Kwa matatizo ya gari

Kwa matatizo ya gari

Vipi Chilubi,
Pole sana kw kero hilo la battery. Nina uhakika problem ni battery. Weka battery ya Chloride Exide kisha nambie matokeo.
Hizo battery zipo ambazo ni mantainance free? Maana nina tatizo hilo la c kwa kiwango hicho
 
Nina Toyota IST cc 1290 nataka kujua kama kuna madhara yoyote ya kwenda nayo masafa marefu mara kwa mara yaani kila baada ya miezi miwili ama mitatu. Asante
 
Hakuna madhara yeyote.
 
Naombeni msaada gari yangu ilikua na tatizo la mis fundi akaniambia shida ni plug baada ya kuweka mpya kweli gari ikakaa sawa lkn baada ya lisaa limoja tatizo tena la misi likajitokeza kuangalia plung ni nyeusi kabisa tiiii zinaonesha hazichomi tena mafuta naombeni ushauri nifanyeje ili plug ziwe zinachoma??
 
Zilkua na harufu/unyevu wa petroli au ni oili?
 
Oili za synthetic kama vile Total Quartz 9000, Mobil 1, Shell Ultra na zinginezo ndio mwafaka na mitambo ya kisasa.
Naamini hapa Bongo katika sheli za Total pekee ndio kuna uwezekano mkubwa wa kupata Total Quartz 9000, maduka ya spea kw kawaida hayaweki bidhaa hii.
Shukran Mkuu nilibadili Jana ngoja niitazamie japo km 5000 ntaleta mrejesho,pia niliambiwa zipo bp castrol zenye kutembea km 7000 je material ni sawa yaani zina hiyo sythetic
 
Naomba kujua gari za Toyota isiyozid CC 1800 inayofaa kwa mazingira ya Barabara za vumbi
 
Shukran Mkuu nilibadili Jana ngoja niitazamie japo km 5000 ntaleta mrejesho,pia niliambiwa zipo bp castrol zenye kutembea km 7000 je material ni sawa yaani zina hiyo sythetic
Synthetic - iliyotengezwa na binadam, ina maana oili imetengenezwa kw kutumia kemikali zilizobuniwa maabarani na kua na uwezo mkubwa wa kuhimili joto na hali zinginezo mle ndani ya engine.
Utapata dum ya mafuta imeandikwa 1. Mineral oil: mafuta asilia ya petroli (petroleum oil) 2. Monograde oil: mafuta asilia ya petroli lakini yakiwa yameboreshwa kuhimili hali flani ya utendakazi 3. Multigrade oil: mafuta ya asilia yakiwa yameboreshwa kuhimili hali kadhaa tofauti za utendakazi 4. Semi-synthetic oil: mafuta ya asilia lakini yameongezwa kemikali au mafuta yaliotengenezwa na binadam na yenye ubora wa juu zaidi kuhimili hali za engine 5. Synthetic au Fully Synthetic oil: mafuta yasiotengenezwa au kua na mafuta asilia ndani yake.
Ukifika sheli, angalia paki ilivyoandikwa pale nyuma; ishara nyingine ni kilometa hadi service hua kw kawaida ni zaidi ya elfu saba.
 
Pia naamini ndani ya wiki moja utakua umeshaona tofauti.
 
Shukran Mkuu huu Uzi inabidi mod wautendee haki unajibu kitaalamu maana hata wenye pijo za urithi wakipata maelekezo hapa zitaamka,narudi Mkuu kwa maswali mengine usinichoke.
 
Asante Bw Relis.
Nayakaribisha maswali, nia yangu kama fundi ni kumsaidia ndugu yangu kuzielewa machine na mifumo yake na sio kulinda 'siri'! Au vipi?
 
Shukran Mkuu ningependa kujua ni aina gani ya mafuta ya breki yanayofaa kwa gari zetu,wengine wanasema dot 4 wengine 3 ila sijajua kama yapo 2 na 1,je mazuri ni yapi kwa maisha ya vyombo vyetu? Maana nasikia mengine ukitumia yanaua raba zilizopo kwenye system ya breki ni kweli,shukran.
 
Muunda gari/chombo hua ameandika kwenye owner/operator manual au/na kwenye mfuniko wa chupa pale kw master cylinder. Ni muhimu kuzingatia
 
Habari Mkuu,
Nina IST ina tatizo la kusitasita ikifikia kati ya speed 60 na 90 ikiwa chini ya 60 au zaidi ya 90 inakwenda vizuri. Naomba unifahamishe tatizo lake na ufumbuzi.
Thanks
 
Habari, nina gari rav 4 yenye engine 3s ina tatizo la kutokuwa na nguvu kabisa milimani nimebadili engine oil na transmission (gearbox) oil but problem ipo palepale, msaada wako tafadhali
 
Mkuu.mimi gari yangu nikiwa nadrive after some time inatoa harufu kama ya kitu kinaungua kwenye vent za ac! Tatizo laweza kuwa nini!!!?
 
Back
Top Bottom