Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
Oya ni Fujo plus 🤣🤣 mpaka wanauaKama OYA?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Oya ni Fujo plus 🤣🤣 mpaka wanauaKama OYA?
😇😇😅Oya ni Fujo plus 🤣🤣 mpaka wanaua
😀 😀 😀 hapo unajiharibia tu mkuu, kama una mpango wa kukopa benki na hauna dhamana. Wanakuwa wanakujua mkuu endapo jina lakolitatokea katika list ya wadaiwa sugu na kama unatumia vitambulisho vyako ndio unaharibu vizuri.Online nimekopa na nimekinbia na line nimebadili...
Vigezo kwa mkopo mdogo mf 1M?Finca
Tembelea tawi lolote lililo karibu nawe.Vigezo kwa mkopo mdogo mf 1M?
Umenikumbusha juzi kati Kuna mtu kaniambia Jane hutaki mikopo utaishia kutusindikiza tu dah🤣🤣🤣Kwakuwa watanzania wengi wajasiriamali bado ni wageni wa masuala ya kifedha na mikopo, sio vibaya tukaelimishana kuhusu huchi kitu. Mazingira ya biashara Tanzania sote twayajua, unaweza lala una biashara ukaamka huna biashara, refer ile case ya masoko kuungua. Au unalala una biashara yako, kesho yake unaamka unakutana na TRA wanasema wanakudai kodi ya malimbikizo bilioni moja au wakati mwingine biashara inafungwa kabisa. Au unasikia account ya benki imefungwa.
Kwa mazingira hatarishi kama hayo kwenye biashara, kuwa na mkopo benki kunatoa kinga kwa mmiliki wa biashara. Mfano kwa suala la majanga kama moto kwenye biashara, ikiwa ulichukua mkopo benki na kununua stocks maana yake kuna kipengele ambacho benki huwa wanaweka, kwamba bidhaa zinakuwa insured na majanga kama moto n.k.
Kwa upande mwingine na wa kuzingatia, biashara yenye mkopo benki sio rahisi sana kupigwa tanji na mamlaka za kodi i.e. kufungwa kwasababu hiyo hatua itakuwa na collateral damage kwenye taasisi za fedha zilizokukopesha. Ila biashara isiyo na mkopo maana yake ni kama binti ambaye ni bikra kwamba anakuwa attractive kwa watu wengi.
Wakati mwngine kama biashara yako ina qualify kupata mkopo wa milioni 200, wewe ichukue tu hiyo hela ukawekeze pembezoni kwenye nyumba au kwenye bonds maana yake inakupa ulinzi mkubwa sana incase kitatokea chochote.
Unakuta mfanyabiashara wa Tanzania anajisifu kutokuwa na mkopo benki, hili sio jambo la kujisifu hata kidogo ndugu zanguni. Nakaribisha michango.
Kwa usaidizi wowote kuhusiana na masuala ya mikopo au ushauri wa kupata mikopo usisite kuwasiliana na mimi. Nina ujuzi mkubwa kwenye haya masuala.
Karibuni.
SikupingiShida kubwa nadhani hawana advantage kama mabenki kwasababu hawapokei deposits kwa wateja. Kwahiyo likely cost of funds yao ni kubwa kuliko benk nyingine hivo hata mikopo yao itakuwa na riba kubwa
Juzi nimeanda crdb,hela ndogo tuu nilikua nataka ila masharti kibaooooo.Kwenye issue
Kwanza sio mikopo yote itakulazimu kuweka dhamana au sio bank zote wanalazimisha kuweka dhamana. Kuna mikopo mingi tu isiyo na dhamana mfano kuna kitu kinaitwa Invoice Discointing. Hiyo kama ukiwa tayar na mahusiano mazuri na benki na historia ya akaunti yako wanaifahamu labda kwa miaka hata 5 utashangaa unapatiwa mkopo kwa mda mchache.
Shida inakuja mtu kafungua akaunyi benki haina hata mwaka anakuja anataka milioni 100 hapo lazima benki watake kwanza kupata hati ya nyumba ya thamani ya milioni 200.
Ila kwa mteja wa siku nyingi na tayari wanamfahamu, dhamana ni kitu cha mwisho sana sema huwa kinaonekana kuwa cha kwanza