwisha (haijafika hata miaka miwala hii battery na bado indicator inaonesha green). Alternator tumeijaribu, nayo inafanya kazi vizuri, maana kawaida ukichomoa battery kama alternator mbovu basi gari itakata moto, au kama umeweka battery basi ile battery itanyonywa yote na gari kukata moto. Nimehakikisha hakuna kitu kinachokaa wazi hata kimoja.
Mwenye kujua wapi pa kuanzia anifahamishe... Mi nahisi ni battery, lakini kama battery kufa kwanini bado inaonesha green indicator kuwa bado ipo good.
Aliosema mkuu hapo ni kweli, diagnosis ndio la kwanza katika urekebishaji na utunzaji was gari kw kua hii ndio njia ya kuwasiliana na mifumo.Niligharamika sana kwa tatizo kama hilo kwa kudharau kufanya engine diagnosis, ilipeleka mpaka engine ku knock, tangu natafuta mzizi wa tatizo mpaka knock zimenitoka hela nyingi sana ambazo ningeweza ata kupachika new engine tu tena ilokuwa powerful kuliko ya mwanzo. Kumbe tatizo lilikuwa oxygen sensor tu. sasa mkuu nakushauri peleka gari ikafanyiwe diagnosis tu.... Haya mambo ikiwaka check engine ikiwaka eti fundi anakwambia ufanye service ni uzushi tu.
Asante mkuu nimekupata, kwenye swala la service nazingatia sana kwa kila 3000 km lazima nimwone fundi na matengenezo madogo madogo. Vp katika matumizi ya mafuta?Jambo Mabala family,
Unapata ugumu upi na gari hii? Kama ni matunzo/ maintenance, tumia oil ya synthetic pekee na filters genuine. Lingine tu ni kuitumia kw care.