Kwa miaka 5 Magufuli alikopa Trilioni 36, kwa miezi 6 Mama amekopa Trilioni 10, Ndugai yuko sahihi, spidi ya kukopa ni kubwa sana.

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Kwa miaka 5 na miezi kadhaa, yaani kuanzia 2015 hadi March 2021 Magufuli amekopa kiasi cha Trillioni 36, kwa wastani wa Trillioni 7 kwa mwaka.

Magufuli amefariki March 2021 Deni la Taifa liko Trillioni 72. Kwa muda wa miezi 9, yaani kuanzia March 2021 hadi December 2021 deni la Taifa ni Trillioni 82, kwa maana kwamba kwa miezi 9 mama amekopa Trilioni 10.

Tukienda kwa kasi hii ya mikopo, miaka 4 ijayo mama atakopa Trillioni zaidi ya 50 na kufanya deni la Taifa kufikia Trilioni 120 ama zaidi mwaka 2025.

Ndugai yuko sahihi, spidi ya kukopa ni kubwa sana. Mama hataki kuangalia vyanzo vipya vya kodi, yeye anakimbilia the easy way out, kukopa, kukopa na kukopa.

Hii nchi miaka 60 ya uhuru tunakopa kujenga madarasa, kujenga vyoo kweli? Hata hilo la ujenzi wa vyoo vya shule tunahitaji kukopa? Tukope kufanya vitu vya msingi.

Kuna watu wasema mama ameleta uwazi wa matumizi ya mikopo sio kama Magufuli, naomba tuulizane, kwenye hizo Trillioni 10, tumetangaziwa matumizi ama mgawanyo Trillioni ngapi? Si hizi 1.5 za covid tu za ujenzi wa madarasa? Nyingine 8.5 tunajua zimetumika wapi?
20211229_190124.jpg
 
Kwa miaka 5 na miezi kadhaa, yaani kuanzia 2015 hadi March 2021 Magufuli amekopa kiasi cha Trillioni 36, kwa wastani wa Trillioni 7 kwa mwaka.

Magufuli amefariki March 2021 Deni la Taifa liko Trillioni 72. Kwa muda wa miezi 9, yaani kuanzia March 2021 hadi December 2021 deni la Taifa ni Trillioni 82, kwa maana kwamba kwa miezi 9 mama amekopa Trilioni 10.
ingependeza ungetuwekea na matumizi ya hiyo mikopo ili tuone kama ina tija kwa taifa letu. Hata sisi wachumia tumbo hukopa na kwenda kutamba kwenye viti virefu kwa 'Faru Johnney' ambapo wajanja hujenga nyumba.
 
Kama kuna wakati ambapo tusingepaswa kusimuliwa kuhusu mapato & matumizi, basi ni wakati wa awamu ya JPM. In short, kazi inaonekana. ^HAPA KAZI TU!^

^Ukijumlisha miaka yetu 30 yote, mwenzetu yeye ametuzidi kwa miaka yake mitano tu^ ~ Ukweli Mchungu wa Mzee Ruksa.

#^Car-taaWar-who-kneeCar-bee-sir!!!^
 
Deni la taifa bado ni himilivu....

Profesa Luoga amefafanua kitaalamu kuwa hatujafika hata nusu ya asilimia 70 ya "cap" ya kukopa.....

#Siempre JMT[emoji120]
#Siempre SSH[emoji120]
Wahuni mnafaidi hii mikopo sio bure
 
Deni la taifa bado ni himilivu....

Profesa Luoga amefafanua kitaalamu kuwa hatujafika hata nusu ya asilimia 70 ya "cap" ya kukopa.....

#Siempre JMT[emoji120]
#Siempre SSH[emoji120]
Au sio
 
Uongo Mtupu,Mama fedha alizokopa ni zile T1.3 ambazo matumizi yake tumeyaona.Rais aliekopa kuliko Marais wote ni Jiwe na hilo liko wazi.
 
Ungetoa mchanganuo wa jinsi Samia alivyokopa hizo Trilioni 10 ingekuwa vizuri zaidi kwasababu Mama amekuja na style mpya ya uwazi wa Fedha anazokopa na matumizi yake. Hata hivyo, Deni linakuwa la hatari zaidi kama linakopwa kwa commercial terms (non concessional loans). Magufuli alifanya hivi kutoka Credit Suisse bank na Standard Chartered Bank. Pure commercial loans zina riba kubwa na ya muda mfupi. Lakini pia kuchukua kwake hakutegemei saaana DSA ya nchi.
 
Wahuni mnaparuana wenyewe sasa. Oooh wapinzani wanatuchelewesha. Sasa mko wenyewe naona hamtodheki.
 
mama anafungua nchi kama clouds wanavyofungua dunia[emoji16][emoji16]
 
Kazi ya bunge ni kuishauri na kuidhibiti serikali...yeye kama spika wa bunge kwanini asitumie mamlaka ya chombo chake kuishauri serikali .? Sasa anapokuja kulalamika kwenye vyombo vya habari maana yake bunge lake halina meno?halina mamlaka? Au hajui majukumu yake?
 
Kwa miaka 5 na miezi kadhaa, yaani kuanzia 2015 hadi March 2021 Magufuli amekopa kiasi cha Trillioni 36, kwa wastani wa Trillioni 7 kwa mwaka.

Magufuli amefariki March 2021 Deni la Taifa liko Trillioni 72. Kwa muda wa miezi 9, yaani kuanzia March 2021 hadi December 2021 deni la Taifa ni Trillioni 82, kwa maana kwamba kwa miezi 9 mama amekopa Trilioni 10.

Tukienda kwa kasi hii ya mikopo, miaka 4 ijayo mama atakopa Trillioni zaidi ya 50 na kufanya deni la Taifa kufikia Trilioni 120 ama zaidi mwaka 2025.

Ndugai yuko sahihi, spidi ya kukopa ni kubwa sana. Mama hataki kuangalia vyanzo vipya vya kodi, yeye anakimbilia the easy way out, kukopa, kukopa na kukopa.

Hii nchi miaka 60 ya uhuru tunakopa kujenga madarasa, kujenga vyoo kweli? Hata hilo la ujenzi wa vyoo vya shule tunahitaji kukopa? Tukope kufanya vitu vya msingi.
View attachment 2063295
Mbaya zaidi atatuachia deni wakati wa kulipa yeye atakuwa ametulia zake Pemba
 
Kazi ya bunge ni kuishauri na kuidhibiti serikali...yeye kama spika wa bunge kwanini asitumie mamlaka ya chombo chake kuishauri serikali .? Sasa anapokuja kulalamika kwenye vyombo vya habari maana yake bunge lake halina meno?halina mamlaka? Au hajui majukumu yake?
Ndugai ni chizi
 
Back
Top Bottom