Kwa miaka 20 ya uongozi wa CHADEMA Manispaa ya Moshi imeshindwa kuwa Jiji, Jafo tuangalie kwa jicho la huruma!

Habari yafo mmeku?

Kumbe kwafo ni Usseri vaita?

Lakini usijali, hata wasipotangaza Moshi kuwa jiji, rais ajae ambae hatakuwa m baguzi na mkabila atatangaza tu.

Hivi nyie huwa mnakosa maneno ya kuongea!!! Moshi kweli liwe jiji!!!!


Sioni ajabu chadema kuongea haya maajabu 😁
 
Tengeneza kwanza Manispaa ya Rombo
Waache wenye Moshi yao
Kwahiyo hamtaki tena theluji ya Mlima Kilimanjaro iwepo? Kila sehemu ikiwa Manispaa itakuwa hatari Jamani ndiyo maana hata nyumba imegawanyika vyumba vyote haviwezi kuwa Master lazima kuwe na store sturdy room choo Umeelewa?
 
Mie hizo mavitu zenu sijui huwa zinzsaidia nini Dar imekuwa jiji miaka yote lakini ndo chafu kuliko mikoa yote mvua ya jero Dar ina simama lini ukasikia moshi ina mafuriko.
 
Na kwa taarifa yako Chato inaenda kuwa Jiji kabla ya Moshi

Ila nashauri Moshi iendelee kuhifadhi ukijani kuulinda mlima unafaida zaidi ya hao watu ma majengo mnayotaka ya badilishe jina kuwa Jii
Unadhani nitashangaa ..kwa serikali hii hakuna cha ajabu...kama korona wanasema ni changamoto ya upumuaji au mafua ya kubana kama JPM anavyosema.
 

Ili kamji ka moshi kakuwe angalau kuifikia Morogoro ama Shinyanga wakazi wa mule wanapaswa wagawe viwanja kwa wageni na sio kuyang'ang'ania wao kama wao wachagga, end of the day wanashindwa kuviendeleza.
 
Hivi jiji hupewa mkoa?
Au manispaa??

NISAIDIENI

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu,

Huwezi kuilinganisha Moshi na Mbeya kwa sababu zifuatazo

Moshi
1. Kijana wa Kilimanjaro akiondoka kwenda kutafuta maisha mikoani akifanikiwa huwekeza huko na mwisho wa mwaka anaenda Moshi kupumzika na kufanya matumizi ya kile alichokipata
2. Uwekezaji wa wenyeji wa Kilimanjaro ni wilaya za pembezoni kama Hai, Siha, Kibosho, Machame na Marangu ila mjini Moshi, Moshi vijijini na Rombo hakuna chochote cha maana;
3.Moshi mjini wamewekeza wahamiaji wa kutoka mikoa mingine
4.Machinga (biashara ndogo ndogo) Moshi mjini zinafanywa na akina mama
5. Wenyeji wakiwa Moshi mjini hawajivunii kuwa wako kwao

Mbeya
1. Mbeya imegawanyika maeneo matatu ambayo ni Uhindini, Mwanjelwa na Mbalizi
2. Wenyeji wa Mbeya wakienda mikoani na kufanikiwa hurejesha uwekezaji maeneo ya Mwanjelwa na Mbalizi
3.Wenyeji wakiwa Mbeya wanaona fahari kuwa hapo
4. Wenyeji wanaendesha shughuli za kiuchumi katika maeneo yaliyoanishwa hapo juu

TANBIHI: IDADI ya watu wenye asili ya Mbeya ni wengi hapo mjini lakini kwa Moshi mjini ni wachache na kwa kawaida hata kama anaendesha shughuli hapo mjini ikifika jioni anarudi milimani hivyo hapo mjini wanaoishi ni watu kutoka maeneo ya nje ya mkoa. Hata hivyo kwa namna moja ama nyingine wanafanana katika tabia ya kujibagua
i. Moshi wanatambuana huyu katoka Machame, Kibosho, Marangu, Uru, Old Moshi, Rombo nk
ii. Mbeya wanatambuana huyu katoka Kyela (goigoi kwa kazi za kujituma na wanajivuna), Tukuyu, Mwakaleli (Busokelo), Ileje, Mbozi, Chunya nk
iii. Idadi ya watu walioko Mbeya mjini ni kubwa ukilinganisha na Moshi mjini hivyo huduma nyingi kuhitajika

USHAURI
Ili Moshi mjini pawe na sifa za kuwa Jiji wanashauri kuishawishi serikali izungumze na mwekezaji wa kiwanda cha sukari TPC waachie maeneo ya mashamba ya miwa yaliyoko Fonga, Kikavu, Chekeleni kisha ifidiwe maeneo ya Mikocheni (Mijongweni), Kahe na kiasi fulani Msitu wa Tembo ili mji upanuliwe na wenyeji pamoja na watu wengine wenye mtaji kuwekeza shughuli za uzalishaji mali na huduma kukidhi vigezo
 
BIG CITIES ARE A BREEDING PLACE FOR SUFFERING AND INJUSTICE! ... I WONDER WHY TANZANIANS WANT CITIES EVERYWHERE!
 
