Kwa matatizo ya gari

Mkuu mimi engine yangu ni 1mz V6,nimeambiwa sensor zilizopo kwenye hicho kifaa zimekufa,nipo tabora naomba msaada wako ni wapi naweza pata ufumbuzi wa tatizo hili.....ASANYEView attachment 736061View attachment 736063
Bro, hapo hakuna sensor ila vacuum switch. Sio vifaa vyote viingiazo wire ni sensor. Hizo kw picha ni solenoid switch za kufunga/fungulia upepo/vacuum. Hua zinazingua mafundi kuziregesha kwani ukichanganya hizo pipe gari linachanganyikiwa pia!

Tupatane PM nikuelezee utakvyo fanya kubaini shida na hata kuitatua! Kwa malipo, ufahamu mapema!
 
Asante sana mkuu,nimeshakufuata PM
 
Nashukuru Mkuu toka nilipobadili mpaka Leo nimetembea kilomita zaidi ya buku naona haijapungua na utofauti ni mkubwa tofauti na ili niliyoitumia kabla ingeonesha utofauti Wa kupungua kidogo.
Mkuu nimerudi tena kuleta mrejesho,juzi nilitimiza km 10000 engen oil niliongezea litre 1 na bado nilipofanya service oil imepungua maana nimetoa kama litre 3 na nusu,bado napata shida ni lingi zimekufa au,nikiwasha asbh baada ya dkk 5 mvuke unatoka na gari bado ina compression kama mpya leakage ndogondogo sana msaada tafadhari.
 
Mark ii balloon kutetemeka ikiwa kwenye silencer hatimae kuzima na kuishiwa nguvu hasa kwenye mlima tatizo ni nini?
 
Nataka ku-over all engen ya ALTEZZA 4 cylinder....maswali yangu
-je kuna uwezekano wa kupata hiyo engene
-Na kuna matatizo yoyote kama nitareplace hyo engen??
 
Nataka ku-over all engen ya ALTEZZA 4 cylinder....maswali yangu
-je kuna uwezekano wa kupata hiyo engene
-Na kuna matatizo yoyote kama nitareplace hyo engen??
Engine yapatikana rahisi na wala hakuna matatizo yeyote.

Sent from my Infinix-X600 using Tapatalk
 
Styvo254 Habari mkuu
Ninaomba Ushauri juu ya Gari Toyota Verosa,kwasababu ni Gari ninayoipenda sana.

Natanguliza shukrani
 
Mkuu nina gari Hyundai Santa Fe ya diesel manual 2006 kuna kipindi Fundi alichomoa terminal kwenye betri Wakati Funguo zikiwa kwenye switch tangu siku hiyo hiyo gari haijawai waka Nimehangaika na mafundi wa kila aina na bado sijafanikiwa nipo Dar tegeta msaaada please

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Styvo254 Habari mkuu
Ninaomba Ushauri juu ya Gari Toyota Verosa,kwasababu ni Gari ninayoipenda sana.

Natanguliza shukrani
Asante kw swali

Verossa ni gari nzuri sana ya luxury class - yaani ya hali ya juu ya starehe. Muhimu kabisa, kama kw magari yote, ni kuzingatia service, spare na matunzo yake vizuri. Kw matatizo, haina udhaifu ila yahitaji fundi muelewa.

Sent from my Infinix-X600 using Tapatalk
 
Ufunguo wako ni Electronic Key na yaonekana umepoteza mawasiliano na ignition switch yake. Hili lilisababishwa na kukatika kw moto ufunguo ukiwa bado kw switch, mwiko sana kw mifumo hii.

Nifate pm ilitujadili suluhu zaidi

Sent from my Infinix-X600 using Tapatalk
 
Mkuu msaada, niko mbioni kuvuta Carina Ti, naomba kufaham udhaifu wake na precautions.
Asante.
 
Mkuu styvo umenipita hapa bila ushauri lkn niliexperience inapungua zaidi km @1600 tokea kuweka oil mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu styvo umenipita hapa bila ushauri lkn niliexperience inapungua zaidi km @1600 tokea kuweka oil mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi mkuu,
Pole kw kukupita bila neno.

Yaonekana leakage na ring ndio zapunguza oili yako. Fanya engine wash ya nguvu ili kuziona leakage kisha mzishughulikie.

Sent from my Infinix-X600 using Tapatalk
 
Mkuu msaada, niko mbioni kuvuta Carina Ti, naomba kufaham udhaifu wake na precautions.
Asante.
Carina Ti haina issue kibao wala utata sana kama wazielewa injection.

Sent from my Infinix-X600 using Tapatalk
 
Mkuu styvo254,kwanza nikupongeze kwa darsa zuri. Kiukweli uko vizuri sana. Elimu yako imetusaidia sana.
Kuna magari mawili mimi nataka kufanya option. Magari hayo siyo kampuni ya Toyota bali ni nje kabisa. Moja ni la kijerumani aina ya VW Touran na lingine ni Subaru Forester angalau la mwaka 2006 na kuzidi 2008.
Naomba kama ukiwa na data,unipe wasifu wa magari hayo mawili,je spea zipo au ni pasua kichwa? Na kama zipo,je kuna mafundi na garage ambazo zina mafundi kuweza kutatua kama dash board ikionyesha hitilafu. Na hapa wasiwasi wangu mkubwa ni hilo VW Touran,kuna mafundi kweli?

Nashukuru kama utanipa A,B,C za hayo magari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother wewe ni fundi!
Mungu akupe maisha marefu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Subaru na VW ni waundaji magari shupavu sana na magari yao yamethibitisha hili mara kw mara. Advantage moja ya Subaru ni haina spare parts gushi/fake! VW pia wanaongoza kw uzinduzi wa teknolojia mpya kama vile DSG transmission na engine zao.
Cha muhimu sana kw haya magari ni kuzingatia service na kuweka spare zinazofaa. Kw kua gari zenyewe sio dhaifu, usiwe na wasiwasi kuhusu fundi sababu service za kawaida sio tatizo kubwa. Mambo ya diagnosis na mifumo ya engine na transmission haiwi na shida mara kw mara.

Sent from my Infinix-X600 using Tapatalk
 
Ahsante sana mkuu kwa kunitia moyo. So kwa maoni yako,kipekee kati ya VW Touran na Subaru Forester,unanishauri nichukue ipi?(just kwa mtazamo wako tu na maoni,other factors being kept constant)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…