Kwa miaka 4 iliyopita sijaona beki wa kati kama Rio Ferdinand

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Niwe muwazi na mkweli, toka kustaafu kwa beki wa kati wa zamani wa Man Utd, Leeds United, QPR na timu ya taifa ya England bado sijaona beki wa kariba yake barani Ulaya.

Rio ni miongoni mwa beki bora wa kati kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuusoma mchezo, utulivu mkubwa, ball control bila kusahau matumizi makubwa ya akili licha kutobalikiwa nguvu lakini haikuwa rahisi kumpita huyu jamaa.

Niseme tu, nimeangalia mabeki wengi wanaotamba kwasasa barani Uropa bado sijaona beki anayemkaribia Rio Ferdinand katika nafasi ya beki namba 5. Pia Rio ni beki kiongozi pale nyuma kwani huweza kuwapanga wenzake vyema.
Refer magoli mawili waliyofungwa Man City jana kwa uzembe wa ukuta wao.

Povu ruksa.
 
Hadi Yesu anarudi hatatokea beki wa kati kama Alessandro Nesta. Ronaldo de lima, Ronaldinho, Messi, Cr7 hao wote hawakuwahi kumpita huyo jamaa. Unamzungumzia huyu Ferdinand aliyeburuzwa na Mchezaji Ricardo Kaka kama mtoto mechi Ac Milan na Manchester United old Trafford hadi wanapandiana mgongoni na mwenzie kama vichaa. Tafuta clip uangalie Nabii Gaucho anampiga kanzu Nesta then Nesta anaivua kanzu kwa kisigino, wakati huo Gattuso anapigwa vyenga anatambaa kama mtoto. Dinho anapiga goli dk ya 88 anawapiga chenga Khaka Kaladze na Nesta inaitwa Back and away ( Mpira unachapwa kofi upande wa kulia alafu unaamia upande wa kushoto huku Nesta na Kaladze wakiamini mpira ule Nabii Dinho anaingia nao upande wa kushoto. Mtukufu Ronaldinho anaupiga kwa shuti la mguu wa kushoto huku kipa Dida akishindwa kuufata mpira ule. Mm mwenyewe Juve damu ila ile Milan ilikua balaa jamani. Ukuta ulijengwa na Paul Maldini, Nesta,Kaladze, Cafu, Jaap Stam,
 
Umeongea mengi sana na nimekufananisha na muimba taarabu.

Ni lini Rio alipigwa chenga hiyo na kaka?
Au Rio Ferdinand wa huko kwenu Kibaigwa?
 
Mkuu nadhani hujamuelewa mleta maana anakwambia kwa miaka minne iliyopita..
We unaanza ku refer Nesta na Ronaldinho.
 
Beki zipo italy wewe peleleza.. uone shughuli ya kina cannavaro enzi zao.. huyo nesta bonge ya cb
 
Alikuwa mzuri ila sio the best, na mwisho wake ulikuwa mbaya alikuwa anatoa maboko mno. Namkubali Gerald Pique na Puyol, combi yao ilikuwa tamu sana hawatumii nguvu wanatumia akili
 
Umeongea mengi sana na nimekufananisha na muimba taarabu.

Ni lini Rio alipigwa chenga hiyo na kaka?
Au Rio Ferdinand wa huko kwenu Kibaigwa?
Da watu wanachuki hadi wanaamua kutengeneza tukio la uongo apunguze wivu ndugu kaka alimpiga chenga heinz na patric evra tena evra akiwa mdogo sana akitokea monaco mishabik ya tanzania ina hasira sana
 
Beki zipo italy wewe peleleza.. uone shughuli ya kina cannavaro enzi zao.. huyo nesta bonge ya cb
Hata england kulikuwa na mabek mjomba huwezi kumuacha john terry na vidic hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…