Likewise miaka 50 ya uongozi wa CCM; taifa limeshindwa kumaliza tatizo la vyumba vya madarasa na madawati shule ya msingi.
 
Umenikumbusha Charles Njonjo aliyepata kuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Katiba nchini Kenya miaka hiyo.
Huyu bwana alipenda sana wazungu na uzungu kupindukia,kiasi akawa anawaponda nakuwadharau waAfrika.
Inasemekana siku moja alipanda ndege,kama kawaida majina ya rubani yalitajwa,na yote yalikuwa ya kizungu.
Baada ya ndege kutua Njonjo akawa anasifia jinsi rubani wa kizungu alivyotua kwa umahiri wa hali ya juu,lakini baada ya kuambiwa kuwa huyo rubani pamoja na kuwa na majina ya kizungu lakini ni Mkenya mweusi ghafla akabadili kauli eti kumbe ndiyo maana nimesikia mshtuko usiokuwa wa kawaida wakati tunatua!!!!!!.
 
Mji wa Moshi ulioko mkoa wa Kilimakyaro uwe jiji? Kwa hiyo kila kiongozi anayetokea eneo fulani apewe fadhila ya jiji hizo ni akili zenye tija?

Fufueni kiwanda cha vipuri na 'Kilimanjaro Machine Tools Manufacturers Ltd' haraka acheni longolongo.
Fufueni kiwanda cha ngozi 'Moshi Leather Industries Ltd)' & '(Himo Tanneries Ltd)'.
Fufueni kiwanda cha madawa ya kilimo 'Twiga Chemicals Ltd'. Fufueni kwanda cha mazao ya mbao ' Kiliwood Products Ltd)'.
Fufueni kiwanda cha voberiti ' Kibo Match Ltd'.
Fufueni kiwanda cha karatasi 'Kibo Paper Ltd'.
Fufueni kiwanda cha magunia 'Tanzania Packaging Manufacturers'.
Fufueni kiwanda cha kukoboa mpunga Kilimanjaro Paddy Hulling Co. Ltd''.
Fufueni kiwanda cha matunda Bella view Fresh Fruits Company Limited'.'
Acheni kupora eneo la mashamba ya kiwanda cha sukari kisha kujenga makazi yenye jina la nchi ya Marekani [New Land]
Acheni kubadili kijiji cha wafugaji cha Mserekia kwa kuvamia na kuanzisha makazi hatarishi kwa ustawi wa upanuzi wa mashamba ya miwa ya kiwanda cha TPC kwenda Kahe.

Badilisheni tabia za wakaazi wa maeneo ya PASUA, KIBORORONI, FONGA, CHEKELENI na MAJENGO ziwe za kiungwana na maadili mema.

Punguzeni kushobokea kuoa au kuolewa na wazungu kwa kuwinda mali zao-naishia hapo

Eneo la wilaya ya Same liko sawa na ukijumuisha wilaya za Siha, Hai, Rombo, Marangu, Moshi-Maajabu ya duni halafu wanalilia kuwa jiji wanaposhauriwa namna bora ya kuipata sifa hiyo wanakushobokea-Too pathetic

Kwa hiyo usinifyatukie wakati wala hauijui vizuri Kilimakyaro

Hakikisheni mji unarejeshewa baridi asili kama ilivyokuwa zamani.
 
Uhuru kamili kwanza kwa raia ndio mambo yajiji badaye. Itakusaidia nini ukiwa na jiji halafu unanira ya maksai shingoni.
 


Tangia msukuma aingie madarakani ni kelele tuuu zisizokuwa na maana. Mkuu, Eti hawa ndio wakupewa nchi kweli!!!! Na ndio maana miaka yote since Tanzania ipate uhuru haijawahi kuongozwa na hawa jamaa, tungekomaje!!! Heri ya mzungu ama mwarabu atuongoze lakini sio hawa.
 
Kuitwa jiji ni jina tu jengeni mji wenu
 
Kama maamuzi yenyewe ndio kama hayo yaliyofanywa kwa Ilala/Dar, wacha isiwe jiji tu. Kama Masaki, Mbezi, Beach Morocco, Mwenge ni sio sehemu ya jiji lolote hapa Tz, itakuwa Moshi?

......hayana chama!
 
The right message has nailed the hypocrites inside the din.

I acknowledge all the insults you flamed out to defend your personality which has assisted to expose the true colour as to how you are and how mentallyweak you are angrily pewing the heartbreak after being blatantly told the truth.

I neither have interest from Moshi and Mbeya nor do I expect to degrade you as you speculate to court around mob psychosis attention.

Please read while relaxed you may approriately discern the contents aimed to forge transformation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…