Hakuna lolote, yani kusiwe na ushindani wa kisiasa? Watu kutaka tu kugombea 2020 nayo inaonekana ni sababu ya mtu kujiongezea ulinzi? Watu wasikosoee?
Basi hakuna haja ya demokrasia. Hivi JK alivyokuwa anakosolewa na hata kutaka kupokonywa kiti ndani ya chama na Edo naye angesema aongezewe ulinzi.
Tusidanganyane, tusitafute kichaka cha kijifichia. Tumekwama kama Taifa, mtu kaharibu mambo wazalendo wanaona sasa inatosha hali hii haiwezi kwenda miaka 10. Kujenga ni kazi ngumu na ya muda mrefu kubomoa ni kazi kidogo sana.
Biashara vilio, kilimo huko ni vilio, uchumi hoi, watumishi hoi, mwaka wa tano huu tunazungumzia Stigler na SG ambao mpaka tukope ndio tujisogezee . Nini cha kujivunia kama Taifa?