Synthetic - iliyotengezwa na binadam, ina maana oili imetengenezwa kw kutumia kemikali zilizobuniwa maabarani na kua na uwezo mkubwa wa kuhimili joto na hali zinginezo mle ndani ya engine.
Utapata dum ya mafuta imeandikwa 1. Mineral oil: mafuta asilia ya petroli (petroleum oil) 2. Monograde oil: mafuta asilia ya petroli lakini yakiwa yameboreshwa kuhimili hali flani ya utendakazi 3. Multigrade oil: mafuta ya asilia yakiwa yameboreshwa kuhimili hali kadhaa tofauti za utendakazi 4. Semi-synthetic oil: mafuta ya asilia lakini yameongezwa kemikali au mafuta yaliotengenezwa na binadam na yenye ubora wa juu zaidi kuhimili hali za engine 5. Synthetic au Fully Synthetic oil: mafuta yasiotengenezwa au kua na mafuta asilia ndani yake.
Ukifika sheli, angalia paki ilivyoandikwa pale nyuma; ishara nyingine ni kilometa hadi service hua kw kawaida ni zaidi ya elfu saba.