Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

You wishes. Thank you for sharing your dreams
Wakati Magu anaingia ndio nimeanza biashara ninayoifanya nilikuwa na kafremu kamoja. Sasa hivi nimechukua fremu nne, nimejenga nyumba moja, ya pili namalizia, nimenunua gari ya pili January. December nimeenda vacation wiki moja Dubai. Labda inawezekana ingekuwa awamu iliopita ningepata mafanikio zaidi ya hayo.
 
Kasema ndinga kali. Ukiwa na 2017 Land Cruiser V8 unaweza kuwa masikini? Masikini utumie 300m kununua gari? Kuna gari kuwa na uwezo wa kuinunua lazima uwe tajiri achana na viusafiri vyetu akina sisi.
2017 Land cruiser V8 siyo matako kila mtu awe nayo.
 
Sasa kwa mfano alioutoa hapo juu kwamba watu wana magari huko kwenye halmashauri haiwezekani wakawa na aina hiyo ya gari .wengi ni hizo Toyota salon used kutoka Japan
Nimeandika hio ujue kuwa KUNA GARI LAZIMA UWE TAJIRI ndio umiliki. Mkuu una stress sana sio? Mbona jazba hivyo? Relax.
 
Miaka 18 kwenye biashara umezeeka ,huwezi mbinu mpya waachie vijana..

Ni ngumu sana kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea ukweli mtupu Biashara za sasa hivi zinaitaji noreji na visheni mpya.

Kwa miaka hiyo 18 umekwepa sana kodi hivyo ni lazima Awamu hii upigike.

Au unashindwa kwenda na kasi hii ya Dunia ya leo ndio maana ngozi nyeupe wanafundisha watoto wao

Na watoto wao wanakuja na New vision kwa kizazi husika.. Unafikiri Baba yake MO ni mjinga kukaa pembeni? Ipo siku watoto wako watamsikia Mtoto wa MO

Biashara ina njia zake na Elimu yake na sio mazoea Kama ngozi nyeusi tunavyo fikiria.

Serikali inatengeneza beat swala la mpangilio wa sauti na hisia za mziki ni wewe.

Awamu ya tano ukishindwa ni wewe usitafute wa kumlaumu.

Ngoja nile bangi kwanza ili nipate kusoma game vizuri la Awamu ya tano.

One love.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua na kiosk changu mtaani tokea mwaka 2012, biashara ilikua nzuri japo changamoto hazikukosekana, average kwa siku nilikua nauza 90k - 120k, ila tokea 2016 biashara ilianza kushuka ilifika kipindi mauzo kwa siku unapata 30k ila nikajipa moyo hiki ni kipindi cha mpito baada ya miezi sita purchasing power ya watu itarudi waendelee kununua kwa sababu kuna siku inapita umeuza soda mbili tu, nilikomaa ila mwaka jana mwezi wa sita sikua na cha kufanya zaidi ya kufunga biashara, na stoo nilikua na bidhaa zingine, niliuza chache kwa jumla, nyingine nikagawa bure na nyingine ziliharibikia ndani, niliachia frem ikiwa na miezi miwili mbele!

Smh
 
Nina miaka 18 kwenye biashara katika kipindi chote hicho,Nimepitia milima na mabonde.” Yani changamoto” Kitu ambacho ni cha kawaida kwenye biashara yoyote.

Lakini leo nakiri kwamba, Awamu hii imeuwa juhudi za watu wengi kufikia malengo yao kibiashara, Biashara zimeyumba kabisa, Mauzo yameshuka kwa asilimia zaidi ya 70, huku mitaji mingi ya wajasiria mali ikiteketea.

Kinachoogopesha zaidi, Sioni juhudi zozote za makusudi kuokoa hali hii mbaya. Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku.
Lakini tukiwasikiliza viongozi wetu wanasema tupo pazuri. Najiuliza pazuri wapi?

Mwanzoni nilijua labda baba anafanyia nyumba usafi, Cha kushangaza tunamaliza miaka tano hali imekuwa tete zaidi ya tulipo toka.

Kuna hitajika jitihada za ziada kwenye uchumi wetu tena kwa speed kubwa la sivyo tutazalisha taifa la wamachinga na wapiga vibomu. Maana soon kodi za pango na serekali hazitalupika tena.

Natamani hii biashara yangu nimpe bure Dr mpango aiendeshe kwa miezi tu ili ajue hali halisi sio kukaa ofisini huku tukimlipa mshahara mnono bila kusaidia uchumi wetu.

Dr. Mpango mweleze rais hali mtaani ni mbaya,Watu tunapiga kazi asubuhi mpaka jioni lakini tunatoka kapa kila siku.

Halafu nimegundua ukiwa na hali mbaya mfukoni na majukumu ndio yanabisha hodi kwa kasi kweli kweli.

Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.
Acha kulalamika, unataka serikali ikufanyie nini ili mambo yako yaende, kwani nimekufunga jela, si bado una uhuru? Tatizo lipo wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasema ndinga kali. Ukiwa na 2017 Land Cruiser V8 unaweza kuwa masikini? Masikini utumie 300m kununua gari? Kuna gari kuwa na uwezo wa kuinunua lazima uwe tajiri achana na viusafiri vyetu akina sisi.
Nani kakwambia ndinga ni hilo v8 !!! Unaelewa maana ya ndinga ???

Huna unachokijua wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom