Kwa mbali nimeanza kuuelewa ulinzi mkali wa Rais...

Hivi Magufuli ulinzi wake ni mkali kushinda wa waliomtangulia?

Ndio na mikwara kibao ya kuwapotezea watu muda pindi msafara wake unapopita. Sio ajabu barabara kufungwa zaidi ya masaa mawili kabla hajapita.
 
Hivi unaamini kuwa hakuna mamluki?
Nakuhakikishia kuwa duniani hakuna usalama wa 100%
Nalog off
 

Sasa hao wastaafu anaweka ulinzi mkali hivyo, je ingekuwa maadui zake ni vijana si angewaleta CIA kabisa?
 
Sasa nimeaza kumuelewa magufuli.watu hii inchi walifanya ya kwao sasa mkuu anataka kuondoa dhana hiyo
Wote wanaopinga hatua anazochukua ni waathirika wa hiki kinachoendelea yaa wanashiriki moves za kumkwamisha
 
Tunahitaji mabadiliko kwa kweli
Nalog off
 

Mimi nadhani tunaposema mtu fulani ni mzalendo basi afunuliwe tuyaone matendo yake. Nani amejenga ikulu kijijini kwake tangia Nyerere mpaka Jk?
Uwanja wa ndege?
Nk
Je hawa wanaoitwa sio wazalendo wameharibu wapi nadhani tuyaweke bayana . Ni wazo tu
 


Usisahau Kikwete aliongezewa ulinzi usionekana na Sheikh Yahaya almaruhumu.


Kwa kauli hizi za baadhi ya wastafu zilizo jaa chuki ya bila kificho ni dhahiri ulinzi wa Rais unahitajika kuimarishwa na kuongezewa ubunifu na mbinu mpya kila wakati. Jamaa wana chuki na kinyongo dhidi yake kwa kumaanisha. The best technique is to identify the persons wanachochea hizo chuki na kumshughulikia mmoja baada ya mwengine kwa njia itayooneka muafaka. Hivyo tu.
 
Kama vipi asitoke ndani ya ikulu na nje ya nchi wasije wakapindua meza
 
Siku hizi ccm imepata watetezi wengi sana kuliko wakosoaji mana wale tuliowategemea kukikosoa hiki chama ndio wamekuwa watetezi hata maovu ya mheshimiwa hawayaoni hasa mleta madalakani hii
 
Hakika tulimuhitaji Rais kama huyu wakuibadilisha Tanzania,pamoja na yote yanayoendelea Mimi nitampambani Rais wangu kwa njia yoyote hata kwa kuvuja damu
Rais wa kuibadili Tanzania au kuibadili chato ,lipeni wastaafu jamani nyie genge la wahuni wa kijani .
 
Sijui kuhusu quantity au quality ya ulinzi lakini visibly ulinzi wa Magufuli unaonekana umezidi sana kwa watangulizi. Sikumbuki kuona watu na bunduki wakiwa na Kikwete
Sikuwahi kuona Kikwete asindikizwe na Chopa juu akiwa anatembea kwa gari ardhini
 
Ulinzi wake unalenga kuwatisha raia zaidi.

Ukitizama kwenye mikutano yake, tofauti iliyopo kati ya wanamsafara na raia ni kubwa mno.

Yeye na msafara wake wapo na mashangingi na ma-AK47 masutizz huku raia ni vilio na malalamiko.

Kwa raia usafiri wao ni miguu yao, chakula ni cha kubangaiza, pesa ndio usiseme, elfu 20 kwa mwaka inasababisha vilio kila mahali....

Kwa hali hiyo anayoiona huko anakopita ni lazima apate hofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…