Kama ndoto yake ni kusoma kozi za afya basi kwa haya matokeo yake ni changamoto kidogo kupata kwa level ya degree! Kama anataka MD basi aanzie tu diploma, clinical officer!
Huwa kuna mwongozo wa TCU unaonesha vigezo vyote vya kusoma kozi za degree, kwa hiyo aangalie huo mwongozo nafikiri atapata kozi zingine za afya za degree kulingana na ufaulu wake tofauti na degree ya medicine.
Pia kuna kozi zingine za afya (non clinical medicine) kama health management system nk ambazo wataalamu wake hawahusiki kutibu moja kwa moja lakini hufanya kazi kwenye sekta ya afya.
Kwa sasa kozi za afya zenye uhaba wa wataalamu ni radiology, dental, physiotherapy, occupational therapy nk ambazo kama anapenda achague mojwapo (aangalie vigezo vyao na ufaulu wake). Kwa hiyo kama anataka ajira mapema ni vyema akaangalia hizo pia.
Mwisho nafikiri anaweza akabahatisha baadhi ya kozi za degree hasa kwenye vyuo binafsi,,,, lakini aangalie vigezo vilivyopo kwenye mwongozo wa TCU, TCU guide book ya mwaka huu.
Kila lakheri.