Mkuu
Unafeli mno,wewe na wenzako wa CCM
Bongo zenu by design politicians wanatumia short term thinking framework.
Wanasiasa short term thinking ndio thinking yao by design,ndio shida ya wanasiasa
Moshi unatakiwa uwe mji mdogo by design utumie eneo dogo mno ku-exist.
Kwa African standards unazotumia wewe,mji kua jiji unatakiwa uwe ume-cover bigger land area na ujinga mwingine mwingi na idadi kubwa ya watu na upumbavu mwingine mwingi sana
Moshi upo chini ya mlima,unatakiwa usikue zaidi ya hapo ili kuokoa huo mlima
Moshi inatakiwa iwe na idadi ndogo ya watu,itumie eneo dogo sana isiwe na systems nyingi za kuharibu mazingira
Ukijaza watu Moshi,wataharibu ardhi wapate makazi,wata-cover eneo kubwa zaidi,watapanda milimani kukata miti wapate makazi mji upanuke
Ni most definitely watapanda milimani zaidi kuliko bondeni kufata hali ya hewa...eneo litakua packed mno na ule mlima ndani ya miaka 20-30 utakufa kabisa
By design na makusudi makubwa,Moshi watu wazuiwe wasijae,watu waende miji mingine,Moshi kua JIJI kwa African standards ni kuua Mlima ambao ni world's heritage
Pamoja na kampeni mbali mbali za kuotesha miti na awareness mbalimbali tangu nikiwa mdogo mpaka leo mid 2000's Moshi ilikua kwenye brink ya kua jangwa na snow cap was the lowest ni its history
Leonidas Gama aliokoa that time kwamba ukitaka kukata tawi la mti shambani kwako ni lazima ukachukue kibali ofisi ya kata na ukikata makusudi unafungwa....Walao leo kuna vimiti somehow
Ukiwa rais wewe takataka utaharibu nchi nzima kwa euphoria ya stupid cities which do no make any sense in a long run.
Mkuu,
Huwezi kuilinganisha Moshi na Mbeya kwa sababu zifuatazo
Moshi
1. Kijana wa Kilimanjaro akiondoka kwenda kutafuta maisha mikoani akifanikiwa huwekeza huko na mwisho wa mwaka anaenda Moshi kupumzika na kufanya matumizi ya kile alichokipata
2. Uwekezaji wa wenyeji wa Kilimanjaro ni wilaya za pembezoni kama Hai, Siha, Kibosho, Machame na Marangu ila mjini Moshi, Moshi vijijini na Rombo hakuna chochote cha maana;
3.Moshi mjini wamewekeza wahamiaji wa kutoka mikoa mingine
4.Machinga (biashara ndogo ndogo) Moshi mjini zinafanywa na akina mama
5. Wenyeji wakiwa Moshi mjini hawajivunii kuwa wako kwao
Mbeya
1. Mbeya imegawanyika maeneo matatu ambayo ni Uhindini, Mwanjelwa na Mbalizi
2. Wenyeji wa Mbeya wakienda mikoani na kufanikiwa hurejesha uwekezaji maeneo ya Mwanjelwa na Mbalizi
3.Wenyeji wakiwa Mbeya wanaona fahari kuwa hapo
4. Wenyeji wanaendesha shughuli za kiuchumi katika maeneo yaliyoanishwa hapo juu
TANBIHI: IDADI ya watu wenye asili ya Mbeya ni wengi hapo mjini lakini kwa Moshi mjini ni wachache na kwa kawaida hata kama anaendesha shughuli hapo mjini ikifika jioni anarudi milimani hivyo hapo mjini wanaoishi ni watu kutoka maeneo ya nje ya mkoa. Hata hivyo kwa namna moja ama nyingine wanafanana katika tabia ya kujibagua
i. Moshi wanatambuana huyu katoka Machame, Kibosho, Marangu, Uru, Old Moshi, Rombo nk
ii. Mbeya wanatambuana huyu katoka Kyela (goigoi kwa kazi za kujituma na wanajivuna), Tukuyu, Mwakaleli (Busokelo), Ileje, Mbozi, Chunya nk
iii. Idadi ya watu walioko Mbeya mjini ni kubwa ukilinganisha na Moshi mjini hivyo huduma nyingi kuhitajika
USHAURI
Ili Moshi mjini pawe na sifa za kuwa Jiji wanashauri kuishawishi serikali izungumze na mwekezaji wa kiwanda cha sukari TPC waachie maeneo ya mashamba ya miwa yaliyoko Fonga, Kikavu, Chekeleni kisha ifidiwe maeneo ya Mikocheni (Mijongweni), Kahe na kiasi fulani Msitu wa Tembo ili mji upanuliwe na wenyeji pamoja na watu wengine wenye mtaji kuwekeza shughuli za uzalishaji mali na huduma kukidhi vigezo