Kwa matatizo ya gari

Kwa matatizo ya gari

Gari yangu ni aina ya premio old model inaniwashia alama ya check engine nimepeleka kwa mafundi lkn hiyo alama haitoki na kupelekea gari kuwa na mis msaada
Vipi kaka
Unahitaji kufanyiwa diagnosis vizuri ili kuisoma hiyo code iliyoashiriwa na taa. Karibu umtafute fundi ana Techstream au uende kw Toyota Tanzania waifanyie diagnosis.
 
Mkuu kwanza nikushukuru kwa elimu unayoitoa jukwaani hapa. Tatizo langu ni kuchelewa kuchanganya kwa gari yangu aina ya toyota nadia, ukitoka inakua nzito then baada ya muda kidogo inakaa sawa. Tatizo lingine kuna wakati inakua inavuma. Msaada wako mkuu
 
Mkuu kwanza nikushukuru kwa elimu unayoitoa jukwaani hapa. Tatizo langu ni kuchelewa kuchanganya kwa gari yangu aina ya toyota nadia, ukitoka inakua nzito then baada ya muda kidogo inakaa sawa. Tatizo lingine kuna wakati inakua inavuma. Msaada wako mkuu
Asante sana kw swali.

Mfumo wa automatic transmission waeza kua na matatizo aitha ya mafuta/mskumo(pressure) au mechanical. Itabidi ifanyiwe diagnosis ili kujua what's what!
 
mm nauliza hivi engen ukiifanyia ovarall inaweza kwenda mbali.mfano dar to mwanza
Ikiwa imefanyiwa overhaul inavyofaa na kwa kutumia spare na vitu sawa, yafaa kwenda hadi iishe tena au kwa umbali kama ilivyoenda ikiwa mpya
 
Nina shida kidogo kwenye gari yangu aina Mazda demio... kuna wakat nakuta kama unga mweupe umeganda kwenye battery(terminal). Sijajua hasa tatizo nini. Naomba mnijuze
Shukran
 
Nina shida kidogo kwenye gari yangu aina Mazda demio... kuna wakat nakuta kama unga mweupe umeganda kwenye battery(terminal). Sijajua hasa tatizo nini. Naomba mnijuze
Shukran
chukua cocacola mwagia hizo terminal wakati gari ipo off engine
 
Naomba unisaidie system charge ya Gali ndogo Mimi ni mwanafunzi wa umeme wa magari madogo mwaka wa kwanza
 
Msaada, toyota wish cc1780 imeanza kula mafita. pia nikitaka kwenda speed zaidi ya 80 inatetemeka na kuvuma. sijui itakuwa na tatizo gani
 
Habar mkuu, naomba darasa kwa gar Noah box watoto wa mjin huita ila c voxy nina mwezi tangu ninue. Ahsante
 
Msaada, toyota wish cc1780 imeanza kula mafita. pia nikitaka kwenda speed zaidi ya 80 inatetemeka na kuvuma. sijui itakuwa na tatizo gani
Check engine oil kama iko sawa. Mara nyingi Gari ikitetemeka ingini unakuta oil imepingua
 
Habari za masiku wanaJF,
Kwa mda flani sasa nimekua nikifatilia swala la matatizo ya magari, na vyombo vya moto kwa jumla hapa, kwa sababu za kutoa ushauri - sio kw malipo, na pia huduma - kw mapatano.
Hapa naanzia uzi wa kutoa msaada wa mawaidha, utakavyofanya au fatilia tatizo ili uelewe utakavyotatua na kujibu maswali yoyote kuhusu ufundi wa magari na vyombo vya moto.
Napendekeza kuweka issue/tatizo hapa kwa forum ili wengine waeze kusaidika ILA kuna mambo yatabidi tuyagange nyuma ya pazia.
So, karibuni nyote.
Naomba msaada wa toyota nadia, inakunywa sana mafuta, inakuwa mzito kuondoka na kuchanganya na inachelewa kubadili gear, pia ukiweka gear ya kuondoka huwa kama inajikita kidogo ...
 
Mimi naomba kusaidiwa kitu kimoja ambacho sasa katika gari kimekuwa kinanikera sana.

Tatizo ni battery kudrain bila ya chochote kuwa kinafanya kazi.

Battery indicator inaonesha green. Alternator ina charge battery.

Asubuhi niliamka kutaka kwenda kazini gari ikagoma, nikapandishia battery mnyama kawaka. Nikafunga safari ambayo ni kama lisaa moja ivi, battery guage kwenye dashboard inaonesha iko powa tu. nikasimamishwa na askari, walitaka mashirikiano nikawapa. Nikaingiza gari kituoni, nikaizima kwa ajili ya kwenda kuwapa mashirikiano. baada ya kumaliza hata dakika 5 hazikufika, nawasha gari imegoma kabisa. ikabidi niite msaada kuja kuboost.

Sasa sifahamu kama ndio battery imekwisha (haijafika hata miaka miwala hii battery na bado indicator inaonesha green). Alternator tumeijaribu, nayo inafanya kazi vizuri, maana kawaida ukichomoa battery kama alternator mbovu basi gari itakata moto, au kama umeweka battery basi ile battery itanyonywa yote na gari kukata moto. Nimehakikisha hakuna kitu kinachokaa wazi hata kimoja.

Mwenye kujua wapi pa kuanzia anifahamishe... Mi nahisi ni battery, lakini kama battery kufa kwanini bado inaonesha green indicator kuwa bado ipo good.
 
Gari yangu ni aina ya premio old model inaniwashia alama ya check engine nimepeleka kwa mafundi lkn hiyo alama haitoki na kupelekea gari kuwa na mis msaada
Niligharamika sana kwa tatizo kama hilo kwa kudharau kufanya engine diagnosis, ilipeleka mpaka engine ku knock, tangu natafuta mzizi wa tatizo mpaka knock zimenitoka hela nyingi sana ambazo ningeweza ata kupachika new engine tu tena ilokuwa powerful kuliko ya mwanzo. Kumbe tatizo lilikuwa oxygen sensor tu. sasa mkuu nakushauri peleka gari ikafanyiwe diagnosis tu.... Haya mambo ikiwaka check engine ikiwaka eti fundi anakwambia ufanye service ni uzushi tu.
 
Back
Top Bottom