Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Kwakuwa watanzania wengi wajasiriamali bado ni wageni wa masuala ya kifedha na mikopo, sio vibaya tukaelimishana kuhusu huchi kitu. Mazingira ya biashara Tanzania sote twayajua, unaweza lala una biashara ukaamka huna biashara, refer ile case ya masoko kuungua. Au unalala una biashara yako, kesho yake unaamka unakutana na TRA wanasema wanakudai kodi ya malimbikizo bilioni moja au wakati mwingine biashara inafungwa kabisa. Au unasikia account ya benki imefungwa.
Kwa mazingira hatarishi kama hayo kwenye biashara, kuwa na mkopo benki kunatoa kinga kwa mmiliki wa biashara. Mfano kwa suala la majanga kama moto kwenye biashara, ikiwa ulichukua mkopo benki na kununua stocks maana yake kuna kipengele ambacho benki huwa wanaweka, kwamba bidhaa zinakuwa insured na majanga kama moto n.k.
Kwa upande mwingine na wa kuzingatia, biashara yenye mkopo benki sio rahisi sana kupigwa tanji na mamlaka za kodi i.e. kufungwa kwasababu hiyo hatua itakuwa na collateral damage kwenye taasisi za fedha zilizokukopesha. Ila biashara isiyo na mkopo maana yake ni kama binti ambaye ni bikra kwamba anakuwa attractive kwa watu wengi.
Wakati mwngine kama biashara yako ina qualify kupata mkopo wa milioni 200, wewe ichukue tu hiyo hela ukawekeze pembezoni kwenye nyumba au kwenye bonds maana yake inakupa ulinzi mkubwa sana incase kitatokea chochote.
Unakuta mfanyabiashara wa Tanzania anajisifu kutokuwa na mkopo benki, hili sio jambo la kujisifu hata kidogo ndugu zanguni. Nakaribisha michango.
Kwa usaidizi wowote kuhusiana na masuala ya mikopo au ushauri wa kupata mikopo usisite kuwasiliana na mimi. Nina ujuzi mkubwa kwenye haya masuala.
Karibuni.